SORRY MADAM (78)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SABINI NA NANE ILIPOISHIA... Nilisikia sauti ikiniita masikioni mwangu, ambayo inaendana na sauti ya mke wangu phidaya , nikageuza shingo yangu kutazama sehemu inapo tokea sauti hiyo, nikawaona watu wawili wakiwa wamesimama huku mmoja akiwa amevalia mavazi meupe huku wapili nguo zake zikiwa na rangi mchangayiko. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “eddy mume wangu upo salama?” Sauti ya phidaya ikaendelea kupenya masikioni mwangu, nikajaribu kuzungumza ila kinywa changu nikakikuta kikiwa ni kizito sana, nikabaki nikimtazama phidaya mke wangu, aliye valia gauni lenye rangi machanganyiko, mkono wa pihidaya ukapita kwenye sura yangu, kisha mwanaume aliye valia nguo nyeupe akamshika na kumuondoa ndani ya chumba Hali yangu ya afya ikazidi kuhimarika siku hadi siku, nikiendelea kupatiwa huduma na madaktari ambao sikuwafahamu, zikapita siku kadhaa nikiwa kitandani nikiendelea kuuguza majeraha yangu ya mwili…