SORRY MADAM (72)

Zephiline F Ezekiel
SEHEMU YA SABINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Wakaendelea kuzungumza huku mmoja akiandika kwenye kijikitabu kidogo alicho kuja nacho.Mmoja akanifunua shuka na kumuonyesha mwenye kijikitabu mkononi sehemu ya mguu wangu, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuuona mguu wangu wa kulia ukiwa umefungwa kitu kikubwa cheupe.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Akaingia nesi wa jana usiku na kusimama pembeni ya madaktari hawa, huku akiwa ameshika kisinia chake cha jana usiku.Nikaanza kumuona nesi akitingisha kichwa akionekana kukataa mazungumzo ya madaktari hao
Wakaanza kubishana, na sikujua ni kitu gani wanacho bishana.Hadi ikafikia daktari mmoja wa aliyekuwa anazungumza na mwenzake anaandika akataka kumzaba kibaa nesi huyo, ila mwenzake akakataa na kumtoa nje, kuepusha ugomvi kutokea ndani ya chumba hichi.Nesi akaanza kuzunguka ndani ya chumba huku akimwagikwa na machozi na kuzidi kunichanganya kwani sikujua ni kitu gani kinacho mwaga machozi kwa kiasi hichi.
“Kuna nini?”
Nilimuuliza na kumfanya asimame na kunitazama, akautazama mlango na kwenda kuufunga kwa ndani, kisha akarudi na kukaa pembeni yangu huku akinifunika na shuka
“Eti nesi, kuna nini?”
Nilimuuliza kwa sauti ya upole iliyo jaa huzuni, akanitazama na machozi yakazidi kumwagika kiasi cha kuzidi kunichanganya mimi
“Watu wa huku, wana roho mbaya sana pale wanapo waona watu wenye ngozi yeupe”
Alizungumza huku akijifuta machozi yanayo mwagika kwa kutumia kiganja chake
“Kwa nini?”
Akanitazama kwa umakini na kwamacho yaliyo jaa huzuni kiasi cha kunifanya nihisi kuna jambo baya ila sikujua ni nini
“Kiufupi hawawapendi watu weusi, ndio maana wanafanya mpango wa kukukata huu mguu wako ulio vunjika”
Nilijihisi moyoni mwangu kama nimepigwa shoti ya umeme, kila nilivyo mtazama nesi sikujua nizungumze nini.Machozi yakaanza kunimwagika kama maji,
“Usilie, nitahakikisha unapona na hakuna mtu anaye weza kukufaniyia ukatili kama huo”
“Kwani umekatika?” Nilimuuliza kwa sauti ya upole sana huku nikiendelea kulia
“Hapana haujakatika, umefunjika mara mbili, ila nashangaa ni kwanini hapa wanapanga kuukata”
“Ila usilie, nipo radhi nipoteze kila kitu kwangu, ila si kukubali kuuona ubaguzi wa rangi kama huu.Kwa maana wakiukata kinacho fwatia hapa ni wewe kupelekwa katika kambi ya walemavu iliyopo Bangdad na kila siku hiyo kambi, walemavu wanakufa kwa njaa kali na mateso makali, na mbaya zaidi wengi wanao pelekwa kule ni wale ambao si raia wa nchi hii”
Maneno ya nesi yakazidi kuniogopesha na kuendelea kunipa wasiwasi mkubwa ulio zidi kunimwaga machozi yangu.
“Jikaze usilie, ngoja nikuchome sindano ya kutuliza maumivu na kukausha kidonda.Wakikuletea chakula tafadhali usile hadi nikuletee mimi”
“Sawa”
“Wanaweza kukupa sumu, ufe bure mtoto wa watu bila ya sababu maalumu”
Nesi alizungumza na kuendelea kunichoma sindano alizo niambia,
“Sasa hivi ninatoka, kazidi ninakwenda nyumbani kukuandalia chakula, hadi saa sita nitakuwa nimesha rudi kukuletea chakula na nikija nitakuja tuzungumze mengi.Ila vumilia njaa yako, usile chakula wala kunywa maji yoyote utakayo letewa na mtu wa aina yoyote sawa”
“Sawa, nashukuru kwa msaada wako nesi”
“Hata wewe nashukuru kwa uelewa wako, niite neshi Phidaya”
“Naitwa Eddy”
“Mungu mkubwa utapona na vua hiyo mashine”
