MAHABA NIUE (49)

Zephiline F Ezekiel
MAHABA NIUE (49)
JINA: MAHABA NIUE Mwandishi: Emmanuel F. Kway SEHEMU YA AROBAINI NA TISA ILIPOISHIA... Baadae aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani, ila bado vita kubwa sana iliendelea baina yake na baba yake KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII SASA ENDELEA... Bado alikua akitaka kumjua muhusika wa ile mimba na kumu haribia binti yake masomo aliapia kuwa akimjua ata muuwa kama sio kumtoa macho au nyongo, ilikua ni kila siku ya Mungu Sabrina alikua akichezea kichapo, Kufikia miezi mitano hali ya Sabrina ilidhofu sana uzuri wake wote ulipotea huku mashavu yakimwingia ndani, kutokana na mateso aliyo kua akiteswa na baba yake ili amtaje mwana ume aliye mpa uja uzito, licha ya mateso yote hayo hakuwa tayari kabisa kumtaja Ramsey , Mateso yalivyo zidi aliamua kutoroka nyumbani na kiasi cha pesa cha shilingi milioni mbili ambazoba ba yake aliwekandani ya kabati, na kukimbia mbali sana ya mji huo na kuamua kupanga chumba . hakuacha kufanya mawasiliano na Ramsey, ambae wakati huo alikua Dar ES SALAAM …