SORRY MADAM (119)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (119)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA TISA ILIPOISHIA... Nikatoka nje huku machozi yakinimwagika. Phidaya akanifwata kwa haraka baada ya kuniona ninatokwa na machozi mfululizo “Baby kuna nini?” “Mama anakufa” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Phidaya kwa haraka akaingia ndani ya chumba cha mama na kuufunga mlango, Shamsa akamchukua Junio na kumpeleka nje, kwani hakustahili kuendelea kushuhudia matukio yanayo endelelea kwa muda huu, ukitegemea kwamba umri wake bado ni mdogo sana. Blanka naye akaanza kutokwa na machozi, akanifwata na kunikumbatia “Ohhh Mungu saidia mama yetu apone, kwa nini inakuwa ni hivi jamani?” Blanka alizungumza huku akiwa ameendelea kunikumbatia, machozi yakimwagika. Tukaendelea kusubiri nje kwa muda mrefu pasipo Phidaya wala doka Angelina kutoka nje. Wasiwasi juu ya kifo cha mama ukazidi kunipanda, mara kadhaa nilihitaji kwenda kuufungua mlango ili kutazama hali ya mama ila Blanka alinizuia akinio…