Nikakivua kifaa nilicho kuwa nimevalishwa kwenye uso kisaha, nesi Phidaya akaondoka na kila kitu chake, baada ya muda kidogo akaingia nesi akiwa amebeba sahani nyenye chakula pamoja na maji kwenye glasi, akaviweka pembeni ya meza yangu na kunitazama usoni.Akawa anatamani kuzungumza na mimi ila anashindwa na nikahisi lugha zetu zipo tofauti sana.Akanza kunionyesha kivitendo kwamba chakula kipo mezani ninaweza kula, na mimi nikamjibu kivitendo kwamba nitakula, akatoka na kuniachia chakula mezani. Harufu ya chakula ikazidi kunitamanisha kuweza kukila kwani inavutia sana, ila kila nilipo jaribu kukumbuka maneno ya nesi Phidaya nilijikuta nikuwa ninakidharau
Baada ya muda mrefu kidogo nesi Phidaya akarudi akiwa emeshika mfuko mweupe wenye vyombo,
“Nani kakuletea chakula?”
“Nesi mmoja mfupi, mwarabu”
Nesi Phidaya akaachia msunyo mkali baada ya kumuambia nesi aliye niletea chakula hicho
“Ndio wale wale”
Akakisogeza chakula nilicho letewa akaniwekea chakula chake mezezani, akaanza kuninywesha taratibu uji alio uweka kwenye kikombe
“Watu wa huku hawana ubinadamu, ndio maana kila siku wanakazi ya kujitoa muhanga na mabomu yao”
“Hivi ni kwa nini?”
“Uchizi tu ndio unao wasumbua, kuna wanao amini kwamba ukijitoa muhanga, mbele za watu mbinguni utaingia moja kwa moja wakati ni uongo mtupu”
“Hivi unakumbuka kitu chochote cha nyuma?”
“Hapana”
“Ona sasa, wamekuchoma sindano ya kukupotezea kumbu kumbu, ndio maana nakuambia watu wa huku hawana maana”
“Wamenichoma sindano?”
“Ndio, na kuna kitu kinacho endelea, na ile siku ya oparesheni kama nisinge kuwepo ninaimani wangekumalizia, nikutokana katika watu walio okolewa wakiwa hai kwenye lile jingo wewe ni mmoja wao na idadi kubwa ya waarabu walikufa pale”
“Kwenye jengo, jengo gani?”
“Usiwe na haraka, hapa itabidi nifanye mpango wa kukutorosha la sivyo watakupoteza”
Maneno ya nesi Phidaya yakazidi kunipotezea imani moyoni mwangu na kunijaza moyo wa woga kwani imani ya kuwaamini madaktari wengine ikaanza kunipotea moyoni mwangu.Nesi Phidaya akamaliza kunilisha chakula alicho niletea na kunihaidi atarudi usiku kisha akaondoka zake
***
Masaa yakazidi kusonga, huku moyoni mwangu nikiomba sana nesi Phidaya atokee aje kunisaidia kwa maana kila daktari kwangu sikuweza kumuamini, kila nilipojaribu kuvuta subira sikuweza kumuona nesi Phidaya akiingia kwenye chumba change, mlango ukafunguliwa na kujikuta nikianza kutabasamu, macho yangu yakiwa na shauku ya kuweza kumuona nesi Phidaya.Nikashangaa kuwaona wale madaktari wa asubuhi wakiingia na kusimama pembeni yangu
Mmoja akafungua kitabu chake kilicho andikwa na maandishi ambayo akanionyesha na sikumuelewa ni maandishi ya lugha gani, akaniandikia tarehe kwenye kijikitabu chake na kuniambia kwamba hii ni tarehe ya leo, kish akaniandikia tarehe nyingine ambayo ni siku inayo fwata.Kisha akachora kijimguu na kukiwekea alama ya ‘X’ akiashiria kwamba kesho ndio siku ya mimi kukatwa mguu wangu.Alipo maliza kunionyesha kwa ishara wakatoka huku wakiwa wanacheka sana.
Hadi kunapambazuka sikuweza kumuona nesi Phidaya, hali ya hatari ikaanza kunijia kichwani mwangu na kuhisi nesi Phidaya anaweza kuwa amekutwa na matatizo, mlango ukafunguliwa na wakaingia manesi wawili pamoja na madaktari wale wawili.Wakaanza kufungua kitandana na kukishusha chini kidogo hadi kikafikia usawa mzuri wa kuweza kusukumwa.Pasipo hata ya kunisemesha wakaanza kunisukuma na kunipeleka nisipo pajua huku nyuso zao zikiwa na tabasamu ambalo sikuliewewa nini maana yeke

