SEHEMU YA THEMANINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Tukapanda kwenye farasi, na kuindoka katika eneo tulilo kuwa. Tukà fika karibu na kijiji, nikashuka kwenye farasi na kumuacha Lutfia atangulie kududi, ili kuepusha hisia mbaya zitakazo jengwa miongoni mwa wanakijiji, dhidi yetu.
Nikafika kwenye kijumba changu, sikuingia ndani nikatafuta mti uliopo karibu na kijumba changu nikapanda, kutokana ni usiku sikuhitaji nilale ndani, kwani bado nimapema.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Nimepakbuka nyumbani” Nilijisemea kimya kimya
“Nitarudije lakini?”
“Hakuna jinsi nilazima nitoroke hapa ki…..”
Nikastushwa na mlio mkali wa king’ora kilichopo hapa kijijini, moti mkali kutoka kilipo kijiji, ukaniogopesha na kunifanya nikae kwa umakini, kuchunguza ni nini kinacho endelea, kelele za wamama na watoto zikazidi kurindina kijiji kizima, huku moto ukiendelea kuteketea. Kwa haraka nikashuka juu ya mti, nikaanza kukimbia kuelekea kilipo kijiji, kabla sijafika, nikashuhudia jinsi wanakijiji wanavyo uliwa na watu wenye bunduki, pamoja na mabomo yakurusha kwa mkono
“Ohhh Mungu wangu!”
Nilihamaki huku nikiwa, sihui chakufanya. Baadhi ya askari wakijiji, wameanguka chini baada ya kushambuliwa kwa risasi, kitu kiluchozidi kunichanganya ni baada ya kumuona Lutfia akiwa amezingirwa na watu hao wenye bunduki nzito na mara nyingi bunduki hizi hutumika kwenye vita vya mataifa makubwa kama Marekani.
“Upanga hauto saidia chochote”
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kujibanza kwenye mti mkubwa, nikishuhudia jinsi wanakijiji wanavyo patishwa matesona watu hao.
Mlio mkali wa helcoptar, ukasikika ukitokea mashariki mwa kijiji, nikaichungulia Helcoptar hiyo, nikaishuhudia ikitua taratibu sehemu yenye uwazi, ambapo ndipo walipo kusanywa wanakijiji, pamoja na chifu wao. Askari mmoja kati ya wengi walio kishambulia kijiji, akakimbilia hadi sehemu ilipo Helcoptar, akafungua mlango, wa helcoptar.Akashuka mwanadada mmoja aliye valio nguo nyeusi, kuanzia juu hadi chini, huku kichwa chake akikivisha kofia nyeusi, huku baadhi ya nywele zake akizishusha eneo la uso wake na kufucha jicho moja kama anavyo fanya mwanadada, mwanamuziki Rihana.
Akashuka jamaa mwengine, ambaye naye amevalia nguo nyeusi, kofia pamoja na miwani nyeusi. Wakapiga hatua hadi, walipo wanakijiji walio wekwa chini ya ulinzi. Wakaanza kuwakagua wanaume wote, walio amrishwa kupiga magoti, huku mikono yao wakiwa wamevishika vichwa vyao. Jamaa huyo akaanza kurusha rusha mikono kama mtu aliye changanyikiwa, baada ya kukagua wanaume wote, akaivua kofia yake na kuitupa chini.
Nikastuska, baada ya kuiona sura ya mtu huyu, ambaye usoni mwañgu si mgeni sana japo jiña lake, bado halinijii kichwani kisawasawa, akamfwata chifu, aliye pigishwa magoti kwa amri ya wa ajeshi hao. Akaichomoa bastola yake kiunoni na kuielekezea kichwani mwa chifu
Kutokana na umbali waliopo sikuweza kusikia nimaswali gani anayo muuliza çhifu, anaye kuwa mbishi kujibu, gafla nikamuona Lutfia akimsukuma jamaa huyo aliyekuwa akihitaji kumfyatulia baba yake risasi, kwa jinsi vitendo anavyo vifanya Lutfia, vinaashiria kumuimba jamaa huyo, amuadhibu yeye na si baba yake.
Jamaa akamtandika Lutfia kichwani, kwa kutumia kitako cha bastola yake, nakumfanya chifu anyanyuke kwa hasira, kabla hajamkabili jamaa huyo, msichana aliye shuka naye kwenye Helcoptar, akafyatua risasi kadhaa zilizo muangusha chifu chini kama gogo kubwa.
“God…!”
Niligamaki, huku nikimshuhudia Chifu, anavyo tapatapa chini, akikata roho, askari mmoja wa kijiji akajaribu kunyanyuka, ila akarudishwa chini kwa risasi, alizo pigwa kwenye miguu yake. Jamaa akachukua kipaza sauti na kuanza kuzungumza
“Natambua upo hapa kijijini, nipo hapa kwa ajili yako, rafiki yangu kipenzi Eddy”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio hukunikijiiza swali, ni kwanini hawa watu wapo kijijini kwa ajili yangu.
“Hutaki uje tupige stori? Njoo basi rafiki yangu Eddy. John nipo hapa ninakusubiri”
Hasira ikazidi kuyaongeza kasi mapigo yangu ya moyo, picha kadha kichwani mwangu zikaanza kujirudia kwa kasi, kama mkanda wa video, unao rudishwa nyuma. Picha za kumbukumvu zikasimama, katika tukio la John, kunipiga risasi za kifua baada ya mke wangu Phidaya kujifungua, miguuni mwangu
“Ohhhh Eddy, hutaki? Basi ngoja niondoke zangu.Ila kabla sija ondoka nina ujumbe kutoka kwa mke wako na mwanao Jimy”
Maneno ya John yakazidi kunichanganya, sikua na lakufanya kwabi askari wake wapo zaidi ya hamsini na wote wana bunduki mikononi mwao.
“Mke wako, na mwanao wanakuhitaji rafiki yangu. Ndio maana nikaamua kuja kukutafuta, baada ya kusikia upo hà i. Kaka mimi na wewe ni marafiki wa damu. Tafadhalu njoo twende nyumbani, ukamuone Jimy wako”
Maneno ya John yaliyo jaa ushawishi, wakibinadamu sikuyapa nafasi katika kichwa changu, kwani asinge fanya alicho kifanya kwa wanakijiji wezangu
“Ohhh ngoja nimpigie simu, umsikie mkeo”
John akatoa simu yake mfukoni, akaiweka sikioni mwake kwa sekunde kadhaa, kisha ajaisogeza karibu na kipaza sauti chake
“Mume wangu Eddy, ninakupenda sana.Nimeishi mbali nawe kwa miaka mitatu sasa, ninakuomba urudi nyumbani, mwanao ananisumbua kila siku kusema baba, baba.”
“Nakuomba Eddy wangu, urudi. Ngoja nimsikilizishe mwanao simu. Jimy talk to dady”(….Jimy zungumza na baba)
“Halloo Dady, where are you? I mis you. Came back home”(Halloo baba, upo wapi? Nimekukumbuka, rudi nyumbani)
Sauti ya mtoto mdogo ilisikia vizuri masikioni mwangu, jambo lililozidi kunitatiza nakunipa wakati mgumu sana, japo sauti ni yamke wangu Phidaya ila sikufanya maamuzi yoyote kwenye kichwa changu
“Muambiw baba, umekua wa kwanza darasani”
Sauti ya Phidaya ilimuamrisha mtoto huyo anaye semekana niwakwangu
“Dady nimekua first in class”
Mtoto, alichanganya kiswahili na kingereza, jambo lililo nipa wasisi wa kuhisi kuna kamchezo kanacho endelea katikati yao. John akakata simu na kujikoholesha kidogo
“Eddy umesikia hiyo. Mke wako, mwanao, wote wanakuhitaji wewe. Njoo twende zetu rafiki yangu”
John alizungumza huku akitazama kila pande ya eneo walilopo, akitarajia kuniona, tarativu nikajikuta nikikaa chini, huku machozi yakinimwagika. Nikautazama upanga wangu kwa umakini, kisha nikachungulia walipo, nikamuona John akikikamata kitoto kimoja chenye umri wa miaka kama mitatu
“Eddy mwanao anafanania na huyu”
John ilizungumza huku akimbembeleza bembeleza mtoto huyo, anaye lia kwa sauti ya juu, hii ni baada ya kutolewa kwenye mikono ya mama yake aliye lazwa chini
“Eddy muda unakwenda, njoo tuondoke. Sasa hivi ni saa saba usiku. Unasubiri ninj rafiki yangu. Au unataka ukae na hawa watu wako, walio vaa nusu uchi eheees?”
John aliendelea kuzungumza huku, akizunguka zunguka katika eneo walilopo, mkononi akiwa na mtoto aliye endelea kupaza sauti ya mayowe.
Gafla John akamgeuza mtoto, kichwa chini, miguu juu, huku akiwa amemshika kwa mkono mmoja, mguu wakulia.
Kitendo cha John kumshika, mtoto huyo hivyo, kikanikumbusha jinsi Derick alivyo mshika mtoto wangu, niliye zaa na Madam Mery.
“Eddy hujui ni jinsi gani, ninavyo chukia kupotezewa muda. Huku mijitoto inayo lia kama hii, inavyo zidi kunicchanganya akili yangu”
John akakitupa kipaza sauti chini, pasipo kua na huruma, akachomoa bastola yake na kuzimimina risasi kadhaa tumboni mwa mtoto huyo, na kumtupa chini kama mzoga
“Fuc……”
Nilizidi kupandwa na hasira iliyo ufanya mwili wangu wote kutetemeka. Vilio vya wamama vikazidi kuutesa moyo wangu, nikamuona John akikiokota kipaza sauti, huku akicheka kwa dharau
“Ohhhhh Eddy, naondoka, ila hili ulilo liona linakwenda kumkuta mwanao Jimy”
John akamrushia kipaza sauti, msichana aliye kuja naye, naye akamkabidhi askari mwengine kipaza sauti. Wakaondoka, wakaingia kwenye Helcoptar yao na kuondoka.
Askari wao wakaondoka kwa umakini, na kutokomea pasipo julikana.
Nikasubiri kwa muda, wa nusu saa, ndipo taratibu nilipo anza kutembea walipo wanakijiji wanao omboleza kwa machungu, vifo vya wapendwa wao. Kila mwanakijiji anaye niona, ananitazama kwa macho makali yaliyo jaa jazba.
Macho yangu yakakutana na macho ya Lutfia, aliye pembeni ya mwili wa baba yake, aliye fariki dunia. Nikatembea kwa haraka hadi ulipo mwili wa chifu, kabla sijaugusa, nikastukia, Lutfia akinisukuma kwa nguvu na, nikaanguka chini
“Eddy, hupaswi kuugusa mwili wa baba yangu. Haya yote wewe ndio chanzo. Umekisababishia kijiji changu matatizo….”
“Lutfia ila si mimi niliye waua hawa wote”
“Wewe, ni chanzo Eddy, nakuanzi sasa hivi ninakuomba uondoke kijijini kwangu, la sivyo utakwenda kuungana na kifo cha hawa wote walio tangulia mbele za haki”
Lutfia alizungumza kwa msisitizo, huku machozi yakimwagika, ñà kifua chake kikipanda na kushuka kwa kasi akionekana kujawa na jazba kubwa dhidi yangu.
“Lu…..”
“Eddy nimesema ondoka”
Lutfia alizungumza kwa kupaza sauti, hadi wanakijiji wote wakatutizama sisi, natambua hawajui lugha tunayo izungumza ila, matendo yanaashiria kwamba Lutfia hataki kuniona mbele ya macho yake. Nikamtazama Chifu, huku machozi yakinilenga lenga. Midomo ya Lutfia, inatetemeka kwa kufura kwa hasira, uzuri wake alio kua nao umetoweka kabisa.
Taratibu nikauweka chini upanga wangu, kisha nikasimama na kutazamana na Lutfia aliye nitumbulia mimacho kiasi cha kunifanya nimuogope. Kila mwana kijiji ninaye mtazama sura yake imetawaliwa na majonzi mengi, wamama wengine wakiwa wanalia kwa uchungu huku wakigara gara kwenye vumbi, wakionyesha ni jinsi gà ni, walivyo umizwa na tukio zima lililo tokea muda mchache ulio pita.
Sikumuangali mtu yoyote usoni zaidi ya kugeuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka, ulio changanyika na hasira kali. Nikafika kwenye kijumba changu, nikachukua kibuyu changu, ninacho hifadhia maji ya kunywa, nikachukua na kisu changu cha akiba, na kutoka nje ya kibanda changu. Nikautizama mji jinsi unavyo teketea kwa moto, hasira dhidi ya John ikazi kunipanda. Nikaanzà kutokomea msituni, nikijaribu kutafuta njia ya kutokea kwenye kijiji hiki, kutokana na hasira pamoja na uchungu ulio nitawala moyoni mwangu, nikajikuta nikitembea hadi kuna pambazuka, pasipo kuchoka.
Nikafika kwenye moja ya mlima mrefu, ulio zingirwa na miti mingi, kwa mbali nikaanza kusikia mngurumo wa gari, likipita eneo la karibu na mlima huu, kwa haraka nikashuka, nikiufwatisha mgurumo huo ni wapi unapo tokea. Kwabahati nzuri nikaiona barabara ya lami, iliyo chongwa kwenye mlima huu. Matunaini ya kufika ninapo pahitaji yakaanza kunijia moyoni mwangu.
Nikasimama, katikati ya barabara. Sikuona aibu kwa jinsi nilivyo vaa nusu uchi, huku sehemu zangu za siri, zikiwa nimezifunika na ngozi ya chui. Mlio wa gari sikuusikia tena, kwani ninahisi lilisha pita, kabla ya mimi kuifikia barabara. Nikaendemea kuzunguka zunguka maeneo ya barabara, nikijaribu kusubiria kama ninaweza kupata usafiri.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com