MAHABA NIUE (49)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Baadae aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani, ila bado vita kubwa sana iliendelea baina yake na baba yake
KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII
SASA ENDELEA...
Bado alikua akitaka kumjua muhusika wa ile mimba na kumu haribia binti yake masomo aliapia kuwa akimjua ata muuwa kama sio kumtoa macho au nyongo, ilikua ni kila siku ya Mungu Sabrina alikua akichezea kichapo,
Kufikia miezi mitano hali ya Sabrina ilidhofu sana uzuri wake wote ulipotea huku mashavu yakimwingia ndani, kutokana na mateso aliyo kua akiteswa na baba yake ili amtaje mwana ume aliye mpa uja uzito, licha ya mateso yote hayo hakuwa tayari kabisa kumtaja Ramsey,
Mateso yalivyo zidi aliamua kutoroka nyumbani na kiasi cha pesa cha shilingi milioni mbili ambazoba ba yake aliwekandani ya kabati, na kukimbia mbali sana ya mji huo na kuamua kupanga chumba .
hakuacha kufanya mawasiliano na Ramsey, ambae wakati huo alikua Dar ES SALAAM, alimuonea sana huruma Sabrina
“mwambie baba yako ukweli Sabrina sitaki uteseke kiasi hiko, tafadhali,acha nife tu”!
“siwezi Ramsey, namjua baba yangu vizuri, ata kuua, ila nili kwambia tangu mwanzo kuhusu kutoa hii mimba uka kataa , naomba usinilaumu kabisa”
“najua, nili kwambia usiitoe, mimi nita kuja kukuona kesho kutwa”
“sawa Ramsey nafanya hivi sababu nakupenda sana, kama ulivyo niambia hapo awali, nikutunzie mtoto wako, namimi nita fanya ivyo”
Yalikua ni maongezi kupitia mtandao wa simu ambapo Sabrina aliweza kumuelekeza Ramsey wapi alipo, siri hiyo wana baki nayo wawili tu! Baada ya siku mbili Ramsey aliingia morogoro na kumta futa Sabrina wali furahi sana siku iyo kuonana tena, ilikua ni kama hawa kuonana siku mia moja,
wali furahi na kunywa wote siku nzima , baadae Ramsey aliaga na kurudi Dar es salaam. Hakuna hata mmoja aliye jua kuwa Ramsey huenda moro goro na kurudi Dar es salaam.
Karibia kila mwisho wa wiki ili kujua hali ya sabrina,
“Ramsey pesa zile zina karibia kuisha , sijui ita kuaje na bado mwezi mmoja niji fungue”
“nita jua cha kufanya Sabrina wangu, usijali juu ya hilo”
“uta fanyaje Ramsey wakati bado una soma, pesa uta toa wapi”?
“baba ata nipa pesa za ada, tuna karibia kufungua shule, nita kutumia wewe”
“sasa wewe shule”?
“niachie mimi”
Baada ya wiki mbili kupita kweli Ramsey alitimiza ahadi yake na kumtumia Sabrina pesa nyingi , alizopewa na baba yake za mauzo ya biashara zake apeleke benki pamoja na ada ya shule ila yeye alimtumia Sabrina ili
aende hospitali akajifungue, mzee Felix baada ya kupokea habari za kupotea kwa pesa zile kutoka kwa Ramsey alimpiga na kumvunja mkono wake ila hakuwa tayari nayeye kutaja wapi alipeleka pesa zile nyingi za mauzo ya dukani, alicho mwambia baba yake kuwa aliibiwa . alificha siri nzito sana moyoni,
Miezi tisa ili fika na Sabrina kuji fungua mtoto wa kike hospitali hapo, RAMSEY hakucheza mbali alienda na kumuona mtoto wake, huku akiwa mwenye furaha sana.
“Sabrina rudi tu nyumbani kaombe msamaha alafu mimi nita kuja kwenu”
“uta kuja nyumbani”?
“ndio nitakuja kwenu”
“kufanya nini”?
