SORRY MADAM (72)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (72)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SABINI NA MBILI ILIPOISHIA... Wakaendelea kuzungumza huku mmoja akiandika kwenye kijikitabu kidogo alicho kuja nacho.Mmoja akanifunua shuka na kumuonyesha mwenye kijikitabu mkononi sehemu ya mguu wangu, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuuona mguu wangu wa kulia ukiwa umefungwa kitu kikubwa cheupe. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Akaingia nesi wa jana usiku na kusimama pembeni ya madaktari hawa, huku akiwa ameshika kisinia chake cha jana usiku.Nikaanza kumuona nesi akitingisha kichwa akionekana kukataa mazungumzo ya madaktari hao Wakaanza kubishana, na sikujua ni kitu gani wanacho bishana.Hadi ikafikia daktari mmoja wa aliyekuwa anazungumza na mwenzake anaandika akataka kumzaba kibaa nesi huyo, ila mwenzake akakataa na kumtoa nje, kuepusha ugomvi kutokea ndani ya chumba hichi.Nesi akaanza kuzunguka ndani ya chumba huku akimwagikwa na machozi na kuzidi kunichanganya kwani sikujua …