SORRY MADAM (7)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (7)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Baba akanipa simu mbele ya mwalimu wa nidhamu japo sheria za shule haziruhusu mwanafunzi kuwa na simu “Sasa Eddy uwe makini na simu yako ili waalimu wengine wasiione wakakupokonya kwa mimi ninakuruhusu kuwa nayo” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Mwalimu wa nidhamu alizungumza huku akiwa anajichekesha chekesha baada ya kupewa laki moja na baba ila sikujua ni ya nini.Baba akaniombea ruhusa ya kwenda na mimi nje ya shule.Baada ya kuipata ruhusa hiyo tukaondoka shule na kwenda katika hoteli moja iliyopo karibu na shule.Tukanunua chakula tukiwa na dereva wa baba tukaanza kula huku mara kwa mara mzee akinihusia kusoma kwa juhudi huku akinipondeza kwa kumbishia mwalimu “Wale waalimu wenu wanaonekana wana tabu sana.Ila wakikuzingua kwa kosa ambalo utaona hawakutendei haki wewe wazingue.Ila wakiniletea kesi ambayo ni ya kijinga jinga kama umekamatwa na demu sijui umegoma kufanya mtihan…