MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (5)

Zephiline F Ezekiel
MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (5)
Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA TANO TULIPOISHIA... Abeid alikuwa ni mjanja sana maana kwa jinsi tulivyofika pale wizarani na maswali tuliyoulizwa na wale walinzi basi ningekuwa peke yangu ningesharudi kwa kuogopa lakini tofauti ni kwamba Abeid kila alipokuwa anajibiwa vibaya yeye alikuwa anatabasamu na kuonyesha kutoshtuka. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Ilifika hatua mpaka wale walinzi wakawa wanacheka kwa jinsi alivyokuwa anawajibu kistaarabu lakini na utani ndani yake. “Haya semeni mnamtafuta nani” “Sisi tunamtafuta Mheshimiwa mmoja anaishia jina lake na Steven.” “Huyu mwanasheria wa Jeshi la Polisi?” “Ndio huyo huyo” “Basi nyinyi hamna ahadi nae kama mngekuwa mna ahadi ya kukutana nae mngeshajua kuwa hayuko tena hapa” “Unasemaje braza?” Nilijikuta nikiropoka baada ya kusikia kuwa hayuko tena pale, “Hebu tulia wewe, mbona una kiherehere, na nyie ndio mmemponza mheshimiwa wa watu, ana…