SORRY MADAM (81)

0
SEHEMU YA THEMANINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Jasho halikuacha kunitiririka japo kuwa ndani ya chumba hichi kuna baridi nzuri yajutosha, jamaa akamuomba mtu wake azitume picha za gari na mwanamke hukyo makao makuu ya polisi kupitia mtandao(internet), ili kuzidi kuwarahisishia kazi askari polisi

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“eddy usiwe na wasiwasi, kama tukio limefanyika kwenye hoteli hii basi, muhalifu aliye mteka mke wako atapatika tu”
“ila mke wangu atakuwa amesha fariki”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, twasira za sura ya mke wangu masaa machache ya nyuma yaliyo pita zikaanza kunisumbua kichwani mwangu, nikajikuta nikianza kujilaamu nikwanini nilitoka chumbani kwangu na kumuacha phidaya wangu akiwa amelala peke yake, jamaa akasogea pembeni na kuzungumza na simu, sikujua anazungumza na nani, baada ya muda akarudi tulipo

“eddy nilikuwa nikizungumza na baba yako, na yupo njiani anakuja”
“baba yake!?”
John aliuliza huku akiwa ameshangaa, sikutaka kumjibu kitu chochote zaidi ya kujikalia zangu kwenye kiti huku mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio, ndani ya dakika ishirini, mlango ukafunguliwa na akaingia baba akiwa na walinzi wake wanne walio valia suti nyeusi pamoja na miwani, nikanyanyuka kwenye kiti na kukumbatiana na baba huku akionekana kuwa nafuraha usoni mwake, kwani hakuamini uwepo wangu, jamaa akaanza kumuelezea baba kila kitu kilicho tokea na kumuonyesha baadhi ya video hizo za mwanamke aliye mteka mke wangu

“pole sana eddy”
Baba alinipa pole na mimi nikaiitikia kwa sauti ya chini, tukatoka ndani ya chumba nikiwa nimeongozana na baba pamoja na walinzi wake, huku jamaa na john wakifwata kwa nyuma, tukakuta polisi wakiwa wanafanya vipimo kwenye chumba change

“mumefikia wapi?”
Baba alimuuliza mmoja wa polisi
“hii damu, inaonekana si damu ya mauaji”
“kivipi?” baba aliuliza tena
“inaonekana mtekaji alimwaga damu kwenye shuka kutoka kwenye pakti za kuhifadhia damu”
Askari alituambia huku akituonyesha pakti mbili za kuhifadhia damu, walizo zitoa ndani ya chumba changu baada ya kukifanyia uchunguzi sana

“ila mtekaji atapatikana kwa maana inaonekana hajatoka mbali sana na hapa”
Polisi alizungumza, ila moyo wangu haukuwa na furaha hata kidogo japo wanadai kwamba ni damu ndizo zilizo mwagwa kwenye shuka la chumbani kwetu, tukatoka na baba hadi sehemu ya kupumzikia, ukimya ukatawala kati yetu, hapakuwa na aliye zungumza kitu chochote zaidi ya mimi kutazama tazama mandhari yaliyomo humu ndani

“eddy, ulikuwa wapi mwanangu?”
“baba, ngoja hayo mazungumzo tutayazungumza baada ya kufikia muafaka kutambua ni wapi alipo mke wangu”
Nilizungumza kwasauti nzito iliyo jaa hasira ndani yake, baba alinielewa na kukaa kimya hakutaka aendelea kunigusia kuhusiana na kitu cha aina yoyote.Simu ya baba ikaita na akaanza kuzungumza na mtu aliye mpigia

“eddy twende sehemu, lile gari lawagonjwa limepatikana”
Baba aliniambia mara baada ya simu kukata, nikawa wakwanza kunyanyuka kwenye kiti na kuanza kuongozana, tukaingia kwenye gari huku john akiingia kwenye gari ya jamaa ambaye ni meneja wa hoteli.Tukatembea umbali wa kilomita kumi, tukafika pembezoni mwa mlima na kuwakuta polisi wengi wakiwa wamelizingira gari lawagonjwa, kwa umbali kidogo ambalo pembeni limezungushiwa mabomo yakutega yapatayo sita, bomo moja nikaliona likiwa limebakisha sekunde hamsini huku zikiendelea kurudi nyuma taratibu

