Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA KUMI NA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Machozi yalianza kummwagika taratibu akiwa ameshikilia Tumbo lake ambalo lilikuwa likiendelea kutikiswa na kitu kilichomo ndani, machozi yalimwagika kwa wingi kwenye mashavu yake asijue ni nini hatima ya maisha yake.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Nderemo na vifijo zilikuwa zinarindima pale nje huku wageni mbalimbali wakiwa wanakula na kunywa, katika hali ya kushangaza iliyomshtua Sam ni baada ya kumuona Mama yake mzazi akiwa Miongoni mwa wageni walioko pale japo akionekana hana raha sana.
Sherehe iliendelea huku wageni wakiwa wanacheza mziki na kuongea kwa nyakati tofauti kama ambavyo MC alikuwa anawaruhusu.
Sam alikuwa ndani ya suti ambayo alishanunuliwa na Rafiki huku pia pete ikiwa imeshanunuliwa na kazi yake ilikuwa ni kuivisha tu kwenye vidole vya Rafiki.
Ilitimu mida ya saa mbili usiku ndipo MC alipomuita sam mbele na kumtaka amtafute mchumba wake alipokaa aje nae pale mbele.
“Sasa braza wangu wa nguvu, Mshkaji wangu wa siku Mingi AFANDE SAM…naomba uje hapa umtafute alipo Yule mpenzi wako umlete hapa mbele”
(vigelegele vilisikika baada ya Mc kutamka hivyo.)
Sam alisogea mbele na kuanza kupita taratibu kweye makundi ya watu ili akamchukue Rafiki, haikuwa kazi ngumu sana kwani watu hawakuwa wengi sana, alipokuwa anapita kuelekea pale ambapo amemuona Rafiki amekaa alishtuka suruali yake ikiwa inavutwa na mtu aliyekaa chini na kujifunika usoni.
Alipotupa macho yake kutazama ile sura alikutana na sura ya Verity ikiwa inabubujikwa machozi na kutia Huruma.
Sam alishtuka na kujikuta akitamani kumuongelesha lakini akaahirisha ghafla na kuondoka lakini aliisikia sauti ya Verity ikiita kwa sauti ya Chini …. “Sam nisikilize kwanza”
Sam hakutaka kubaki tena pale aliendelea na adhma yake ya kumtafuta Rafiki kama alivyohitajika na MC.
Aliendelea na safari yake mpaka akafika pale alipoketi Rafikia AKAMCHUKUA na kwenda nae mbele huku kamshika mkono.
Walipofika mbele huku wakisindikizwa na makofi na vifijo walisimama na MC hakuwaruhusu kukaa…
SASA BRAZA SAM NAOMBA UFANYE KILICHOTULETA HAPA…
Sam aliingiza mkono mfukoni akitafuta pete lakini akawa haioni alijipapasa sana kila kona lakini haikuonekana.
Watu wote walikuwa wamemkazia macho wakiwa wanamuonea huruma huku wamepigwa na butwaa kwa kile ambacho kinatokea
RPC na mkewe walikuwa wamekaza macho yao mbele kule kwa Sam huku RPC akidhani kuwa ni Janja ya Sam ili asimuoe binti yake.
Hasira zilikuwa zimemkaba vilivyo na alishaanza kuamka pale alipokaa akitaka kumfwata Sam kule mbele ili akamfundishe adabu.
………………………….
Nisha akiwa ana hasira na fedheha ikiwa imemjaa machoni na moyoni alianza kujivuta akielekea nje ya Geti la Nyumba ya RPC.
Alikuwa anaumia moyoni kwa fedheha aliyofanyiwa tena akiwa ugenini, alijisikia kuaibishwa na kudharauliwa sana.
Alijiwazia moyoni mwake …
“Hivi mimi nina kasoro gani na nimekosa nini”
“Hivi huyu Sam ana nini haswa cha kunifanya mimi nimtetemekee hadi nidhalilishwe kiasi hiki”
“Kama kile kidada kilichokuwa pale ndio kinamtaka Sam hakiniwezi kwanza hakinizidi kwa lolote, nitawakomesha”
Nisha aliona Bajaji ikipita akaisimamisha na kupanda, “Nikupeleke wapi DADA?”
“Nipeleke sehemu yenye baa iliyotulia ambayo haina makelele”
“Poa”
Bajaji ilichanja njia na kuingia kwenye hoteli moja yenye ukumbi nje ikiwa imeandikwa Tunduma INN…
Ilikuwa ni Hoteli nzuri ambayo ilikuwa nje ya mji wa Mbeya kidogo huku kukiwa na ukumbi wenye mandhari nzuri huku watu wachache wanaoonekana wana maisha yao mazuri wakiwa wamekaa na kula na kunywa vitu vya gharama
Vinywaji hapa vilikuwa mezani ni kama Heinken, Amarula, St Anne, Savanna, Windhoek na vingine, Miguu ya Mbuzi na mikausho ya Kuku ni moja ya vitu vilivyokuwa vinatafunwa hapa kwa wingi.
Kwa hasira alizokuwa nazo Nisha aliamua kufanya kitu ambacho alikuwa hajawahi kukifanya katika maisha yake…kunywa pombe.
Hata pombe gani aanza nayo alikuwa hajui kwani hana uzoefu, mziki wa taratibu uliokuwa unapiga ulikuwa ni AMARULA ulioimbwa na mzambia Roberto.
Hapo hapo Nisha aliamua kuagiza AMARULA, “niletee amarula dada”
“naomba elfu ishirini”
Nisha alitoa kiasi hicho cha fedha na kuletewa kinywaji alichoagiza, kilivyoletwa alikaribishwa na kukibugia kwa fujo na ndani ya dakika tatu kilikuwa kimeisha….
“Psiii, psiii”
Alimuita mhudumu aliyemhudumia
“Niongeze nyingine”
“Naomba hela”
Mhudumu alipewa hela lakini alikuwa anawaza kuwa Yule dada ataweza kumudu hizo pombe anazokunywa?
Alivyofika counta alimuita meneja na kumueleza kuhusu mteja anayebugia amarula kama soda…
Meneja alionnyeshwa alipo Nisha na kuahidi kuwa atakuwa anamuangalia mwenendo wake kwani alionekana ana stress.
Amarula ya pili ilitua Mezani kwa NISHA na kufunguliwa, alivyotaka kuipeleka mdomoni alianza kujisikia mikono yake haina nguvu za kutosha, na kichwa kimekuwa kizito.
Yule mhudumu alilitambua hilo akamfwata na kumuuliza…
“Dada nikuitie mtu wa Jikoni upate hata supu, hivyo vitu vinaendana na Supu”
“Poa mwambie alete mchemsho wa Kuku”
Mtu wa Jikoni alikuja na sinia lenye mchemsho wa kuku na ndizi akaviweka mezani lakini Nisha alikuwa ameuchapa usingizi.
“Dada, Dada amka supu yako hii hapa”
Nisha aliamka na kuifakamia Supu huku akivutana na minofu ya kuku, alikuwa na njaa sana ukichanganya na Pombe alizokunywa ndio zilimkwangua Tumbo kabisa.
Alivyomaliza Supu yake alijisikia nafuu kidogo, Yule mhudumu alikuja tena akamwambia,
“nikuletee maji dada? , ni vizuri ukipata maji ya baridi”
“Sawa niletee”
Mhudumu alienda akarudi na chupa kubwa ya maji yaliyoandikwa Udzungwa na kummiminia kwenye glass na kumkaribisha.
“Dada maji yako haya hapa kunywa”
“asante sana”
Nisha alikunywa yale maji taratibu huku akirembua macho, Yule mhudumu alikaa palepale mezani na kujaribu kuongea stori mbili tatu na Nisha ambaye alikuwa anamjibu kilevi na kivivu.
Yule mhudumu alifanya vile kwani alitamani kujua sababu ya unywaji ule wa Pombe kwa mdada mzuri kama Nisha.
“Dada niko hapa kama utataka huduma yeyote usihangaike kuniita”
“Usijali”
“Kwani uko mwenyewe au kuna mgeni unamsubiri”
Nisha alinyanyua sura yake na kumtazama Yule mhudumu akitamani amtukane lakini alivvyomtazama machoni alikutana na sura ya dada mrembo ambaye alionekana ni mstaarabu huku akiwa ana tabasamu lisilokuwa na sababu ya kutukanwa.
“Samahani mimi naitwa Esther”
“Mimi naitwa Nisha”
“Karibu sana dada hapa kazini kwetu, ni sehemu iliyotulia kwa watu na heshima zenu kama wewe”
“Asante”
“VIP nikumiminie kinywaji chako kwenye Glass?”
“Sawa nawewe njoo na Glass tujumuike”
“Usijali, mimi niko kazini ila nitakusindikiza kidogo kidogo”
Yule mhudumu alirudi akakaa na Nisha akajimiminia kinywaji kidogo, lengo lake ilikuwa ni kumchangamsha Nisha na kumzuia asinywe ile chupa nyingine yote.
Alifanya haya yote akiwa hataki yamkute mwanamke mwenzake kama yeye yalivyomtokea miaka ya Nyuma na kumharibia kabisa ndoto zake.
Walianza kunywa taratibu huku wakipiga story mbili tatu, na kujikuta wamezoeana ndani ya muda mfupi.
“psiii…psiiii”
Mhudumu aliitwa na wateja waliokuwa wamekaa meza ya pembeni.
“Tuletee AMARULA KUBWA”
Wateja wale walitoa noti ya Dola mia na kumpa mhudumu ambaye aliondoka nayo kwani hoteli ile ilikuwa inapokea hata fedha za kigeni
Alivyorudi na chenji aliambiwa abaki nayo na wanaweza kujiagiza na wao kinywaji wanachotaka.
“Alafu Dada tunaomba tujiunge na kampani yenu”
Yule mhudumu alikuwa anashindwa cha kusema kuwa akatae ama akubali kwani tayari mkononi alikuwa amebaki na chenchi ya watu kama dola elfu themanini hivi ambayo ni sawa na shilingi laki moja na elfu sitini za kitanzania.
Mimi nimekupenda wewe na mwenzangu amempenda Yule mrembo uliyekaa nae, mkikubali kampani yetu mtafurahi mpaka jino la mwisho.
……………………………….
Hasira zilikuwa zimemkaba RPC na alishaamka kwenye kiti anaelekea kule mbele aliko Sam ambaye aliamini anazuga kwa kutoiona pete ili asimuoe binti yake.
RPC likuwa ametia mkono mfukoni ambapo alikuwa ameweka bunduki yake aina ya Pistol. Verity kule alikokaa aliliona tukio na alishaisoma akili ya Baba yake na kile anachoenda kufanya. Hakusita ilibidi aamke kwenye kiti.
Sam alikuwa anamtazama RPC Kwa woga kwani alijua kuna kitu sio kizuri kinaweza kikatokea, alitamani kukimbia lakini hakuyaamini maamuzi yake, alikuwa anajiuliza ni wapi ile pete imeenda wakati aliiweka mwenyewe mfukoni.
Verity alikuwa anakaza mwendo na tayari alikuwa amekaribia pale alipo Sam na Rafiki!
RPC alishangaa sana kumuona binti yake Verity akiwa anaelekea kule mbele kwani hakujua kuwa yuko pale ukumbini.
Verity alipofika pale mbele alidaka maiki kutoka kwa MC na kuanza kuongea…
“Kwa dada yangu kipenzi Rafiki na Shemeji yangu Sam”
“Leo nimeamua kujitolea pete hii ili umvishe dada yangu ninayempenda na ninawaombea maisha mema hadi siku mje mfunge ndoa yenye furaha.”
“Ndugu na wageni waalikwa; Poleni kwa sapraiz ambayo tumeamua kuwafanyia mimi na shemeji yangu kuwafanya muhisi kwamba tumepoteza pete…najua hata wewe dada yangu umeshtuka…usijali SAM ni wako tu”
Sam alikuwa ameduwaa kwa maneno ya Verity, hakushiriki mpango wowote na Verity lakini kile kilichotokea alihusishwa, kilichompa amani na furaha ni baada ya tatizo kupata tiba.
Hakutaka kuwaza zaidi kuwa ile pete Verity ameitoa wapi, alichotaka yeye ni amvalishe Rafiki Pete ili aondokane na lile tatizo lililokuwa mbele yake.
Wkati anataka kumvisha Rafiki pete alisikia mlio wa meseji kwenye simu yake akaifungua na kuisoma ambapo alikutana na ujumbe kutoka kwa Nisha!
“Sam nakupenda sana, nahisi huko uliko unataka kufanya maamuzi ambayo hujayaridhia kwa moyo mmoja, tafadhali njoo nina hamu nawewe, nimelewa sana na wanaume wananitaka kwa lazima, tafadhali njoo sitaki kulala na mwanaume mwingine, usipokuja watanichukua!
Sam alikuwa kama anaota, ukweli ni kuwa alikuwa anampenda sana Rafiki lakini mazingira ya kulazimishwa amuoe hakuyataka, lakini zaidi ya hilo alikuwa anavutiwa sana na Nisha na siku hiyo walipanga wawe wote!
Kitu kimoja kilimpa moyo … kumvisha mwanamke pete sio kumuoa, bado nina nafasi ya kutengua maamuzi.
Haraka haraka alipiga magoti chini na kutoa pete kwenye kibox chake na kukishika kidole cha Rafiki na taratibu huku akiwa amepiga magoti akaaanza kuingiza pete kwenye kidole huku Rafiki akidondokwa na machozi.
Kwa taratibu huku akiwa anamuangalia Rafiki machoni wakisindikizwa na shangwe na vigelegele pete ilipenya mpaka ikakaa sawia kwenye kidole cha Rafiki ambaye alikuwa anabubujikwa na machozi ya furaha.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)