MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (10)

Zephiline F Ezekiel
MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (10)
Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA KUMI TULIPOISHIA... Goooooooooooooooooooooooooooooo! Mpira ulikuwa wavuni na uwanja mzima ulikuwa ni shangwe na nderemo kwa upande wa polisi kwani tulikuwa tumeshinda Kombe hili. Pamoja na kucheza mechi moja lakini kamisaa alinitaja kuwa Golikipa Bora wa michuano hii huku akiniita afande Sam. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Nilipokea zawadi ya shilingi laki moja kiasi ambacho sikuwahi kukimiliki. Tulikabidhiwa kombe letu na zawadi ya shilingi milioni tano kutoka kwa wadhamini mbalimbali pamoja na ofa ya kulala kwenye hoteli ya Mbeya Inn ambayo ni ya nyota tano kwa siku mbili huku ukila chochote ukitakacho. Baada ya mechi ile kulikuwa na tafrija kubwa iliyoandaliwa kwenye ukumbi mkubwa wa Jeshi la Polisi pale Central Mbeya ambapo kulikuwa na burudani nyingi na watu walikuwa wanalewa sana. Watu wengi walikuwa wanadhani mimi ni Polisi lakini ukweli nilikuw…