SORRY MADAM (75)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SABINI NA TANO ILIPOISHIA... Nikiwa nifikiria cha kufanya nikastukia kitu kigumu kikinigusa kichwani mwangu, na kusikia sauti ya mwanaume ikiniamrisha nilale kama nilivyo na nisifanye kitu chochote la sivyo atauchangua ubongo wangu, taa kubwa lenye mwanga mkali likageukia sehemu ya sisi tulipo, juu ya ukuta na kuwafanya Khalid , Dorecy na watu wake kutuona. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Na Khalid akaagiza mtu huyo kunishusha kwenye ukuta. Nikashusha pumzi taratibu, jamaa akanigusa tena na ndunduki yake kwenye kichwa changu na kuniamrisha kushuka kwenye ukuta, kwa haraka sana nikajigeuza na kuichota miguu yote ya mtu huyo na kumfanya aangukie ndani kama mzigo wa kuni, nikajirusha na kuangukia nje ya sehemu ambayo nimetokea, cha kumsukuru Mungu sijaumia sehemu yoyote ya mwili wangu ambayo itanizuia mimi kukimbia.Nikanyanyuka haraka na kuhakikisha bastola yangu ipo sehemu nilipo iweka nikaikuta …