SORRY MADAM (62)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SITINI NA MBILI ILIPOISHIA... Uzuri wa gari hili,unaweza kutumia mfumo wa ‘ MANUEL ’ au ‘ AUTOMATIC ’ katika uendeshaji wake.Nikabadilisha mfumo kutoka Automatic hadi Manuel ambayo inaniruhusu kuingiza gia mimi mwenyewe tofauti na automatic gia zinajiingiza zenyewe. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Kwa kioo cha pembeni nikalishuhudi gari la polisi likikunja kona kwa bahati mbaya likazima na dereva akawa na kazi la kuliwasha “Muombeni mkuu wenu awanununulie magari mapya” Nilizungumza huku nikiiachia breki na kuondoka kwa kasi.Namba za mbele na nyuma ya gari langu nikazigeuza kwa kuminya kitufe kinachofanya kazi hii ya kuzibadilisha namba hizi za gari.Sikupanga kurudi Dar es Salaam leo ila ikanibidi kufanya hivyo kwani tayari Arusha nimesha haribu hali ya hewa.Nikafika Moshi na kuendelea na safari yangu,gafla nikaona gari mbili nyeusi zikinifwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi “Nani hawa?” Zikazidi kunifw…