KITABU CHA SHETANI (2) Jina: KITABU CHA SHETANI Mtunzi: Aziz Hashim SEHEMU YA PILI TULIPOISHIA... Kwa kuwa alikuwa na uelewa mkubwa wa namna ya kuchezea simu na kompyuta, muda mfupi baadaye alifanikiwa kuifungua simu hiyo, juu kabisa akakutana na picha ya msichana yule aliyemtoa nishai, jambo lililomfanya awe na uhakika kwamba ni kweli ile simu ni yake na aliiangusha pale alipoikuwa anaangalia jinsi gari lake la kifahari lilivyogongwa na bodaboda. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Katika hali ambayo hakuitegemea, Edmund alijikuta macho yake yakiganda juu ya picha ya yule msichana, akawa anamtazama huku akiwa ni kama haamini alichokuwa anakiona. Mwisho alishusha pumzi ndefu na kuendelea kuishangaa simu hiyo. Kitu kingine kilichozidi kumshangaza, licha ya kufanikiwa kuifungua simu hiyo sehemu ya kwanza, kila kitu ndani ya simu kilikuwa kimefungwa kwa namba maalum za usalama, kuanzia kwenye meseji, kwenye picha, kwenye majina na kila kitu. *** Gari la ki…