ROHO MKONONI (1) JINA: ROHO MKONONI Mwandishi: Zuberi Maruma SEHEMU YA KWANZA Familia ya afisa wa jeshi la polisi John Butu inaingia katika hatari inayomweka afisa huyo wa jeshi la polisi katika wakati mgumu wa kuipoteza familia yake,sekeseke hilo lilianza baada ya inspekta huyo kupokea simu ya mtu alojitambulisha kama ' raia mwema ' na kumpa taharifa za watu waloingiza madawa ya kulevya,kitendo cha yeye kuamua kulivalia njuga swala lile kuna amsha vita kali ambapo anapoamua kuvikimbia anagundua alishachelewa mapema sana. Ungana na mtunzi mahiri wa riwaya za kijasusi Zuberi Maruma utiririke nayo.... KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA 👈 SURA YA KWANZA Alikuwa ni kijana mrefu, mwembamba, maji ya kunde, sura yake ya upole ilipendezeshwa na tabasamu jepesi lililoundwa katika mdomo wake kila mara umtazamapo,alikuwa si muongeaji ila maneno yake machache yalikuwa kivutio masikioni mwa wamsikilizaye kw…