WAKAZIDI KUKISUKUMA KITANDA NILICHO LALIA HADI HADI TUKAFIKA KWENYE MAJA YA MLANGO AMBAO JUU KUNA MAANDISHI YA KIHARABU AMBAYO SIKUWEZA KUYAELEWA, NESI MMOJA AKAUSUKUMA MLANGO NA KUFUNGUKA, NA WAKANIINGIZA NDANI NIKIWA JUU YA KITANDA CHANGU, MWANGA MWEKUNDU WA TAA ULIOO NDANI YA CHUMBA UKAZIDI KUNIOGOESHA.CHUMBA KIZIME KIMEZUNGUKWA NA MASHINE MBALIMBALI AMBAZO SIKUJUA ZINAKAZI GANI.DAKTARI MMOJA AKACHUKUA MASHINE YENYE KIMVIRINGO MBELE, KISHA AKAKIWASHA NA KUANZA KUZUNGUKA, AKACHUKUA MOJA YA MIWANI KUBWA AMBAYO NI NYEUPE AKAIVAA NA KUANZA KUCHEKA KITU KILICHOO ZIDI KUNIOGOPESHA ZAIDI.

GAFLA TAA YA MWANGA MWEUE IKAWASHWA NA KUWAFANYA MADAKTARI NA MANESI, KUSTUKA, MACHO YETU WOTE TUKAYAELEKEZEA MLANGONI NA KUMUONA NESI PHIDAYA AKIWA AMESHIKA, BASTOLA HUKU JASHO JINGI LIKIWA LINAMWAGIKA USONI, AKAANZA KUZUNGUMZA KWA KIARABU NA TARATIBU MADAKTARI WAKANYOOSHA MIKONO JUU WAKITETEMEKA, AKAZUNGUMZA NENO LILILO WAFANYA MADAKTARI KUANZA KURUDI NYUMA KUTOKA KILIO KITANDA CHANGU.
“EDDY, WAMEKUFANYA CHOCHOTE KIBAYA?”
“HAPANA”
“POWA”

NESI PHIDAYA AKAZUNGUMZA NENO JENGINE LILILOWAFANYA MADAKTARI NA MANESI KULALA CHINI, SAKAFUNI HUKU MIKONO YAO WAKIWA WAMEIWEKA JUU YA VICHWA VYAO.NESI PHIDAYA AKANIFWATA HADI KITANDANI NA KUUITISHA MKONO WAKE MMOJA KWENYE, MGONGO WANGU NA KUNIOMBA NIWE KUSHUKA CHINI, JAPO NINAJIHISI MAUMIVU ILA NIKAJIKAZA KIUME KWANI KUENDELEA KUKAA HAOA KUTAHATARISHA MAISHA YANGU.
“JIKAZE BABA YANGU”

