SORRY MADAM (84)

0
SEHEMU YA THEMANINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Jamaa mmoja alimshauri mwenzake na kuinyanyua tena simu yake na kuiweka sikioni, nikajikuta nikiitumbulia mimacho simu ya victoria nikisikilizia kuingia kwa simu hiyo.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Ila haikuingia nikamsikia akizungumza

“bosi tumemkosa eddy”
“tumefwatilia, tumefanya shambulio la gafla ila hatujamuona”
“sawa, bosi”
Jamaa akakata simu na kuwatazama wezake
“oya jumbe, bosi anasemaje?”
“anasema tuhakikishe tunarudi na kichwa cha eddy, la sivyo atavikata vichwa vyetu”
“mmmm”

Jamaa mmoja akaguna, huku akishusha pumzi nyingi, mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, hapa ndipo nikapata uhakika wa victoria ndio adui yangu namba moja na ndio yupo nyuma ya mpango mzima wa kumuua mke wangu akishirikiana na john, rafiki yangu wa karibu

“kama atakuwepo atakuwepo eneo, haya tumt……..”

Kabla ya mkuu wao, anaye itwa jumbe hajamalizia sentesi yake, sote tukastushwa na sauti ya simu ya john, iliyopo mfukoni mwangu.Nikasimama kwa haraka huku nikiwatazama jamaa, ambao nao wakanitazama huku akionekana kutokuamini macho yao, nisawasawa na mtu aliye okota embe dodo chini ya mti wa mpapai

“kamaataaaaaaa mshenzi yule”

Jumbe alizungumza huku akininyoosheaa kidole, kwa haraka nikaanza kukimbia nikieleka kwenye msitu huu, ambao ulikuwa na barabara tuliyo kuwa tunapita.Taa za pikipiki wanazo ziendesha jamaa, zikazidi kunifwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi, nikazidi kukimbia kuelekea nisipo pajua huku nikikatisha katisha kwenye miti, nikikwepa risasi nyingi zinazo kuja nyuma yangu

“eheee mungu wangu, nisadie mie”

Nilizungumza huku nikiendelea kukimbia, nikafanikiwa kupandisha kwenye kilima chenye mawe mengi makubwa ambayo si rahisi kwa pikipiki kupita, nikazidi kuongeza mwendo wa kukimbia, huku nikihema sana, nikazidi kupandisha mlima huku nikijitahidi kwa kadri yangu, kutafuta sehemu ambayo ninaweza kujibanza na kuwakwepa jamaa wana nitafuta

Nikafanikiwa kuingia kwenye moja ya mwamba wenye tobo kubwa, sikujali kama kunaweza kuwa na kutu cha hatari ndani ya mwamba huu, zaidi nilicho kijua mimi ni kujibanza huku, jasho jingi likinimwagika, kutokana na mwanga mzuri wa mbalamwezi nikawaona watu hao wakiendelea kutazama huku na huku na kuzidi kwenda mbele wakiamini kwamba nimekimbilia juu kabisa kwenye milima.Walipo potea kwenye macho yangu, nikaanza kurudi nyuma tulipo toka, safari hii nikijitahidi kufunga breki za miguu yangu, kuhakikisha sianguki kwani kasi niliyo nayo ya kushuka mlimani si ndogo, ikitokea bahati mbaya nikakosea kushuka nilazima kichwa kipige chini, hapo kuna mawili, kuvunjika vunjika mifupa au kufa kabisa

Simu ya john ikaanza kuita mfukoni mwangu, nikaitoa na kukuta jina la ‘my victoria’ huku pembeni kukiandikwa namba 2.Ikimaanisha ni namba ya pili kuwekwa kwenye simu hii, nikajibanza sehemu, yenye jiwe kubwa na kuitazama kwa muda, huku nikijaribu kuyalazimisha mate kupita kwenye koo langu lililo kauka kwa kiasi kikubwa, na taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni

“hahahaaaa, eddy, rafiki yangu, si kila unaye muona kwako ni mwemaaaaa, wengine ni maadui.Kumbuka tanzania wewe ulijifanya ni mjanja kunionea na kunidhalilisha kwa kunipiga, sasa ni muda wako wakudhalilikaaa, ahahaaaaaaha”

Sauti ya john ilisikika huku, akizungumza kwa dharau na kucheka sana.Asira ikazidi kunipanda huku mwili mzima ukinitetemeka kwa hasira iliyo kali

