KITABU CHA SHETANI (3)

Zephiline F Ezekiel
KITABU CHA SHETANI (3)
Jina: KITABU CHA SHETANI Mtunzi: Aziz Hashim SEHEMU YA TATU TULIPOISHIA... “Ok hakuna shida dada’angu,” alijibu Edmund kisha simu ikakatwa, tabasamu pana likachanua kwenye uso wake kwani licha ya ukweli kwamba msichana huyo alikuwa amemfanyia kitendo cha kumdhalilisha sana asubuhi ya siku hiyo, IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... alijikuta akimsamehe kirahisi na kutamani kumjua zaidi, akaona hiyo ndiyo nafasi yake. “Ebwana mbona mudi yako imebadilika ghafla? Tabasamu pana muda wote utafikiri umeokota pochi ya Mzungu?” Walungasa, mfanyakazi mwingine waliyekuwa akifanya kazi na Edmund alimuuliza baada ya kumuona muda wote akiwa na tabasamu pana, akaishia kucheka tu bila kueleza chanzo cha furaha yake. Saa zilizidi kuyoyoma, hatimaye muda wa chakula cha mchana uliwadia, Edmund akawa anaitazama simu yake kwa shauku kubwa akisubiri Samantha ampigie kwani walikubaliana kwenda kula chakula cha mchana pamoja. Hata hivyo, muda mfupi baaday…