SORRY MADAM (84)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA THEMANINI NA NNE ILIPOISHIA... Jamaa mmoja alimshauri mwenzake na kuinyanyua tena simu yake na kuiweka sikioni, nikajikuta nikiitumbulia mimacho simu ya victoria nikisikilizia kuingia kwa simu hiyo. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Ila haikuingia nikamsikia akizungumza “bosi tumemkosa eddy” “tumefwatilia, tumefanya shambulio la gafla ila hatujamuona” “sawa, bosi” Jamaa akakata simu na kuwatazama wezake “oya jumbe , bosi anasemaje?” “anasema tuhakikishe tunarudi na kichwa cha eddy, la sivyo atavikata vichwa vyetu” “mmmm” Jamaa mmoja akaguna, huku akishusha pumzi nyingi, mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, hapa ndipo nikapata uhakika wa victoria ndio adui yangu namba moja na ndio yupo nyuma ya mpango mzima wa kumuua mke wangu akishirikiana na john , rafiki yangu wa karibu “kama atakuwepo atakuwepo eneo, haya tumt……..” Kabla ya mkuu wao, anaye itwa jumbe hajamalizia sentesi yake, sote tukastushwa na sauti…