Notifications
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…

SORRY MADAM (78)

SEHEMU YA SABINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Nilisikia sauti ikiniita masikioni mwangu, ambayo inaendana na sauti ya mke wangu phidaya, nikageuza shingo yangu kutazama sehemu inapo tokea sauti hiyo, nikawaona watu wawili wakiwa wamesimama huku mmoja akiwa amevalia mavazi meupe huku wapili nguo zake zikiwa na rangi mchangayiko.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“eddy mume wangu upo salama?”
Sauti ya phidaya ikaendelea kupenya masikioni mwangu, nikajaribu kuzungumza ila kinywa changu nikakikuta kikiwa ni kizito sana, nikabaki nikimtazama phidaya mke wangu, aliye valia gauni lenye rangi machanganyiko, mkono wa pihidaya ukapita kwenye sura yangu, kisha mwanaume aliye valia nguo nyeupe akamshika na kumuondoa ndani ya chumba

Hali yangu ya afya ikazidi kuhimarika siku hadi siku, nikiendelea kupatiwa huduma na madaktari ambao sikuwafahamu, zikapita siku kadhaa nikiwa kitandani nikiendelea kuuguza majeraha yangu ya mwili mzima huku phidaya akija kunitembelea kila siku, ila kitu kikubwa ambacho ananificha ni jinsi ya mimi kufika katika hospitali hii
“baby ngoja mimi nirudi hotelin”
Phidaya alinyanyuka kiuvivu huku tumbo lake likiwa kubwa kiasi, kutokana na ujauzito wake alio kuwa nao

“ngoja kwanza”
Nilimuambia phidaya huku nikimshika mkono wake wa kushoto, uliokuwa karibu yangu
“kwa nini huniambii ukweli, juu ya kufika kwangu hapa”
“eddy nilisha kueleza kwamba, nitakujibu mume wangu siku ukiwa umepona vizuri, hili swala halina haja ya wewe kulijua kwa wakati huu
“hata kama, kwani kukuuliza jinsi ya mimi kufika hapa imekuwa ni shida, si ndio?”
“hapana mume wangu, ila kikubwa ni wewe afya yako kuwa katika hali ya uzima”
“powa kama hutaki kuniambia chochote ninakuomba uende zako”

Nilizungumza kwa hasir huku nikimtazama phidaya aliye simama pembeni ya kitanda changu,
“baby umekasirika?”
“hapana, wewe nenda”
Phidaya akaanza kupiga hatua za kuondoka kuelekea ulipo mlango wa kutokea katika chumba cha hospitalini, kabla hajaufikia nikamstua
“na usipo nikuta, usijilaumu”

Ikamlazimu phidaya kugeuka na kunitazama kwa macho ya mshangao mwingi, taratibu akarudi na kukaaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na huzuni kidogo
“mume wangu ni kwanini unazungumza maneno kama hayo, unajua ni jinsi gani unavyo utesa moyo wangu”
“tatizo sio kuutesa moyo wako ila tatizo ni kwanini hutaki kuniambia ukweli juu kufika kwangu hapa, kwa mtazamo wangu hapa si iraq, siwezi kuendelea kukaa sehemu ambayo siijui ni wapi nikifa j…?”
“eddy inatosha…”

Phidaya alinikatisha na kuzungumza kwa sauti kubwa ya ukali huku machozi yakimwagika usoni mwake, akanitazama na macho yake makubwa kiasi ambayo tayari yalisha anza kubadilika rangi na kuwa mekundu kiasi
“eddy unajua ni jinsi gani, tabu niliyo ipata hadi kukuleta hapa eheeeee? Ulikuwa ni mfu wewe usiye jitambua, umeyafanya maisha yangu kuwa ni yakuwindwa kama kitu cha thamani kwa ajili yako”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo jaa hasira
“utaka kujua kwamba hapa ni wapi si ndio?”

Swali la phidaya likaniacha mdomo wazi huku nikishindwa kujua ni jinsi gani nimjibu
“si unataka kujua, mbona uzungumzi?”
“ndio”
Nilijibu kwa unyonge baada ya kumuona phidaya akinijia juu
“hapa manila, philipines”
“ndio wapi?”
“ndio hapa”

Phidaya alinijibu kwa ufupi huku akinitazama machoni, akanyanyuka na kupiga hatua za haraka hadi shemeu ulipo mlango akafungua na kutoka, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, huku nikuutazama mlango aliotoka phidaya.Kitu kikubwa ambacho kunaniumiza kichwa ni juu ya kwanini phidaya hataki kunieleza ukweli jinsi ya yeye alivyo fika hapa
Siku mbili zikapita pasipo kumuona phidaya, jambo lililoanza kuzua wingi wa maswali kichwani mwangu, huku nikijiuliza ni nikwanini sijkumbili hizi hajatokea.
“au hao watu wanao muwinda ndio wamemteka?”