“phidaya”
Nilianza kukimbia kuelekea lilipo gari lawagonjwa polisi wakanidaka, na kunizuia nisiendelee kwenda mbele, gafla mlipuko mkubwa ukalipuka kwenye gari na kusababisha polisi walio nikamata kuniangusha chini na kunifunika na miili yao waliyo valia nguo maalumu zinazo zuia kuadhirika na vipande pande vya vyuma vitokanavyo na mabomu endapo vitawaangukia
“phidayaaaaaaaaaaaaaaaaaa”
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku machozi ya uchungu yakinimwagika usoni mwangu, huku nikilishuhudia gari alilopo mke wangu likiteketea kwa moto mkali
 
Askari wa kikosi cha zima moto wakaanza kulishambulia gari la wagonjwa kwa kutumia mipira mirefu inayotoa maji kwa kasi kiasi kwamba, moto ukaanza kupunguza makali yake ya kuteketea, amchozi yalizidi kunitoka huku askari wakiendelea kunizuia nisikaribie eneo ambalo lipo gari, wakanikabidhi kwa walinzi wa baba, ambao waliendelea kunishika.Si mimi tu ambaye nipo kwenye huzuni, ila hata rafiki yangu john, machozi yalianza kumtoka, na kuzidi kunizidishia hisia ya kumwagikwa na machozi mengi

“eddy, jikaze mwanangu”
Baba alizungumza huku akinikumbatia, akiendelea kunipigapiga mgongoni ikiwa ni ishara ya kunituliza hasira na uchungu ambao nimeupata, askari wengine wakaanza kazi ya kuchambua kama kuna kitu kilicho salia kwenye gari, ikiwemo kupata udhibitisho wa kama kuna mwili wa mtu ambaye alikuwepo ndani ya gari, mwili mzima ukazidi kunitetemeka kwa woga, kila ninapojaribu kutazama gari lililo teketea kwa moto, dua yangu kubwa ni kumuomba mungu aweze kutenda miujiza phidaya asiwepo ndani ya gari hilo.

Askari mmoja akatufwata sehemu nilipo simama mimi pamoja na askari wa baba, huku mkononi mwake akiwa ameshika kibegi kidogo, na viganjani mwake akiwa amevaa gloves nyeusi.Akamsalimia baba, kasha akatusalimia na sisi, akamuomba baba wazungumze pembeni, baba akatii ombi la askari huyo, sikusikia kitu ambacho wanakizungumza
Mlio wa simu ya john, ukanistua kutoka katika dimbwi kubwa la mawazo na kujikuta nikimgeumkia na kumtazama kwa macho yaliyo jaa huzuni nyingi, john akaitazama simu yake kwa muda huku akiwa amekunja ndita, akaipokea na kukaa kimya

“nani mwenzangu?”
John alizungumza baada ya sekunde kadhaa ya simu yake kuwa sikioni
“hapana, mimi ninawapa watu wengi namba yangu, kwahiyo usipo taja jina lako mimi siwezi kutambua kwamba wewe ni nani?
John alizungumza kwa sauti  ya ukali huku macho yake akiya pepesa pepesa

“wee mwendawazimu nini, usinichangenye”
John alizungumza huku akiachia msunyo mkali na kukata simu yake, nikaanza kupiga hatua kulifwata gari lililo teketea ambapo kuna askari, pamoja na madaktari wakiendelea kufanya uchunguzi na vifaa vyao maalumu.Nikafanikiwa kufika pasipo mtu yoyote kunishika mkono, nikakuta wakiyapiga picha, mafuvu mawili ya watu, yaliyo tekete kwa moto, ikiashiria kwamba miili yao, imesha teketea, nikajikuta nikianguka chini kama mzigo, kutokana na kuishiwa na guvu za mwili wangu.

Madaktari wakaniwahi kunipa huduma ya kwanza, ikiwemo kuniwekea mashine ya kunisaidia kuhema, japo fahamu hazijanipotea, ila sikuwa na uwezo wakuuamuru mwili wangu kufanya kitu, ambacho ninakihitaji, machozi yakaanza kunichuruzika, kumbukumbu za gari kulipuka dakika chache zilizo pita zikaanza kunijia kichwani mwangu, nikaanza kuisikia sauti ya phidaya kwa mbali ikiniita masikioni mwangu, nikataka kunyanyuka, ila madaktari wakanizuia nisinyanyuke

“mwanangu atapona?”
“ndio mzee atapona, ni mstuko tu, ndio umempata ulio pelekea yeye kuishiwa na nguvu, kidogo na uwezo wa moyo wake ulishindwa kudunda kama inavyo paswa ufanye”
Daktari mmoja nilimsikia akimjibu baba, huku wezake wakiniinyanyua kwenye machela, waliyo kuwa wameniweka wakinipatia huduma ya kwanza na kuniiingiza ndani ya gari.John akawahi kuingia ndani ya gari la wagonjwa, lililokuja muda mchache baada ya mimi kuanguka chini.