“kuji tambulisha”
“, usije..RAMSEY, angalia huyo mtoto alivyo fanana nawewe, wewe mtupu”
“muongo wewe, bado mdogo sana”
“ndo nakwambia sasa”,
Waliongea mengi sana wakiwa wenye furaha sana,
Bada ya Sabrina kuji fungua salama salmin
Miezi sita ili pita yote na Sabrina kuamua kurudi nyumbani baada ya kupotea takribani mwaka mzima, alivyo fika nyumbani mama yake alimshangaa sana na kumrukia , sababu alipoteza kabisa matumaini ya kumuona mwanae, baba yake alitoka ndani na kutoamini kama aliye muona mbele yake alikua Sabrina alimfuata na kumkombatia ,
Hali ili endelea kuwa nzuri wakiishi vizuri na motto wa Sabrina ambae walimpa jina la Catherine, huku bibi yake akimuonesha kila aina ya upendo wote, kesho yake kimnya kimnya Ramsey aliiingia moro goro , kwa nia moja tu kwenda kwa Sabrina na kumuona mtoto wake, hakika yalikua ni maamuzi magumu sana,
Ili timu jioni na taratibu Ramsey alianza safari ya kwenda kwa Sabrina moyoni hakuwa na uhakika kama ange toka salama, alijua sana jambo alilokua akitaka kuli fanya lili kua la hatari sana, alipiga moyo konde na kujitosa,
baada ya kufika ali mkuta Sabrina akiwa na mama yake hakika ujio ule uli washangaza sana, mojakwa moja alini jitambulisha, baadae kidogo aliiingia mze huyo mwana jeshi ambaye Ramsey alimjua fika ni baba yake na Sabrina, alisimama na kumpa mkono aki msalimia. , ilikua ni kazi ngumu ni wapi aanzie ila taratibu alianza kujielezea kuhusu mtoto nayeye ndiye alikua baba wa mtoto aliye zaa na Sabrina, hakika lili kua ni jambo la kija siri sana.
“aaaah kijana, kumbe ndo wewe karibu sana nafurahi kuku fahamu”
Baba Sabrina aliongea vile huku akitabasamu na kumshangaza sana Sabrina hakuelewa kwanini baba yake alimpokea Ramsey kwa furaha, alijua wenda angeanza kumpa kipigo ilia ilikua kinyume,
Na alivyodhania
“karibu sana mwanangu hivi walikupa chakula ule”?
“hapana mzee nipo sawa”
“aya mi nipo chumbani, ila nakuja sasa hivi”
Mzee huyo aliondoka huku akiwa na tabasamu
“kumbe mzee mtu poa sana, hana tatizo kabisa”
Alizungumza Ramsey huku akikaa sawa na kuji tanua baada ya kupokelewa vizuri, aliona mambo yameenda vizuri sana kwa upande wake, lakini kwa Sabrina bado alikua na hofu sana, hakutaka kuamini kuwa baba yake alikuwa vile wakati alikua akimuwinda mwanaume aliye mpa mimba na leo hii kamuona, ana muachia kirahisi, .
Katika hali ya kushangaza Ramsey alimuona mzee huyo ametoka huku akiwa na bastola mkononi, ponea yake kwake ilikua sababu mlango ulikua wazi, alitoka kama mshale ulioachiwa kwa nguvu, na kukimbia mbio aliparamia geti bila hata kugeuka nyuma, alijua ange fanya ivyo, ange uwawa pale pale.
“PUMBAVU SANA. NA NINGE MUUWA, MWENDA WAZIMU. NA AMA ZAKE HAMA ZANGU, SHWAIN! “
Aliongea baba Sabrina akiwa bado na jazba nyingi sana baada ya kumkosa Ramsey, chini kwa chini Sabrina na Ramsey walikua wakionana bila wazazi wake kujua, habari izo zina mfikia baba Sabrina na kuamua kumuamisha nchi
na kumpeleka Uganda , ili akate mawasiliano na Ramsey, hapo ndipo walipo potezana na Rarmsey tangu siku hiyo hawa kuwahi tena kuwa siliana..
*******
“LEILA NAOMBA UNIACHIE Ramsey, nili teseka sana, hayo ni machache , mara ya mwisho nili umia sana, nilivyo sikia ame fariki dunia.”
Sabrina aliongea baada ya kumpa Leila stori fupi hiyo, huku akilia machozi na kumueleza ukweli kuwa alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ubongo,
“eeeh Mungu”
Dokta Leila alijikuta akianza kulia nay eye huku akimkombatia Sabrina, hakika ulikua ni msiba mwingine kwao, hakuwa na sababu ya kuendelea kumganda Ramsey ili mbidi achukue maamuzi magumu tu! Japo moyo wake
ulimuuma sana kukubaliana na mtokeo hayo, pia alimua kutoa mchango ili Ramsey aweze kusa firishwa kwenda india kwa ajili ya matibabu.
Wiki ili pita tayari Sabrina akiamini kuwa ame pata kiasi cha kutosha baada ya kukopa baadhi ya sehemu na kurudi Dar es salaam, alikuta hali ya Ramsey ikiwa bado ina zidi kuwa mbaya sana, aliweza kuongea kwa mbali sana.
