MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (5)

0

SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
Abeid alikuwa ni mjanja sana maana kwa jinsi tulivyofika pale wizarani na maswali tuliyoulizwa na wale walinzi basi ningekuwa peke yangu ningesharudi kwa kuogopa lakini tofauti ni kwamba Abeid kila alipokuwa anajibiwa vibaya yeye alikuwa anatabasamu na kuonyesha kutoshtuka.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Ilifika hatua mpaka wale walinzi wakawa wanacheka kwa jinsi alivyokuwa anawajibu kistaarabu lakini na utani ndani yake.
“Haya semeni mnamtafuta nani”
“Sisi tunamtafuta Mheshimiwa mmoja anaishia jina lake na Steven.”
“Huyu mwanasheria wa Jeshi la Polisi?”
“Ndio huyo huyo”
“Basi nyinyi hamna ahadi nae kama mngekuwa mna ahadi ya kukutana nae mngeshajua kuwa hayuko tena hapa”
“Unasemaje braza?”
Nilijikuta nikiropoka baada ya kusikia kuwa hayuko tena pale,

“Hebu tulia wewe, mbona una kiherehere, na nyie ndio mmemponza mheshimiwa wa watu, anawasaidia alafu mnasema mmempa Rushwa.”
Nilimuona abeid akinipa ishara ya kunyamaza kisha akamfwata Mlinzi mmoja kwa karibu kisha wakaanza kuongea kwa sauti ya chini.
Waliongea kwa takribani dakika mbili kisha akawaaga na kunionyesha ishara ya kuondoka nami nikamfwata.
Nilikuwa na shauku ya kujua kuwa waliongea nini lakini Abeid alikuwa kimya tu, nilivumilia kwa mda lakini mwishowe nikaamua kumuuliza, “Kaka vipi wamekwambiaje?”
“Subiri kidogo”
Tuliendelea kutembea kwa dakika kadhaa mpaka nilipoona bango limeandikwa IFM (INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT)

Tuliingia pale tukaelekea moja kwa moja mpaka kwenye canteen ya pale tukachukua nafasi tukakaa,
“unajua hapa posta ukiingia hoteli zake unakung’uta waleti yako kabisa, hizi za wanafunzi at least zina bei nafuu”
Tulikula wali samaki na Juice ya matunda kisha maongezi yakaendelea,
“Wale jamaa wanasema Mheshimiwa ameondolewa kwenye kitengo na amehamishiwa Mbeya bila kutajiwa kazi anayoenda kufanya”
“HAAH KWANINI SASA”
“inasemekana alikuwa anakula Rushwa sana ila kwa mujibu wa wale jamaa ni kwamba alikuwa hali Rushwa ila alikuwa na moyo wa kusaidia watu”

Kusema ukweli nilinyong’onyea sana, nilishindwa kabisa kumalizia ile juice japokuwa chakula kilikuwa kimeshaisha.
Nilijikuta nikijihisi mimi ni mtu wa Mikosi, matatizo yalikuwa yameniandama sana.
“Usijali Sam, hiyo sio sababu ya ndoto zako kutotimia, wewe tuliza akili alafu tutajua cha kufanya”
Wakati tuko pale nilikuwa nashuhudia wanafunzi wa kile chuo wakipita wakiingia na kutoka, kulikuwa na wadada wazuri sijawahi kuona, walikuwa wamevaa nguo za mitego kiasi kwamba nilihisi mapigo ya Moyo yakienda mbio mno.

Jambo moja liliuvaa moyo wangu na kuniambia kuwa mimi sikuwa hadhi yao hivyo ntakula tu kwa macho.
Katika hali ambayo sikuitarajia nilimuona Abeid akiamka na kukumbatiana na dada mmoja mfupi mweusi ambaye alikuwa na shepu moja matata sana.
Walisalimiana kwa bashasha kubwa kisha nikawasikia wakiongea kikabila cha kwetu, hapo ndipo niliposhtuka vilivyo.
“Wewe si niliambiwa umekuwa askari polisi hapa unafanya nini”
“Ah Abeid si unanijua lakini, siwezi kuwa askari wa cheo cha chini kila siku, hapa nimekuja kuongeza elimu na ninachuukua degree ya Banking and Accounting”
“Dah Hongera sana”
“Asante, mbona huyo hapo kama namfaham”
“Unamjua sana, wakati nyinyi mnamaliza darasa la saba alikuja akiwa anakaa pale kwa mwalim Kahema”

“Haaa huyu si ndio Yule alikuwa Golkipa wa shule”
“Ndio huyo huyo”
Nilishtuka kusikia kuwa Yule dada ananifaham kwani sikuwa namkumbuka hata kidogo, alivyotaja swala la ugolkipa alinishtua zaidi kwani ukweli mimi nilikuwa Golkipa maarufu mpaka nilikuwa nakodishwa.
Alinifwata Yule dada akanisimamisha na kunikumbatia huku akionyesha tabasam mwanana.
“Vip unasoma hapa Sam?”
“Hapana nimekuja tu”
“Subiri ntakwambia ishu yake” (Abeid alidakia)
Yule dada alikaa akajitambuliasha kuwa anaitwa Vicky na Baba yake alikuwa Daktari wa shule moja ya Misheni kule kijijini. Alivyosema hivyo nikaanza kumkumbuka kuwa alikuwaga dada mkuu pale shuleni.
…………………………….
“Bwana Z. Steven amehamishiwa Mbeya ila inasemekana atakula cheo cha juu hivyo kama ni msaada bado anaweza akatoa, kama ameelekezwa kwake amfwate tu”

(Aliongea Vicky)
“Sam inabidi uende Mbeya ukaonane nae, kama ni nauli tutakuchangia”
`…………………….
Nilikuwa na shilingi elfu thelasini mfukoni ikiwa ni Nauli amenipa Abed niende mbeya, nikiwa pale Ubungo akapita jamaa mmoja anauza simu anadai anauza shilingi elfu ishirini.
Niliiangalia ile simu nikaipenda kisha nikamwambia aiwashe, wakati wanaiwasha ile simu alipita jamaa mmoja kwa nyuma akaniambia…
“Wewe dogo mbona unanikanyaga”
“samahani braza ni bahati mbaya”
“Usirudie tena”

Wakati nageuka kumuangalia Yule jamaa wa simu nikagundua kuwa hakuwepo, sikujali sana nikaelekea kwenye kituo nilichoambiwa nikate tiketi.
Niliingia ndani nikaelekezwa kiwango cha nauli kuwa ni elfu ishirini na tano nikawa najipapasa mfukoni nilipe huku Yule Konda akiendelea kuandika tiketi.
Nilijikuta nikitetemeka mwili mzima kwani mfukoni hakukuwa na hata senti tano….
Kitendo cha kuibiwa nauli pale Ubungo ndio kilinifanya nijue kuwa kweli nimeingia mjini, story za watu kuibiwa pale Dar es Salaam nilikuwa nazisikia tu lakini leo zimenikuta.
Wakati wote huo Yule Konda alikuwa ameshamaliza kuniandikia tiketi na ananinyooshea kunipa.
“Shika tiketi yako”

Niliipokea tiketi lakini sikuwa na cha kurudisha, wakati konda amenyoosha mkono wake akitaka nimpe hela nilianza tena kujipapasa, nilijipapasa ila nilikuwa nazuga tu, nilijua kabisa kuwa mfukoni hakuna kitu.
Chaajabu ni kwamba wakati najipapasa nikashika kitu kama karatasi nikahamaki na kukitoa, nilivyokiangalia nikakuta ni noti ya shilingi elfu mbili.
“WE dogo unatoa hela au nini, mbona hueleweki”
“Broo nina hii tu, nyingine imeibiwa”
“Mjinga nini, toka hapa ofisini, tokaaaa”
Alinisukuma kama mwizi kidogo nidondoke ila nikajikaza.
Nikiwa pale nje ya ofisi nilijikuta machozi yakitaka kunitoka lakini nikajisemea moyoni, safari hii silii nakomaa kiume.

Nilijikaza kutokulia na kweli sikulia, nikawa natembea tembea pale kituoni.
Wakati naekekea lango la kutokea magari nikaona basi moja kubwa limeandikwa Happy Nation linatoka huku baadhi ya wapiga debe wakisema “wale wa mbeya, Iringa zama ndani gari ya kuondoka hiyo”
Sijui yale maamuzi niliyatoa wapi, nilijikuta nakanyaga ngazi za basi na kutumbukia ndani.
“Gari nyeupe hiyo tafuta siti ukae.”
Kweli gari haikuwa na watu wengi sana hivyo nikajichagulia siti nikakaa,
Gari ilianza kuondoka kwa mwendo wa taratibu kwani kulikuwa na foleni kuanzia ubungo mpaka tunafika Mbezi mwisho.
Wakati wote huo bado nilikuwa sijadaiwa nauli na kote huko njiani walikuwa wanaendelea kupakiza abiria.

