ROHO MKONONI (3) JINA: ROHO MKONONI Mwandishi: Zuberi Maruma SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... "Hizo namba umeshazituma kwa kpl 001?!" "Ndiyo mkuu!" "Ok!,wapigie nyumbani Kwanza ujue wanaendeleaje then uwai utanijulisha kila kitakachoendelea,mi nawasiliana na Kpl 001 kujua huyo mtu ni nani ok?!," KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA 👈 SASA ENDELEA... "Sawa mkuu" Akaitikia Butu sambamba na kukata simu,Kpl 001 kilikuwa Ni kitengo cha mawasiliano ndani ya idara ya jeshi la polisi. Inspekta John Butu baada ya kukata simu alokuwa akiongea na mkuu wake sasa akaelekea upande zilipo bodaboda akapanda akampa ishara aondoe,wakati huo huo akampigia simu mlinzi wake "Aloo Sam mpo salama?!" "Ndio mkuu kwani kuna tatizo gani!" "Kuna hatari cha kufanya funga geti kwa ndani usimfungulie mtu yoyote mi nipo njiani nakuja sawa?!" "Sawa mkuu" mlinzi alotam…