Kway nae tayari alifika hospitali akitoa nchini Uganda baada ya kusikia Ramsey ameonekana, alifika moja kwa moja mpaka hospitalini na kumuona Ramsey ambae wakati huo alikua akimaliza kuiosma barua aliyokua imeandikwa na Marehemu Prosper,aliumia sana kusikia kuwa Prosper kajinyonga
“kway karibu sana”
“asante Ramsey, pole na kila kitu”
“nishapoa ndugu,”
Afya ya Ramsey ili dhoofu sana Kway aliligundua hilo, hakukuwa na sababu ya kuuliza mara mbili mbili kuwa Ramsey ana umwa sana, ila ili onekana ali jitahidi kuongea,
“vipi shem Joylah yupo”?
“aaah hapana,”
“hapana vipi wakati nakuona na pete ya ndoa hapo bwana Kway”
“tuliachana Ramsey, nimeoa mwana mke mwingine, ngoja nimuite umsalimie”
Kway alitoka nje na kurudi ndani akiwa na mwana mke mnene kiasi mwenye macho makubwa sana,
“huyu ndo mke wangu ana itwa Julia, ni mkongo”
“mkongo tena ana jua Kiswahili, au ndo mpaka tuanze, kuongea kilingala”?
“ndio Ramsey, ana jua Kiswahili kidogo”
“baby huyu ni frend wangu anaitwa Ramsey ni kama petit wangu(mdogo wangu), tullicheza wote na kusoma wote”
“merci, nafurahi kuku fahamu . utakua bien,”
Julia aliongea kwa rafudhi ya kikongo na Ramsey kumuomba atoke nje kidogo ili wawili hao waweze kuongea, kwa upande wa Ramsey alijua fika kuwa siku zake za kuishi zime karibia kutokana na hali yake
kuwa mbaya sana, wakati mwingine alikua akikohoa na kutoa damu, hakika alijua kifo chake kipo usoni. Ivyo nia yake ilikua ni kumuomba Kway aweze kumtunzia mali zake huku akiwa ana saidiana na familia yake,
“kway nakuomba sana, mimi nakufa muda wowote ule,. Wewe ni kama ndugu yangu, tume toka mbali sana, nina mtoto ana itwa Catherine, naomba umwangalie najua mama yake hatoweza kufanya jambo hilo peke yake, mtunze dada yangu Kway , nitunzie familia yangu”
“usiseme ivyo Ramsey, uta pona tu, niamini mimi, Mungu yupo, usisememaneno hayo”
“NO Kway,!, mimi ni mtu wa kufa, japo wame ni ficha ni ugonjwa gani naumwa, ila kupitia macho ya Loydah, najua sitopona kabisa. Nina kiwanja bunju prosper alitaka kuni tapeli, . ila naomba uhakikishe kina kua mikononi mwa
Sabrina na Catherine, kama iki tokea nikifa hata kesho, waambie jinsi gani nilivyo kua nawapenda, Kway naomba umfundishe mwanangu katika misingi ya kuipenda dini na kuwaogopa sana wana ume wana ume ni waongo sana.”
“Ramsey, usiseme maneno hayo”
Aliongea Kway huku machozi yakianza kumlenga hakika yalikua ni maneno ya kuuzunish asana , yalikua ni maneno ya kuogopesha na ya kutia simanzi,
“sikiliza sija maliza, sitaki waje kumdanganya mwanangu kama mimi nilivyo kuwa niki wadanganya wana wake wengine”
“kitu kingine Kway mw,,,”
Ramsey alishindwa kumalizia kuongea na kuanza kulalamika kichwa kina muuma sana hu ku akitupa tupa miguu na mikono kama mtu anae kata roho kushiria kua hali yake ni mbaya sana huku damu zikianza kumtoka puani..
Hali ya Ramsey ilizidi kuwa mbaya mno, na kumfanya Kway azidi kuchanganyikiwa hasa alipomuona Ramsey katulia asemi tena, moyo ulimuenda mio sana , mbio mbio alitoka na kugongana kikumbo na Loydah dada yakena Ramsey na wote kudondoka chini wazima wazima,
“kway vipi”?
“hakuna kitu”!
“hakuna kitu kivipi, mbona macho mekundu, ramsey anaendeleaje”?
“subiri kidogo”
Kway alitoka mbio mbio na baadae kurudi na daktari na kuingia nae ndani ya chumba alicholazwa Ramsey, walikua ni kama wame changanyikiwa loydah alianza kuangua kilio alivyomuona mdogo wake katulia tuli, alijua tayari mwisho wa maisha yake ume ishia hapo
Kutokan na kuwa na hali mbaya sana hapo siku za nyuma, ivyo kupona kwa Ramsey ilikua asilimia hamsini peke yake, na wala si vinginevyo, alilia machozi, madaktari wale waliwaomba watoke nje ili wao waweze kufanya kazi yao ya kujaribu kuokoa maisha yake,vile vile hata kwa madaktari hawa kua na uhakika kama mgonjwa wao huyo ataweza kuishinda hali hiyo ya umauti,
USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni