SORRY MADAM (70)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SABINI ILIPOISHIA... Moyo ukaanza kunienda mbio huku mapigo ya kawaida yakibadilika na kuwa ya kasi sana kiasi kwamba nikaanza kujihisi vibaya “Ahh….haaa sio mimi?” Wakanitazama kwa umakini “Samanani ninaomba niende msalani” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikawaaga na kunyanyuka, nikatamani kutoka nje ya baa ila macho yao yote tapo kwangu, nikamuuliza muhudumu ni wapi kilipo choo, akanielekeza na bahati mbaya kipo ndani ya baa hii na kama kingekuwa ni nje ingekuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuwakimbia.Nikaingia chooni na kusimama kwenye moja ya kioo kilichomo humu ndani, nikaivua kofia yangu na kujitazama vuzuri “Sijabadilika chochote usoni mwangu” Nilizungumza kwa sauti ya chini, nikajiweka sawa na kuivaa kofia yangu na taratibu nikaanza kuelekea ulipo mlango, nikakishika kitasa cha mlango huku nikiwa ninahema sana, nikashusha pumzi nyingi na kuufungua mlango, nikapiga hatua mbili, gafla nikastukia…