MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (20) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA ISHIRINI TULIPOISHIA... Dada alikata simu kisha nikaisikia simu ya shemeji ikiita huko chumbani nikajua kuwa ni dada atakuwa ameamua kumpigia mume wake. Baada ya masaa kama matatu hivi dada alirudi kisha akaingia chumbani kwa mme wake ambapo niliwasikia wakiongea taratibu kisha mimi nikawa naendelea na kazi zangu kama kawaida. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Baada ya kama wiki nzima ya kutokumuona shemeji akienda kazini niligundua kuwa kampuni ambayo alikuwa anafanya kazi shemeji kama mhasibu illikuwa imefungiwa leseni ya kazi kwasababu ya kusababisha ajali na kudaiwa kukwepa kodi. Shemeji yangu alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya usafirishaji wa mizigo kama mafuta na bidhaa zingine lakini pia na ilikuwa na mabasi ya abiria. Habari za chini ya kapeti ni kwamba mmiliki wa kampuni alikosana kisiasa na viongozi wa serikali baada ya kuonekana anaukarib…