Niswali jingine lililotokea kuniumiza kichwa change, kutokana nimeshaanza kuruhusiwa kutoka nje ya maeneo ya hii hospitali iliyojaa watu wenye asili ya bara la ulaya na asia.Sikuwa na rafiki zaidi ya kuzunguka kila eneo la hospitali huku nikiwa nimevalia nguo nyeupe zinazo fanana na wangonjwa wengine wanao zunguka zunguka katika eneo hili la hospitlini

Baada ya kuhisi kuchoka nikaamua kurudi kwenye chumba change, kabla sijakifikia nikawaona jamaa wawili walio walia nguo nyeusi pamoja na miwani wakiingia ndani ya chumba change, ikanilazimu kujibanza kwenye moja ya kona ya ukuta kutazama kujua ni kitu gani amacho kitaendelea, baada ya dakika kama tatu hivi jamaa wakatoka na kuondoka, jambo lililo anza kunipa mashaka mengi
“niende au nisiende?”

Nilijiuliza huku mwili mzima ukinitetemeka, nikatazama mlango wa chumba changu kisha nikajipa matumaini mimi mwenye kwamba hakuna kitu kibaya kitakacho tokea juu yangu, nikaanza kupiga hatau za kwenda kilipo chumba change, nikafika kwenye mlango na kukishika kitasa, nikashusha pumzi na kufungua mlango taratibu.Nikamkuta phidaya akiwa amekaa kwenye kiti pamoja na mwanamke aliye valia baibui jeusi, huku usoni mwake akiwa amejiziba na kubakisha macho yake, nikawatazama kwa muda huku nao wakinitazama, msichana aliye vaa baibui akajifungua uso wake na kujua kwamba ni dorecy
“mbona unashangaa?”

Dorecy aliniuliza huku akinyanyuka kwenye kiti nilicho kikalia
“hapana”
“karibu ndani ukae”
Nikapitiliza moja kwa moja na kukaa kitandani mwangu, na kuwatazama phidaya, aliye nunu na dorecy ambaye sura yake ipo kawaida tu
“ninafuraha kukuona tena ukiwa hai eddy”
“asante”
“niliwaagiza watu wangu wakakutafute huko nje, kutoka tulilkuja muda mrefu hatukuona, ila tulivyo wauliza manesi wakadai kwamba upo kwenye maeneo ya viwanja vya michezo”

Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa amesimama akinitazama kitandani sehemu nilipo kaa
“ila vipi bado unamaumivu ya vidonda vya risasi?”
“hapana vimesha kauka”
Ukimya ukatawala ndani ya chumba huku kila mmoja akiwa yupo kimya akimtazama mwenzake aanze kuzngumza.Phidaya akasimama na kutaka kutoka ndani ya chumba ila dorecy akamkamata mkono
“shoga yangu ninakuomba utulize hsira usiondoke”
“sioni sababu ya mimi kuendelea kukaa hapa”
“ndio ninatambua ya kwamba unahasira sana, ila ninakuomba utulie kwani kuendelea kuwa na hasira haitasaidia kupatana kwenu”

Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa ameushika mkono wa phidaya aliye vimba kwa hasira, sikujua ni kitu gani ambacho kimemkasirisha phidaya hadi ikafikia hatua ya yeye kunichukia kupita maelezo.Phidaya akarudi na kukaa kwenye kiti chake alichokuwa ameka
“eddy natambua ya kwamba hujui ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa wakati huu, ila utaelewa tuu”
“kwani mke wangu unatatizo gani?”
“nani mke wako?”
“haaaa”

Ilinibidi kushangaa tu kwani sikulitarajia jibu kama hili la phidaya kunijibu mimi, kwaishara dorecy akaniomba ninyamaze kimya kwamaana ananijua mimi vizuri sana pale ninapokuwa nimekasirika
“eddy ile siku ambayo ulipigwa risasi kule porini, mume wangu alinichukua mimi pamoja na mtoto, akiamini kwamba wewe umeshafariki.Walinipeleka hadi nyumbani, ila kwa siri sana nilizungumza na hawa walinzi wangu wawili nilio kuja nao huku”

