SEHEMU YA TISINI
ILIPOISHIA...
Nikasimama, katikati ya barabara. Sikuona aibu kwa jinsi nilivyo vaa nusu uchi, huku sehemu zangu za siri, zikiwa nimezifunika na ngozi ya chui. Mlio wa gari sikuusikia tena, kwani ninahisi lilisha pita, kabla ya mimi kuifikia barabara. Nikaendemea kuzunguka zunguka maeneo ya barabara, nikijaribu kusubiria kama ninaweza kupata usafiri.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Gafla gari moja ndogo, likapita kwa kasi pasipo kufanikiwa kulipungia mkono, ila halikufika mbali sana, likasimama. Dereva wa gari hilo akaanza kulirudisha nyuma kwa kasi, hadi sehemu nilipo simama. Kioo cha upande wa dereva kikashuka, nikamuona mvulana mmija wa kizungu, Ã kiwa na mchumba wake, wakabaki wakinishangaa kwa jinsi nilivyo vaa.
Binti wa kizungu akatoa kamera yake, aina ya digital, na kuanza kunipiga picha, huku akiwa amesimama upande wa lili wa gari, nikaanza kuwafwata taratibu
“Casey get in the car”(Casey ingia ndani ya gari)
Mvulana huyu, alizungumza kwa haraka baada ya mimi kilikaribia gari lao, kabla hajafanya chochote, nikawahi kuingiza mkono kupitia upenyo wa kioo alicho kifungua. Nikachomoa funguo ya gari lao, nakulifanya lizime. Jamaa akashuka, huku akiwa amekasirika, akajaribu kunirukia, ila nikamuwahi kumtuliza kwa ngumi ya shingo iliyo muangusha chini na kuzimia hapo hapo.
Msichana akajaribu, kukimbia ila nikamuwahi na kumdaka, nikambeba begani na kumrudisha ndani ya gari. Nikachomoa kisu changu na kumuwekea kooni mwake huku kidole changu kimoja kikimpa ishara ya kukaa kimya la sivyo nitamkata kichwa. Nikaufunga mlango wake, ña kuzunguka upande wa pili, sehemu alipo anguka mpenzi wake. Kwa haraka nikamvua nguo mpenzi wake, na kuzivaa mimi japo hazinitoshi sana ila nikazilazimisha kukaa mwilini mwangu.
Nikachukua soksi za jamaa, na kumkandamiza nazo mdomoni, kisha nikamnyanua na kufungua, uoande wa pili wa gari. Kwa bahati nzuri nikakuta kamba, kwa haraka nikamfunga miguuni na mikononi. Kisha nikamuwena vizuri nyuma ya gari, hii yenye viandishi vidogo vilivyo andikwa Verosa, kisha nikafunga, nikarudi alipo mpenzi wake.
Nikamkuta akihangaika na simu yake, akijaribu kupiga namba anazo zijua yeye, kwa bahati mbaya, maeneo tuliyopo hakuna mawasiliano.
Nikampokonya simu yake na kuiweka mfukoni mwangu
“Ukijaribu kufanya ujinga wowote, nitakuu”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali nikitumia lugha ya kingereza, jambo lililo mfanya binti huyo kushangaa, kwani nahisi alijua kwamba mimi ni mtu misiye jua lugha yoyote zaidi ya lugha ya jamii niliyo tokea
Nikawasha gari na kuondoka, huku mara kwa mara niki muamrisha binti huyu kunielekeza barabara ya kufika kwenye mji wowote. Mwendo wa karibia masaa tisa, tukafika kwenye moja ya mji wenye nyumba, nyingi sana zilizo tengenezwa kwa mbao
“Hapa ni wapi?”
“Soweto”
Casey alinijibu kwa kifupi huku, akiwa amenuna, kwani hajafurahishwa na uwepo wangu mimi, ndani ya gari hili. Nikasimamisha gari nje ya baa moja, iliyo tulia sana,
“Mbona umesimamisha gari?”
“Nahisi njaa, nahitaji kula, nipatie pesa”
Casey akanitazama kwa woga, taratibu akaingiza mkono wake kwenye, mfuko wa suruali aliyo ivaa, akatoa noti moja ya dola mia na kunikabidhi, nikafungua mlango, kabla sijashuka, nikamgeukia Casey.
“Shuka ndani ya gari, tuongozane”
Casey hakuwa na kipingamizi zaidi yakushuka kwenye gari, tukaingia ndani ya baa hii kwa bahati nzuri tukakuta, sehemu wanauza chakula
“Wewe unaitwa nani?”
Casey aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendelea kukisubiria chakula tulicho kiagiza
“Eddy”
“Una jina kama la mchumba wangu”
“Yupi, huyo niliye mfungia kwenye buti ya gari?”