“ohhhh kaka eddy, kumbuka mimi sio ndugu yako.Baba yako kwa nyege zake alimchukua mama yangu kutoka mikononi mwa baba yangu, kwa kutumia pesa zake, kisha wewe ukamtesa mama yangu na kumfanya afe, you’re a loser…………”(….., wewe ni mpotezaji)

Sauti ya victoria ilisikika huku wote wawili wakionekana kufurahia ushindi walio upata dhidi yangu

“wait bro eddy, ukirudi nyumbani utamkuta baba yako ni maiti, love you baby boy eddy, mwaaaaaaa”(subiri kaka eddy……., nakupenda eddy mtoto wa kiume,……)

Nikajihisi, mwili ukipasuka kwa hasira nikataka kupiga hatua moja mbele, ila kuna kitu kigumu kikanigusa kwenye kichwa changu upande wa kulia

“ohhhh lete simu yako”

Ni sauti nzito ya mmoja wa majambazi walio tumwa na victoria, kuja kuniangamiza.Taratibu akapita mbele yangu, huku bunduki yake akiwa ameielekeza kichwani kwangu

“utanaka simu eheeee”

Nilizungumza kwa kujiamini, huku nikimtazma kwa macho yaliyo anza kudondosha machozi ya asira pamoja na uchungu mwingi.Kwa haraka nikairusha simu juu, na kumfanya jambazi kuiangalia jinsi inavyo kwenda juu kwa kasi, nikaushika mkono wake wenye bastola, na kuvivunja vidole vyake vya mkono ulio shika bastola, akainama huku akitoa maumivu makali ya kuumia huku akilalamika.Nikampiga kigoti cha mso na kumfanya asimame, huku akiyumba yumba.Ngumi niliyo ikunja vizuri, ikatua kwenye shingo yake, ikampeleka chini, simu yake ya upepo aliyo kuwa ameishika na mkono mwengine ikaanguka chini huku sauti ya mkuu wake ikisisika

“g umepatwa na nini, eheeee”

Akanyanyuka na kutema mate pembeni yaliyo changanyikana na damu, ikiashiria kuna sehemu kwenye kinywa chake imepata itilafu.Akarusha teke, nikainama chini, na kujizungusha kwa haraka, nikaichota miguu yake na kumbwaga chini kama mzigo wa kuni.

Macho yangu yakatua kwenye bastola iliyo anguka karibu yangu, nikaiokota kwa haraka, jamaa akanishika mguu wa kulia na kuuvuta, ikapelekea mimi kuangukia mgongo na kuichia bastola ikasogea pembeni kidogo.Jamaa akaniwahi kunikalia tumboni, akaanza kunikaba koo kwanguvu nyingi kwa kutumia mkono wake ambao sijauvunja vidole, nikajitahidi kuminyana naye, huku mkono wangu mmoja nikiupeleka ilipo bastola, jamaa akazidi kuniminya koo langu, hadi nikajihisi kuanza kufanya mawasiliano na malaika mtoa roho
‘ukiwa mwanaume hutakiwi kukata tamaa kirahisi, pambana hadi dakika ya mwisho, hata kuua ikibidi fanya hivyo, ili tu uwe mshindi’

Nimaneno ya baba yangu mkubwa mzee godwin, kipindi alipokuwa akinifundisha mazoezi ya kupigana, nilipokuwa kijana wa umri mdogo sana, na maneno yake haya alikuwa akiniambia pale anaponizidi ikiwemo kunipoga kabala.Nikazidi kuupelekea mkono wangu sehemu yanye bastola, kidole change kimoja cha katikati, mkono wa kulia, kikaanza kuivuta taratibu bastola, hadi ikafika kwenye vidole vyangu vyote vitano vya mkono wa kulia. Sikuuliza zaidi ya kuvuta traiga, ya bastola mara sita na kuziruhusu risasi sita kutoka kwenye bastola, na kupenya kwenye mbavu za jambazi huyu, akaanguka pembeni yangu huku akivuta pumzi yake ya mwisho

Nikasimama na kumtizama jambazi huyu jinsi anavyo hangaika hangaika, nikafyatua risasi mbili, zikaingia kichwani mwake, akatulia tuli, nikaiokota simu ya john pamoja na simu ya upepo ya jambazi iliyo anguka

“upo wapi g wewe, tukufwate?”

Suti ya mkuu wao ambaye anaitwa jumbe, ilisikika vizuri kwenye spika za simu hii

“zamu yenu inafwata”

Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo mingi, nikaipiga simu ya upepo kwenye jiwe kubwa, ikapelekea kuchanguka changuka vipande vingi.Nikakaanza kushuak kwenda chini, kwa bahati nzuri nikakuta sehemu walipo zisimamisha pikipiki zao, nikapanda kwenye moja ya pikipiki, nikaiendesha kwa kasi hadi umbali kidogo na zilipo nyingine, nikashuka na kurudi zilipo nyingine, nikaziangusha chini zote, nikazifungua mifuniko ya matanki ya mafuta, kisha nikarudi nilipo iacha pikipiki niliyo ichukua.Nikafyatua risasi mbili, zilipo pikipiki na kusabisha zilipuke zote

Nikaondoka kwa kasi, huku nikiotea otea njia ya kurudi barabarani, nikafanikiwa kutokeza kwenye barabara niliyo ifahamu, kwani ndio barabara kuu ya kurudi nyumbani kwa baba.Nikazidi konyeza mwendo kasi wa pikipiki, kimoyo moyo nikiapa kuwaua john na victoria kwa mkono wangu mimi mwenye.Hadi ninafika nyumbani kwa baba imesha timu saa kumi na mbili asubuhi

“nifungulieni geti nyinyi”

Niliwafokea walinzi wa getini, waliokuwa wakinihoji maswali, ikanilazimu kulivua kufia la pikipiki, ndipo wakanitambua ni mimi, wakafungau geti na kuingia ndani kwa kasi, walimzi wakabaki wakinishangaa, nikafika mlangoni na kuisimamisha pikipiki, kwa haraka nikashuka huku bastola yangu ikiwa mkononi, nikapandisha  ngazi kwa haraka nikielekea kwenye chumba change, nikaupiga teke mlango, ukafunguka, chumbani sikukuta mtu zaidi ya kitanda kilicho changuliwa mashuka.Nikaelekea chumba cha victoria, ila sikuwakuta.Nikaelekea chumba cha baba yangu, nikawakuta walinzi wake wawili wakiwa wamesimama mlangoni, ila mmoja akanizuia nisiingie

“mzee amepumzika, hadi muda wake wa kuamka ukifika ndio, unaruhusiwa kuingia”

“nini wewe”
“hiyo ni sheria na si ombi”
“unajua mimi ni nani?”
“hata kama, ila muda wa mzee kuamka ni sambili kamili kwa sasa jaturuhusu mtu kuingia ndani ya chumba hichi”

Nikamshika tai mlinzi anaye nisemesha upuuzi wake, nikamvuta na kumuangusha chini, mwenzake akataka kunishika ila kwa haraka nikaielekeza bastola yangu, kwenye pua yake, akabaki kimya akinitumbulia mimacho yake.Nikausukuma mlango wa chumba cha baba, nikamkuta akiwa anazunguka zunguka kwenye feni lililo juu, huku akiwa amefungwa kwa kamba ngumu, mdomoni mwake akiwa amefungwa kwa plasta kubwa, huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba.

Nikabaki nikiwa nimeduwa, nikastukia walinzi nilio gombana nao mlangoni wakinipita kwa kasi na kukimbilia anapo ning’inia baba na kuanza kumshusha huku wakiwasiliana na wezao kuomba msaada.Machozi ya uchungu yakaanza kunimwagika, walinzi wakazidi kujazana chumbani kwa baba yangu, huku daktari wake akijitahidi kumpatia baba huduma ya kwanza

Nikamuona daktari akitingisha kichwa baada ya kuweka sikio lake kwenye, kifua cha baba, na kukuta mapigo yake ya moyo yakiwa yamesimama, ikiashiria kwamba ni marehemu tayari.Sikutaka hata kukisogelea kitanda cha baba, nikatoka ndani ya chumba, huku nikiwa nimefura kwa hasira kali.Sikujua hata walipo john na victori, na wao ndio wamesababisha mauji ya baba yangu.Simu ya john ikaita, na kukuta ni namba ngeni ndio inayo ita, nikaipokea haraka

“edddyyyyyyyyyy upo wapi kaka”

Sauti ya john ilisikika kwenye simu

“mshenzi, mpumbavu, nikikukamata nitakunyonga kama mulivyo fanya kwa baba yangu”

“hhaahahaaaaa kumbe umefika nyumbani….Ohhhhh boy, huwezi fanya chochote kwani hujui nilipo”

“kaka eddy, mwaya samahani kwa kumuua baba yako”

Sauti ya victoria ilisikika, alizungumza kwa dhara kubwa sana.Sikutaka kumjibu chochote, nikaikata simu, na kuingia kwenye mtandano wa goole, nika ‘download’, apps inayoitwa google map pamoja na ‘mobile location tracker’, inayo saidia kujua ni wapi namba ya simu iliyo pigwa inapatikana.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)