MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (15) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA KUMI NA TANO TULIPOISHIA... Machozi yalianza kummwagika taratibu akiwa ameshikilia Tumbo lake ambalo lilikuwa likiendelea kutikiswa na kitu kilichomo ndani, machozi yalimwagika kwa wingi kwenye mashavu yake asijue ni nini hatima ya maisha yake. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Nderemo na vifijo zilikuwa zinarindima pale nje huku wageni mbalimbali wakiwa wanakula na kunywa, katika hali ya kushangaza iliyomshtua Sam ni baada ya kumuona Mama yake mzazi akiwa Miongoni mwa wageni walioko pale japo akionekana hana raha sana. Sherehe iliendelea huku wageni wakiwa wanacheza mziki na kuongea kwa nyakati tofauti kama ambavyo MC alikuwa anawaruhusu. Sam alikuwa ndani ya suti ambayo alishanunuliwa na Rafiki huku pia pete ikiwa imeshanunuliwa na kazi yake ilikuwa ni kuivisha tu kwenye vidole vya Rafiki. Ilitimu mida ya saa mbili usiku ndipo MC alipomuita sam mbele n…