MAHABA NIUE (42) JINA: MAHABA NIUE Mwandishi: Emmanuel F. Kway SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI ILIPOISHIA... Kweli wali fanya kazi kwa kuhaha sana wakitumia umakini wa hali ya juu sana, japokua KIKUNDANKYALO , alikua katili ila alimuogopa sana mwasha sababu alikua katili wa chini chini. KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII SASA ENDELEA... "Aisee tukimkosa huku sijui itakuaje!..." alisika akisema kijana mmoja liyekua akiendesha gari hilo. "ni lazima tumpate" KIKUNDANKYALO alisema kwa ghadhabu kubwa huku akitoa mimacho, ilionesha alipania kumuua Ramsey kwani hakutaka kumuangusha bosi wake aliyemuweka mjini. walifika hospitali hapo na kufanikiwa kumkuta Ramsey aliyekua amelazwa hapo. pia walifanikiwa kumuhonga daktari mmoja aliye waahidi kuwapatia mavazi na vitambulisho vya kidaktari ambavyo vingewawezesha kuingia hospitali kwa urahisi na bila kuulizwa na mtu yeyote. wakati yule daktari akishughulika na kufoji vyeti vya kumhamisha Ramsey hospitali uroho wa hela ukiwa umemjaa kama fisi ajavyo…