“eddy”
John aliniita, na kumtazama taratibu, pasipo kumjibu kitu chochote, kwani hata kuzungumza kumenishinda kabisa
“mungu, atasaidia kila kitu kitakuwa sawa”
John alizungumza kwa kunifariji tu, kwani ukweli halisi nimeshaujua, kwamba phidaya sipo naye tena duniani, kwani mafuvu mawili ni yawatu ambao nimeyakuta kwenye gari, yanaashiria kwamba ni mke wangu ni marehemu.

Wakanishusha kwenye gari, wakaniweka kwenye kitanda cha kusukuma, manesi wawili wakaanza kukisukuma kitanda nilicho lalia hadi kwenye moja ya chumba na kuniingiza humu, nikakuta madaktari wawili wakiwa ndani ya chumba wakiwa tayari kwa kunihudumia.Wakanichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto sehemu ya mshipa wa damu, kasha waniwekea baadhi ya vifaa kifuani kwangu, ambavyo sikuelewa kazi yake ni nini.Wakamaliza kufanya kazi yao, ya kunihudumia na kutoka ndani ya chumba, msongamano wa mawazo ukazidi kunipelekesh, huku sura ya mke wangu phidaya ikiwa haichezi mbali na fikra zangu

“eddy I love you”(eddy ninakupenda)
Sauti ya phidaya ikaendelea, kusikika kwenye masikio yangu, nikajitahidi kuyazungusha macho yangu kila pande ya chumba kutazama kama nitaweza kumuona mke wangu ila sikufanikiwa, kuiona sura yake.Baada ya masaa manne mlango ukafunguliwa na akaingia baba pamoja na john, kila mmoja anaonekaa kuwa na huzuni, baba akasimama pembeni ya kitanda change, huku john akikaa sehemu ndogo ya kitanda nilicho lalia

“unajisikiaje mwangu”
“safi”
Nilimjibu baba kwa sauti ya chini, iliyo jaa mkwaruzo
“baba, yale mafuvu yapo wapi?”
 Baba hakunijibu zaidi ya kumtazama john, kisha wakanitazama hakuna aliye jibu swali langu, ila macho yao nikatambua kwamba yanakitu wanacho kijua ila wananificha

“ahaa…., inabidi kwamba…… ahaaa kesho urudi nyumbani, ukapumzike kwa muda kidogo ili uwe sawa”
Baba alizungumza kwa kubabaika, nikamtazama john, akatizama chini baada ya macho yangu kukumbana na macho yangu. Simu ya baba ikaita ikambidi atoke nje kwenda kuipokea

“john niambie ukweli mke wangu amekufa?”
“eddy………………”
John aliniita, nikabaki nikimtazama pasipo kumuitikia.Ukimya ukatawala, kama dakika mbili john hakunijibu swali langu nililo muuliza.Kijimlio kifupi kikasikika kwenye simu ya john iliyopo mfukoni, ikamlazimu kuitoa simu yake, mfukoni.Akasoma meseji aliyo ingia, akanitazama kwa jicho la kuiba na kuitazama tena meseji anayo isoma

“kaka hembu soma hicho kilicho indikwa”
John akanipa simu, kabla sijaisoma meseji iliyopo kwenye simu, baba akaingia ndani akiwa ameongozana na madaktari walio, nitibu muda mchache ulio pita, wakafika kwenye kitandani nilicho lala.Daktari mmoja akanitoa vifaa walivyo niwekea kifuani,

“how do you feel?”(unajisikiaje?)
Daktari mmoja aliniuliza
“najisikia powa”
Daktari wa pili akaniwekea kifaa kigo cha kusikilizia mapigo ya moyo, akamtazama baba

“kwa sasa yupo salama, tunaweza kumruhusu kurudi nyumbani”
“shukrani daktari”
Baba alizungumza, huku akimpa mkono dokta, wakanipa vidonge vya kuupa mwili wangu nguvu, nikaruhusiwa kutoka hospitalini, tayari giza lilisha anza kutawala anga, kwa mbali, ikiwa ni majira ya jioni, tukaingia kwenye gari moja mimi pamoja na john, huku baba akiwa katika gari lake jengine

“uliisoma ile meseji?”
“ngoja noisome”
Nikaitoa simu mfukoni na kumpa john anitolee namba za siri alizo ziweka kwenye simu yake upende wa meseji kisha akanirudishia
{kaa mbali na hii vita kati yangu mimi na eddy, utaumia}

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)