SORRY MADAM (63)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (63)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SITINI NA TATU ILIPOISHIA... Mzee Godwin akajishika kichwa na kuzunguka mara mbili huku akisunya misunyo mkali “Nitamuua Eddy leo mbele yako” Mzee Godwin alizunguza na kuanza kupiga hatua za kuingilia kwenye mlango wa sebleni.Kabla sijafanya kitu chochote nikastukia nikishikwa kwa nyuma na kuzibwa mdomo NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “Shiii” Ilikuwa ni sauti ya kike,mwanamke aliye nishika kwa nyuma akaanza kunivuta kwa nyuma huku tukielekea gizani.Tukatokea upande wa pili wa nyumba kwenye miti mingi,ndipo nikagundua mtu aliye nishika ni yule dada aliyekuwa ameniletea chakula “Kimbia kabla kifo hakija kukuta hapa” Msichana alizungumza,huku akiwa amenitazama kwa macho makali, “Asante” “Amina ninaitwa” “Eddy” “Ninakujua,haya nenda” Nikaanza kujikaza na kutokomea porini,Japo mara kwa mara ninaanguka ila nikazidi kujikaza na kwenda mbele,Giza likatawala anga na sikujua ni wapi nielekeaa,nikajiegemeza kweny…