SEHEMU YA TISINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Nikalirudisha kwa haraka upande wa kushoto ambapo ndipo ninapo stahili kupita, dereva wa gari ambaye alikuwa upande mmoja na mimi, nikastukia akigongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo, tukio lililo mstusha mwenzake ambaye nipo naye upande mmoja.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Akajikuta akifunga breki, bila hata ya kutegemea gari lililo kuwa nyuma yake, likamvaa na yote kwa pamoja yakatoka nje ya baranara huku yakizunguka, na kutimua vumbi jingi, huku vyuma vya magari yao vikisagika ikiashiria kwamba yana gongonga kwenye mawe makubwa yaliyopo pembezoni mwa barabara.
Nikakanyaga breki, kusimamisha gari. Nikashusha pumzi nyingi, huku nikilitazama vumbi likielea angani.
“Kila mmoja yupo salama?”
“Ndio”
“Ndio”
“Ndio”
Kila mmoja alijibu kwa wakati wake, nikatazama upande wa mbele tulipo tokea, sikuona gari lolote likija, saa iliyopo pembeni yangu inaonyesha ni saa kumi na moja alfajiri. Taratibu nikaliemdesha gari hadi, hadi zilipo gari hizi mbili.
“Bakini ndani ya gari”
Nilizungumza kwa kujiamini, nikaichukua bastola yangu niliyo kuwa nimeiweka pembeni mwa siti, niliyo kalia. Nikafungua mlango wa gari na kushuka, huku nikiwa makini sana na tayari kwaa lolote litakalo jitokeza mbele yangu.
Nikafika ilipo gari ndogo, na kumkuta dereva akiwa amelalia mskani wake, ulio mbana maeneo ya kifuani. Nikamchunguza na kugundua bado anahema kwa shida, huku damu zikimtoka puani na mdomoni.
“Ni…ss..aid..ie”
Aliniomba msaada huku akinitaza kwa macho yaliyo mtoka. Mithili ya mtu aliye kwabwa na kitu kizito kooni.
“Nani aliye kutuma?”
“Nisa….i..die…ni.tamtaj….a”
Nikaikoki bastola yangu kuziandaa risasi kutoka, kidole changu kimoja kikianza kuivuta traiga, taratibu, huku nikiwa nimemuelekezea bastola kichwani kwake.
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho. Ninani aliye watuma?”
Jamaa alipo litazama shimo dogo, la kutolea risaai la bastola, akayarudisha macho yake usoni mwangu.
“J….oh..n”
Jamaa, alinijibu kwa shida kubwa sana, na kichwa chake kikalegea, akiashiria ameiaga dunia. Kwa hasira nikamsindikiza huko aendapo kwa risasi moja iliyo tua kichwani mwake.
Nikasikia sauti ya mtu akikohoa kwenye gari, tulilo liacha sehemu ya tukio.
Nikaanza kutembea kwa umakini, huku bastola yangu nikiishikilia vizuri, nikamkuta yule amlinzi tuliye muacha eneo la tukio, akiwa amekaa chini huku ameliegemea gari, mkono wake mmja akiwa amejishika tumboni mwake, kunapo vuja damu nyingi, sura yake ikiwa imechanika chanika kwa kuchwana na vipande vya vioo vya gari.
Alipo niona akatabasamu kidogo, huku akikohoa na kumwaga madonge ya damu mdomoni mwake.
“Muheshimiwa yu..po salama?”
“Ndio yupo salama”
Nilimjibu, huku nami nilipiga goti chini, nikijaribu kumtazama ni nini kilicho mpata sehemu ya tumbo.
“Asante kwa msaada wako, wewe ni mwanaume shujaa.”
Alizungumza huku, akitabasamu na kukohoa juu.
“Damu nyingi, imenitoka. Suwezi pona”
Alizumgumza maneno haya baada ya kujaribu, kumpa huduma ya kwanza. Akanishika mkono wangu wa kulia
“Toa pochi yangu, kwenye……mfuko wa nyuma”
Nikaitoa pochi, akaniomba niifungue na kitu cha kwanza kukiona na kitambulisho chake chenye jina la George Jr.
“Fungua, upande wa pili”
Nikafungua na kukuta, picha mbili moja akiwa mdogo na nyingine akiwa amesimama na msichana aliye nifanya niitumbulie mimacho picha hiyo.
“Chukua hii chane, naomba umtafute dada yangu anaitwa Victoria, umkabidhi hii cheni.”
George Jr. Alinikabishi cheni aliyokua ameivaa shingoni mwake. Huku taratibu, akianza kuyapepesa macho yake. Akanyayua mkono wake taratibu, huku alitetemeka, akanipigia saluti na kukata roho.
Taratibu machozi yakaanza kunimwagika, nikayafunika macho yake kwa kupitia kiganja cha mkono wangu wa kulia. Nikageuka nyuma, nikamkuta baloIi akiwa amesimama na watoto wake, huku Casey machozi yakimwagika. Nikanyanyuka taratibu, na kwenda lilipo gari na kuingia. Nikaitazama picha ya George aliyopiga na Victoria. Nikajikuta donge la hasira likinibana kifuani mwangu.
Nikasikia milio ya helcoptar, nikawasha gari kaa haraka, ila Casey akanikimbilia
“Eddy tupo, salama hao ni wanajeshi wa Marekani, wanakuja”
Casey alizumgumza huku, akichungulia dirishani. Helcoptar mbili zikashuka hewani na kusimama, katikati ya barabara. Wakashuka wanajeshi wengi, wenye bunduki mikononi. Balozi akaanza kuzumgumza nao, huku kaka yame Casey, akipewa nguo ajisitiri mwili wake.
Wakatuchukua, sote wanme na kuondoka huku, Helcoptar nyingine ikibaki, na wanajeshi kadhaa wakiupima pima mwili wa George Jr.
Tukafika makao, makuu ya jeshi la Marekani lililopo hapa, nchini Afrika kusini. Tukapewa huduma za kwaza ikkwemo vifungua kinywa, kwani hatukupa chakula kwakipindi kirefu. Matumbo yalipo kaa sawa, nikatambulishwa mm wa baadhi ya wakuu wa jeshi. Wengi wao wakanisifu kwa kazi nzuri na pevu, niliyo ifanya.
Tukapelekwa kwenye moja ya hoteli kubwa, tukiwa chini ya uangalizi mkali wa jeshi. Balozi Brayan Daniel, hakusita kunitambulisha kwa kila rafiki yake ambaye, huku akinimwagia sifa kedekede.
Tukakaa hotelini, kwa siku nne, ambapo Balozi Brayan Daniel akaendelea na majukumu yake ya kazi, huku akiniomba niwaliende watoto wake kwa kipkndi kifupi kabla hatujaenda Marekani, kuhudhuria mazishi ya askari walio kumbwa na tukio la uvamizi.
Mida ya saa sita mchana, ikafika gari katika hoteli tuliyopo, huku akija muwakilishi wa balozi, akituomba twende ofisini kwake, tukakutane na baadhi ya viongozi wa hapa nchini Afrika kusini. Tukajiandaa, kila mmoja akavalia mavazi tuliyo numuliwa siku kadhaa, tumaingia ndani ya gari, huku mimi nikiwa makini kuhakilisha Casey na kaka yake wapo salama salmini.
Tukafika kwenye ofisi za ubalozi wa Marekani, tukapokelewa vizuri na kupelekwa kwenye ofisi za balozi, ambapo tulimkuta yupo na watu baadhi, wanao onyesha kua ni viongozi. Tukakaa kwenye viti vilivyo andaliwa kwa ajili yetu.
“Jamani mutatiwia radhi kidogo kwa kuchelewa kufika kwenye halfa hii”
Sauti ya John, ilisikika kutokea mlangoni, akiingia akiwa ameongozana na Victoria, mpenzi wake.Pasipo kutazama waliopo ndani ya ofisi John na Victoria, wakakaa kwenye viti vyao na kukamilisha idadi ya watu ishirini na tano, tuliomo humu ndani, Nikaivua miwani yangu nyeusi niliyo ivaa, nikamuona John, akilegeza mdomo wake kwa kunishangaa, huku naye Victoria akiinamisha kichwa chini kwa aibu, wasiju nini cha kufanya. Huku nikiwakazia macho yaliyo jaa hasira kali kama Simba.
Ukimya wa sekunde kadhaa, ukakatiza huku macho yangu nikiyahamisha kutoka kwa John, kwenda kwa Victoria. Swali la kwanza kujiuliza ni kuhusiana na John anahusika kivipo kwenye huu mkutano, hiyo moja mbili anamahusiano gani na balozi wa Marekani bwana Brayan Daniel.
“Nashukuru kwa kufika kwenu, kwa maana nyinyi ni wachache kati ya wengi nilio tamani wafike hapa.”
Balozi B.Daniel alizungumza huku akiwa amesimama.
“Lengo langu la kuwaita hapa, ndugu zangu, ni kumtambulisha shujaa wangu, aliye jitolea kuyaokoa maisha yangu na familia yangu.”
“Huyu ninaye mzungumzia hapa si mwengine bali ni Eddy Godwin.”
Balozi alininyoonyea mkono, watu wote wakapigaiwemo Jonh na Victoria.
“Japo nimepatwa na pigo, lakuwapoteza vijana wangu, kumi katika shambulio lile, Ila kusema ukweli ni jbo la kumsukuru sana Mungu, kwa kijana Eddy kujitokeza na kuweza kuitetea nafsi yangu. Pasipo kujali yeye ni nani, ila ni kitu kikubwa sana kufanywa na mtu wa kawaida.”
Kila muda ulivyo zidi kwenda, ndivyo nilivyo jikuta nikizidi kupandwa na hasira kali, hata yañayo zungumzwa ndanivya hichi chumba sikuweza kuyasikia hata kdogo.
Matukio baadhi aliyo yafanya John, yakanza kunisumbua akilini mwangu, taratibu nikajikuta nikitokwa na machozi ya uchungu sana. Casey akaniangalia kwa muda, kwa haraka akanifwata nilipo kaa
“Eddy una tatizo gani?”
Watu wote wakabaki wakitutizama mimi na Casey. Mapigo ya moyo hayakusita kunienda mbio hadi nikaanza kujihisi kizungu zungu. Nikaanza kujishangaa, baada ya kuona jinsi matone ya damu yakianza kunitoka puani
“Muiteni dokta”
Nikajaribu kunyanyuka, ila kizunguzungu kikali, kikaniyumbisha kabla sijaenda chini, Casey aksniwahi, akisaidiana na kaka yake.
Macho yakaanza kujaa ukungu mwingi ulio nifanya niwaine watu wawili wawili. Nikamuona John, akitabasamu. Huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia.
“Tupeni nafasi, tumuhudumie.”
Sauti za madkari, nilizisikia kama sauti ya kengele zinazo gongwa.
“Nakufa”
Nilizungumza kwa sauti ya chini, sana, huku nikizidi kujihisi vibaya.
***
Nikastuka gafla, kabla sijanyanyuka, nikastukia nikirudishwa chini, kitandani na dada mmoja aliye valia mavazi meupe.
“Tulia kaka yangu.”
“Nipo wapi?”
“Hospitali”
“Kwañi ninaumwa?”
“Ndio”
Nikatizama pembeni, nikaona dripu la maji likishusha kiwango cha maji kwenye, mishipa ya mkono wangu wa kushoto, kupitia mrija wake mwembamba ulio unganishwa na sindano yake na kuchomwa kwenye sehemu ya kukunjia mkono.
“Unajisikiaje?”
“Vizuri”
“Basi tulia, dripu hili likiisha, unaweza kuruhusiwa”
“Litachukua muda gani?”
“Mmmmm masaa kama mawili hivi, kwani ndio nimekuwekea muda huu”
Nikajichnguza mwili wangu, na kujikuta nikiwa na mavazi niliyo yavaa, mchana. Saa ya ukutani inaonyesha ni saa moja jioni. Nesi akatoka ndani ya chumba, dakika jadhaa akaingia Casey na kaka yake.
“Unaendeleaje Eddy?” Çasey alizungunza.
“Nipo poa”
“Pole kaka Eddy”
“Asante Bruño”
“Baba yupo, na daktari, wanazungumza kuhusiana na tatizo lako”
“Daktari amesema nina tatizo gani?”
“Amesema kwamba, una….”
Bruno akamziba Casey mdomo asizungumze, anacho taka kukisema kwa muda huu.
“Hapana kaka Eddy, huna tatizo mwaya.”
Nikatabasamu huku nikimtazama, Bruno na Casey, nikatambua kwamba kuna tatizo tu, ila nahisi wameambiwa wasizungumze.
“Mbona umemziba mwenzako mdomo?”
“Hapana, anapenda kuongea ongea sana huyu.”
“Si uniaçhe, nizungumze..”
Bruno akamziba tena mdomo, Casey na kujikuta wakianza kugombaba, kama jawaida yao.
“Heii jamani acheni kugombana”
Casey akatoka chumbani kwa hasira na kuubamiza mlango. Bruno akaachia msunyo mkali na kukaa katika sofa lililomo ndani ya hichi chumba.
“Bruno hivi, mbona unapenda kugombana na Casey?”
“Ahaa domo lake, lipo wazi sana”
“Sawa, hivi yule jamaa aliye ingia, baada ya sisi kufika una mfahamu?”
“Yule ndio nina mfahamu, ni rafiki mkubwa sana wa baba”
“Tangu lini?”
“Kivipi yani?”
“Namaanisha wamejuana lini?”
“Tangu mwaka jana, tunakuja hapa Afrika kusini, tukitokea Marekani.”
“Ahaaa”
“Tena yule John, ana roho nzuri sana. Haswa yule mke wake.”
“Chanzo cha baba, kua rafiki na yule John. Walitoa Hotel yao sisi kuishi tangu tunakuja hadi tulipo pewa nyumba, tuliyo andaliwa. Kwani balozi aliye pita kabla ya baba, alifariki kwa ajali ya ndege.”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com