MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (4) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA NNE TULIPOISHIA... Nilianza kupiga hatua kwenda pembeni ya barabara nitafute sehem yenye kivuli nikae lakini kila nilipokuwa nakata hatua nilikuwa najisikia unyonge sana, miguu ilianza kuwa mizito huku nikisikilizia maumivu ya lile kofi nlilopigwa na Yule konda. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Jua lilikuwa kali sana na tayari nilikuwa nasikia kiu mno, sehemu hii ilikuwa ni vichaka tupu na hakuna gari iliyokuwa inasimama kwani hakukuwa na kituo wala nyumba za watu. Nilipiga macho mbele nyuma na pembeni nikashuhudia vichaka vya miti mikavu kuonyesha kuwa hii sehemu hakukuwa na makazi ya watu, sikuona hata dalili ya mtu kupita isipokuwa magari yaliyokuwa yanapita kwa kasi sana. Katika hali ambayo sikuitegemea nilishuhudia majimaji yakishuka kwenye mashavu yangu nikaaanza kuyafuta, kumbe yalikuwa ni machozi. Nilikuwa najihisi hali ya upweke sana, nilijiona…