SORRY MADAM (64)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SITINI NA NNE ILIPOISHIA... Nikafanya kama Dorecy anavyo niagiza,gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Macho yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na sehemu tulipo simama, Nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, Kitendo cha kukunja tu, bomo alilo lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo …