SORRY MADAM (92)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA TISINI NA MBILI ILIPOISHIA... Nikalirudisha kwa haraka upande wa kushoto ambapo ndipo ninapo stahili kupita, dereva wa gari ambaye alikuwa upande mmoja na mimi, nikastukia akigongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo, tukio lililo mstusha mwenzake ambaye nipo naye upande mmoja. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Akajikuta akifunga breki, bila hata ya kutegemea gari lililo kuwa nyuma yake, likamvaa na yote kwa pamoja yakatoka nje ya baranara huku yakizunguka, na kutimua vumbi jingi, huku vyuma vya magari yao vikisagika ikiashiria kwamba yana gongonga kwenye mawe makubwa yaliyopo pembezoni mwa barabara. Nikakanyaga breki, kusimamisha gari. Nikashusha pumzi nyingi, huku nikilitazama vumbi likielea angani. “Kila mmoja yupo salama?” “Ndio” “Ndio” “Ndio” Kila mmoja alijibu kwa wakati wake, nikatazama upande wa mbele tulipo tokea, sikuona gari lolote likija, saa iliyopo pembeni yangu inaonyesha ni saa kumi …