“Hapana, huyo ni kaka yangu, mpenzi wangu yupo hospitali”
“Anaumwa na nini?”
“Alishambuliwa na majambazi, wiki moja iliyo pita”
“Ohoo pole saña, ila hali yake inaendeleaje?”
“Sio nzuri, kwani yupo chini ya uangalizi wa madaktari, kwani alipigwa risasi nne za kifua, alipokua anapeleka pesa benki”
Casey alizungumza kwa sauti yaunyonge huku kwambali nachozi yakimlenga lenga, tukachukua chakula tulicho kiagiza na vinywaji, tukarudi kwenye gari
“Eddy nakuomba kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Ninakuomba umfuñgulie kaka yangu, nahisi atakuwa anajihisi njaa”
Casey aliniomba kwa utaratibu, nikamtazama kwa umakini, machoni mwake
Nikamkabidhi mfuko wa chakula nilicho kishika, nikazunguka nyuma ya gari, nikajifikiria kwa muda kisha nikakishika vizuri kitasa cha kufungulia buti ya gari.
Kabla sijafungua, gari ya polisi, ikasimama nyuma yangu, jambo lililo nifanya nisitishe zoezi, nikaanza kuondoka, nyuma ya gari
“Hei kijana”
Sauti ya askari mmoja ikaniita, nikageuka kwa kujiamini, na kuwatazama askari wawili walio simama mbele ya gari lao, dogo linalo endana na gari ninalo liendesha.
“Njoo”
Nikapiga hatua kurudi walipo, askari hawa walio zichomeka bastola zao viunoni mwao
“Fungua, buti ya gari. Tunahitaji kukagua gari yako”
Alizungumza askari mmoja huku akinifwata sehemu bilipo simama, nikaanza kuchanganyikiwa baada ya Casey kushuka ndani ya gari na kuja tulipo
“Ofisaa”
Casey alimuita askari mmoja, aliye simama akitutiza, Casey akanitazama kwa macho makali, jambo lililo wafanya askari hao kuipeleka mikono yao kwenye bastola zao walizo zichomeka viunoni.
Nikataka kurudi nyuma, ila nikajikuta miguu ikipata uzito wakutekeleza azma yangu ya kurudi nyuma. Askari wakazichomoa bastola zao, kwa haraka wakatusukuma mimi na Casey, tukaanguka chini.
“Laleni chini”
Askari mmoja alizungumza kwa sauti ya juu huku akianza kutambaa, wakielekea ilipo baa, tuliyo toka muda mchache. Milio ya risasi ikaanza kurindima, ndani ya baa, nikatazama vizuri, nikashuhudia kundi la majambazi walio valia makofia meusi vichwani mwao, yaliyo bakisha sehemu za macho yao, wakiwamrishà watu waliomo ndani ya baa hiyo kutoa walivyo navyo.
Ikawa kama mkanda wa kuigiza, kwani majambazi hao walianza kuwashambulia askari hao walio kua wakitambaa, mmoja wao, akapigwa risasi ya kichwa na mmoja wa majambazi, na ukawa ndio mwisho wa askari huyo, aliyetoka kuzungumza na Casey muda mchache ulio pita.
Nikamtazama Casey, na kumuona akijaribu kunyanyua kichwa chake kuchungulia upande walipo majambazi hao, na akaanza kupiga mayowe yaliyo wafanya majambazi kutazama eneo lilipo gari, letu.
“Weka kichwa chako chini, Casey”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali, huku nikibingiria kwa haraka, na kumuwahi Casey aliyekuwa ameshikwa na butwaa, akimshuhudia askari aliye zungumza naye, jinsi ubongo wake ulio changanyikana na damu, ulivyo sambaa chini.
“Heiii, nisikilize wewe”
Nilizungumza huku nikimpiga piga Casey mashamvuni, ili arudi katika hali yake ya kawaida.
“Eheeee!”
Alizungumza huku akiwa amenitumbulia mimacho, asijue nini azungumze. Gari yetu ikaanza kushambuliwa kwa risasi na majambazi hao, huku sisi tukiwa upande wa pili wa gari hili. Nikatazama upande lilipo gari la polisi, nikachungulia kupitia durisha la gari, tulilopo nikao majambazi wawili wakilisogelea gari letu huku wakiendea kuzimimina risasi kwenye upande wa pili wa gari letu.
“Hei Casey, unaweza kutambaa?”
“Heee”
“Unaweza kutambaa?”
Casey akanijibu kwa kutingisha kichwa kwamba anaweza.
“Nakuomba, utambae uende lilipo gari lapolisi”
“Eddy una akili kweli wewe, unataka na mimi nife kama hao polisi?”