“walienda kukuchukua kule porini nakunipele kwenye moja ya hospitali pasipo khalid kugundua kitu cha aina yoyote.Kwa kipindi chote ulipokuwa kwenye hospitali ya siri, ukifanyiwa matibabu ya kuyaokoa maisha yako, niliendelea kulifanyia kazi ombi lako la wewe kumtafuta mke wako, hadi nikafanikiwa kimpata”
Tulinyamaza kimya mimi na phidaya tukimuacha dorecy akizungumza,

“baada ya kukutana na bibie hapa, nilimueleza kila kitu juu yako, na maisha yetu ya nyuma, kitu ambacho sikukijua ni kwamba kunabadhi ya mambo ambayo wewe hukumuadisia mkeo na mimi nikajikuta nikumuadisi”
“phidaya alikasirika sana, na kukiri kwamba hakufahamu wewe, ila nileiendele kumbembeleza ili asifikie hatua ya kukutenga wewe, nashukuru mungu kwamba alinielewa, kumbe kunakipindi kunatukio ambalo mulilifana wewe na yeye, ambalo kule iraq hadi leo munatafutwa na serikali ya kule”
“ngoja kwanza, tukio la mimi kutoroshwa hospitali ndilo lilolofanya sisi kutafutwa?”
Nilimuuliza dorecy na kumfanya phidaya kunitazama kwa jicho kali lililo jaa hasira
“ndio, ila kuna ishu khalid alitaka kukufanyia wewe na phidaya akaiingilia kati na kuwa adui namba mwengine wa khalid”
“jambo gani hilo?”

Hata kabla dorecy hajanijibu tukasikia milio mingi ya risasi kwenye kordo yetu huku kelele za watu wagonjwa na manesi wakike zikisikia jambo lililo tustua sote ndani ya chumba

Milio ya risasi ikaendelea kurindima nje ya chumba tulichopo na kuzidi kutupagawisha sote tuliopo ndani ya chumb hichi, wasiwasi mwingi ukawa kwa dorecy ambaye fika anaoenekana kuchanganyikiwa
“eddy hao ni watu wa mume wangu”
Dorecy alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, nikapiga hatua za haraka hadi dirishani na kuchungulia chini ambapo kuna umbali wa ghorofa mbili kwenda chini.
“hatuwezi kutoka humu ndani”
Nilizungumza huku nikiwatazama dorery na phidaya
“itakuwaje sasa?”

Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika kwa wingi.Nikapiga hatua hadi mlangoni, nikachungulia kwenye sehemu ya kuingizia funguo, nikamshuhudia jamaa mmoja akitandika risasi ya kichwa mzee mmoja aliye ambiwa alale chini ila akaleta kiherehe cha kujinyanyua, ndipo akakutana na maafa hayo ambayo ni yakinyama sana.

Gafla simu ya phidaya ikaita na kutufanya sote kumgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao, kwa kiwewe alicho nacho akashindwa hata kuikata na kujikuta akiiachia na kuanguka chini, nikachungulia tena kwenye tobo la kuingizia funguo na kumuona jamaa aliye muua mzee, akiutazama mlango wetu kwa umakini.
“ingieni bafuni”

Nilizungumza kwa sauti ya chinichini, dorecy akamshika mkono phidaya na kukimbilia kwenye bafu liilopo humu ndani ya chumba changu.Jamaa akapiga hatua hadi ulipo mlango uku bunduki yake aina ya ‘short gun’ ikiwa mkononi mwake.
Nikajibanza nyuma ya mlango, huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwani bado sijaiamini afya yangu kwa kiasi kikubwa kutokana na majeraha ya risasi yaliyopo mwilini mwangu.

Mlango taratibu ukafunguliwa, nikaanza kuona kiatu cheusi kikitangulia mbele, jamaa akasimama kwa muda, gafla simu ya phidaya iliyo anguka chini ikaanza kuita tena na kumfanya jamaa kupiga hatua za taratibu hadi sehemu ilipo anguka simu na kuiokota.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, kwani endapo jamaa atageuka nyuma nilazima ataniona.Akaitazama simu ya phidaya kwa muda na kuitupa chini na kuchanguka, akatazama mlango wa kuingilia bafuni ambapo ndani yake yupo phidaya na dorecy

Simu ya jamaa ikaita, akaitoa kwenye koti lake, akaipokea nakuiweka sikioni mwake, akazungumza kwa lugha ya kiarabu, nikastukia kumuona jamaa akichomoka kwa kasi, ndani ya chumba pasipo kuniona nyuma ya mlango, ving’ora vya gari za polisi, nikaanza kuvisikia na kunifanya nishushe pumzi nyingi, na kujikalia chini, huku jasho jingi likimwagika.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
37 Simulizi Sorry Madam
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni