MAHABA NIUE (40) JINA: MAHABA NIUE Mwandishi: Emmanuel F. Kway SEHEMU YA AROBAINI ILIPOISHIA... Yalikua ni maongezi ya maaskari hao wakiwa ndani ya deffender yao, kweli walifanya kazi iyo kwa hali ya umakini wa juu sana kutokana na vitisho walivyo pewa kutoka ngazi za juu, na kufanya waanze kuhaha kupita kiasi, huku nyuma kukiwa kuna deffender nyingine kweli ulikuwa msako wa kutisha sana ambapo nyuma ya msako huo kulikua na mkono mkubwa kutoka serikalini , KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII SASA ENDELEA... Nyuma ya gari hilo ili fuatiwa na gari ya kway akiwemo LOydah na Joylah. gari zote zili simama pembeni ya kituo cha tandale kwa tumbo, na mmoja wa maskari kushuka na kifaa kidogo mithili ya simu, ambacho kilianza kumuongoza simu waliyokua wakiitafuta ilipo, waliamini kuwa waki mpata huyo mtu wata jua kivyovyote vile Ramsey alipo. hayo ndiyo yalikua mawazo yao katika kila kichwa cha askari, "oyaa mkush! umeona pila lile,"? aliongea mmoja wa mateja huku akimwambia mwenzake, huku akiji kuna k…