Casey alizungumza kwa sauti ya kuto kujiamini huku akinitazama usoni, huku jasho likimtiririka.
“Fanya kama nilivyo zungumza”
Nilizungumza, huku nikiwachunguli majambazi hao, wanao zidi kulisogelea gari letu lilipo.
Casey hakuwa na uchaguzi mwengine zaidi yakufanya nilivyo muambia kufanya. Kwa haraka akatambaa hadi lilipo gari la polisi na kujibanza huku akihema sana, macho yake yote yakawa kwangu. Ukimya ukatawala gafla, kwani majambazi waliacha kupiga risasi, nikachungulia nikawakuta wakinong’onezana, mmoja akaanza kunyata taratibu, akilisogelea gari nililopo, huku bunduki yake akiwa ameiishika vizuri mkononi mwake.
Nikakichomoa kisu changu, na kukishika kwa mkono wangu wa kulia. Taratibu nikanza kuhesabu moja mpaka tatu, kitendo cha jambazi huyo kuufungua mlango wa gari, upande wa dereva, ikawa ninafasi yangu kufanya shambulizi la kukirusha kisu changu kwa nguvu zangu zote, kisu changu
kikatua shingoni mwa jambazi aliye simama, hatua chache toka gà ri lilipo, akatoa ukelele ulio mduwaza mwezake, aliye karibu yangu. Kwa haraka nikapanda juu ya gari, nikajizungusha kwa kasi, kwakuitumia miguu yangu, na kumpiga kichwani jambazi, akaanguka chini. Nikawahi kuochomoa bastola iliyo kiunoni mwake, na kumpiga risasi kadhaa za tumbo.
Nikakimbia kwa haraka, hadi kwenye moja ya gari, lililopo kwenye maegesho ya hapa baa, nikajibanza kutazama ni kitu gani kinacho endelea ndani ya baa. Jambazi mmoja akajitokeza mlangoni kuwachungulia wezake, alipo waona wamelala chini, akarudi ndani kwa haraka, sekunde kadhaa wakatoka majambazi wanne, wakaanza kufyatua risasi zao ovyo, pasipo kujua muhusika mkuu wa mauaji ya wezao wawili yupo wapi.
Sikuhitaji kufanya makosa, ambayo yangenigharimu maisha yangu. Kwa haraka nikanza kufyatua risasi zilizo wapeleka chini, majambazi wote wanne, Nikatoa magazini ya bastola, nikskuta imebakiwa na risasi nne tu.
“Shitii”
Nilizungumza huku nikiirudisha kwa harana Magazine hiyo ndani ya bastola, nikanyanyuka kwa umakini, nikaanza kukimbilia katika mlango wa kuingilia baa.
Nikachungulia na kuwakuta watu wote wakiwa wapo chini ya ulinzi mlali wa majambazi sita waliomo ndani ya baa hii, iliyo kusanya wateja wengi.
Jambazi mmoja, akajisumu kutoka nje, nikamrukia kwa nyuma na kumkaba kabali, huku nikimvuta pembeni kabisa ya mlango. Taratibu jambazi huyu akaanza kuiaga dunia, kwa nguvu zangu zote nikaivunja shingo yake.
“Nisalimie huko uendapo”
Nikamlaza chini, taratibu nikachukua bunduki yake à ina ya ‘Short Gun’, Nikamvua jaketi lakuzuia risasi alilo livaa, nikaanza kushangaa baada ya kuguñdua jambazi huyu ni mwanamke.
Nikalivua kofia lililopo kichwani mwake, sikuamini macho yangu, kwani ni binti mdogo sasa, jinsi anavyo onekà ña usoni mwake.
“Umekosa nini, binti mzuri kama wewe?”
Nilizungumza huku nikilivaa jaketi la kuzuia risasi. Kazi ikawa ni moja tu, kuhakikisha ninawamaliza mambazi wote. Haikuwa ngumu kwangu, kwani ndani ya dakika kadhaa nikafanikiwa kuwaua majambazi wote ndani ya baa hii. Mtu mmoja akaanza kupiga makofi, mwenzake wa pembeni naye akafanya hivyo, watu wote waliomo ndani ya baa wakaaendelea kunipigia makofi kwa kazi nzuri niliyo ifanya.
“Asanteni”
Nilizungumza, kwa kizulu jambo lililo zidi kuwafurahisha, walio na simu zao wakawa na kazi ya kunipiga picha, huku wengine wakichukua video. Casey akanifwata na kunikumbatia, huku akitokwa na machozi
“Vipi?”
Nilimuuluza kwa wasiwasi, huku kitu cha kwanza kukifikiria kichwani mwake ni kaka take, niliye muacha ndani ya buti ya gari lililo shambuliwa vibaya kwa risasi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com