SORRY MADAM (77)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (77)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi : Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SABINI NA SABA ILIPOISHIA... Nikaitega mikono yangu usawa wa sehemu anayo ning’inia Dorecy , nikahesabu moja hadi tatu, Dorecy akajiachia na kutua kwenye mikono yangu, cha kushukuru MUNGU ametua vizuri kwenye mikono yangu, nikamsimamisha chini na kumuacha akiendelea kuhema kwa nguvu, kama bata mzinga. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikaanza kupiga hatua za kuondoka katika eneo hili pasipo kusubiria asante ya Dorecy huku moyoni mwangu nikijikuta nikianza kusamehe kuhusiana na madini yangu, kwani hakuna uwezekano wowote wa mimi kuyapata kutokana na Khalid kujizatiti vizuri katika swala la ulinzi “Edd….y” Nilisikia sauti ya Dorecy ikiniita kwa unyonge nyuma yangu, nikasimama pasipo kutazama nyuma, nikashusha pumzi nyingi na kugeuka taratibu, nikamuona Dorecy akianza kukaa chini taratibu huku akiwa amelishika tumbo lake “Eddy nakufa mimi, tumbo langu” Dorecy alilalamika huku akiwa amelishika rumbo la…