NESI PHIDAYA ALIZUNGUMZA HUKU AKIENDELEA KUNISHUSHA KWENYE KITANDA, AKANISAIDIA KUSIMAMA VIZURI, HUKU MUHIMILI WANGU WOTE WA KUSIMAMA NIKIUTEGEMEA KUTOKA KWAKE, NESI PHIDAYA AKAWATAZAMA WATU MADAKTARI WALIO LALA CHINI, AKAZUNGUMZA NENO LA UKALI LILILO WAFANYA MADAKTARI NA MANESI KUZIDI KUZIFUNIKA SURA ZAO CHINI PASIPO KUZINYANYUA JUU. TUKAFANIKIWA KOTOKA NJE YA CHUMBA WALICHO NIINGIZA, NESI PHIDAYA AKAFUNGA MLANGO KWA NJE NA SOTE TUKAANZA KUONDOKA TARATIBU HUKU NESI PHIDAYA AKIIFICHA BASTOLA YAKE NA BAADHI YA WAHUDUMU WAKABAKI WAKIWA WANATUSHANGAA.TUKATOKA NJE NA KUKUTA GARI AINA YA TAKSI IKIWA INATUSUBIRIA
“AHAAAA”
NILITOA MGUNO WA MAUMIVU BAADA YA MGUU WANGU NILIO VUNJIKA KUGONGWA KWENYE MLANGO NILIPOKUWA NINAJIAANDAA KUINGIA NDANI YA GARI, SITI YA NYUMA
“POLE EDDY”
“ASANTE”

NESI PHIDAYA AKANISAIDIA KUINGIA NDANI YA GARI NA KUFUNGA, KISHA YEYE AKAINGIA KWENYE SITI YA MBELE KWA DEREVA NA KUMUONGELESHA DEREVA KIARABU NA AKALIONDOA GARI LAKE KWA KASI.
“ASANTE SANA, NESI PHIDAYA”
“USIJALI NIPO KWA AJILI YAKO, ILA NINGEPENDA UNIITE PHIDAYA TU NA SI NESI PHIDAYA”
“SAWA”

NIKAENDELEA KUJILAZA KWENYE SITI YA NYUMA YA TAKSI TUIYO IPANDA, ILA KUNA MWANGA MKALI WA TAA UKAWA UNAINGIA KWENYE GARI LETU, IKANILAZIMA KUNYANYUA KICHWA CHANGU KUTAZAMA NYUMA, NIKAONA GARI NDOGO IKIJA KWA KASI SANA,
“PHIDAYA KUNA WATU WANATUFWATA NYU……”
KABLA SIJAMALIZIA SENTESI YANGU NIKASTUKA RISASI IKIPIGA KWENYE KIOO CHA NYUMA NA KUNIFANYA NIRUDI CHINI, NA KULALA KWENYE SITI YANGU.DEREVA AKAANZA KULALAMIKA, NA PHIDAYA AKAANZA KUMUHIMIZA DEREVA KUONGEZA MWENDO KASI WA GARI,RISASI ZIPATAZO NNE ZIKAINGIA KWENYE KIOO CHA NYUMA CHA GARI NA KUSHANGAA RAGI IKIAANZA KUYUMBA HUKU DEREVA AKIWA AMEULALIA MSKANI WAKE,

“SHIT DEREVA AMEPIGWA RISASI YA KICHWA”
PHIDAYA ALIZUNGUMZA KWA KUCHANGANYIKIWA KIASI KWAMBA NA MIMI NIKAANZA KUCHANGANYIKIWA, RISASI ZIKAENDELEA KUMIMINIKA NDANI YA GARI NA KUZIDI KUNICHANGANYA
“MTOE HUYO DEREVA”
NILIZUNGUMZA KWA SAUTI YA JUU, PHDIAYA AKAFANYA KAMA NILIVYO MUAGIZA, AKAUFUNGUA MLANGO WA DEREVA NA KUMSUKUMIA KWA NJE, KISHA AKAFUNGA MLANGO NA KUKAA KWENYE SITI YA DEREVA
“NIPE BASTOLA YAKO”

PHIDAYA AKANIRUSHIA KWA NYUMA BASTOLA YAKE, NIKAUCHUKUA MKANDA WA SITI WA SITI YA NYUMA NA KUANZA KUUVUTA NIKIJARIBU KUUKATA ILA NIKASHINDWA.NIKAMTAZAMA
“EDDY UNATAKA KUFANYAJE?”
“NATAKA KUKATA HUU MKANDA NIUFUNGE MGUU WANGU UNAVUTA SANA”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni