SORRY MADAM (67)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (67)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SITINI NA SABA ILIPOISHIA... Kwa ukubwa wa gari yangu haikuwa shida sana kuzikanyaga pikipiki mbili zilizopo mbele yangu. Nikapata kiupenyo cha kuingia barabarani na cakumshukuru MUNGU, hakuna magari ya foleni ambayo yanaweza kunizuia kuendelea na safari yangu, huku nikiwaacha waendesha pikipiki wakitoa matusi mengi juu yangu NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Kwa mbali nikaliona gari, walilokuja nalo majambazi likichanja mbuga barabara ya kuelekea mkoani “Wale ndio majambazi walio piga tukio benki” Nilizungumza huku nililiinyooshea kidole gari la majambazi aina ya Rangerover . “Mmmmm” Dorecy aliguna, huku akinitazama machoni.Nikazidi kukanyaga mafuta na kuzidi kulisogelea majambazi, ambalo nalo linakwenda kwa mwendo wa kasi sana “ Eddy kuwa makini, wasije wakatushambulia” “Powa” Sikuona gari yoyote ya polisi inayokuja nyuma yetu, Nikazidi kulifukuzia gari la majambazi na gafla likakunja na kuingia porin…