Tulipofika kibaha siti zote zilikuwa zimejaa na hivyo hakukuwa na abiria wengine ambao wangepata siti, Konda alianza kuzunguka kuuliza kila abiria anaishia wapi, waliokuwa wanaishia sijui Chalinze au Morogoro waliambiwa waachie siti kwa wanaokwenda mbali
”Dogo unaishia wapi”
“Mbe..mbe..ya broo”
“Sasa unatetemeka nini, jiamini dogo kwani si umepanda kwa nuli yako”
Moyoni nikataka kumwambia unajua hapa nina elfu mbili tu.
……………………
Tayari tulikuwa tumeipita Mlandizi, tunakatisha kwenye Bonde hili la mto Ruvu na hatimaye tukavuka daraja ndipo nikamuona Konda akianza kupita na chati yake anakagua tiketi na kupokea hela kwa wale ambao hawajalipa.
Alisogea na hatimaye tukiwa tunaikaribia Chalinze akawa amefika kwangu.
“Dogo naomba tiketi”
“Sina”
“Haya leta elfu ishirini ”
Nilianza tena kujipapasa kwa kuzugia mwishowe nikaibuka na shilingi elfu mbili.
“Hiyo ni noti mpya ya shilingi elfu ishirini au”
Bado niliendelea kuinyoosha ile hela ili aipokee huku mkono ukitetemeka.

“We dogo kwani unaishia wapi”
“Naenda Mbeya”
“sasa hiyo shilingi elfu mbili yanini mdogo wangu”
“Sina nyingine nimeibiwa nauli kaka”
“Haya ilete”
Nilimpa ile shilingi elfu mbili nikajua nimepona tena kwa mara nyingine
“Sasa kama umeibiwa nauli tukifika Chalinze tutakusaidia kukushusha kwa polisi ili washughulikie swala lako la kuibiwa, sawa dogo”
Nilishtuka lakini nikajibu “sawa broo”
Safari iliendelea na ndani ya dakika kumi na tano tukawa tuko Chalinze, gari lilisimama Yule konda akaja na kuniambia

“Begi lako liko wapi”
“Hili hapa kaka”
“Haya shuka nalo tukaripoti kwa hao askari hapo nje”
Nilifwatana nae mpaka tukafika chini, tulipofika alianza kusalimiana na wale askari ambao waliongea na kuchekeana.
Gari lilipomaliza kupima mizani akawaambia wale askari.
“Nawaachia kijana wenu huyo anataka aende Mbeya kwa shilingi elfu mbili hebu msikilizeni vizuri.”
“Njoo hapa wewe chokoraa”

Roho iliniuma kuitwa chokoraa lakini sikuwa na namna ikabidi nimfwate Yule askari huku natetemeka.
Maisha yangu yote japo nilikuwa naenda kuutafuta uaskari ila nilikuwa ninawaogopa sana.
“Dogo wewe ni mwizi eenh”
“Hapana Baba”
“Nani baba yako hapa, sisi hatuwezi kuwa na mtoto mwenye bichwa kubwa hivi”
Nilisikia kitu kama chuma kimeshuka kichwani kwangu kumbe ni Konzi la Yule askari. Niliumia kiasi kwamba nilianza kuona vitu kama nyota nyota.
“mbona mnapenda kutupa kazi ambazo hazina msingi nyie, hebu chuchumaa chini”
Nilichuchumaa huku machozi yakinidondoka.

“Unapanda kwenye gari huna nauli ulitaka ukawaibie watu kwenye gari sio”
“Hapana afande”
“Unafikiri hatuwajui nyie, mnaingia kwenye gari ili muibie watu wakati hamna mpango wa kusafiri”
“Hapana afande nimeib..b…biwa nauli”
“Nani akuibie wewe, wewe ndio mwizi alafu uibiwe”
“Mungu anajua afande nimeibiwa kweli”
“Kama Mungu anajua mimi sijui. Twende huku Mbweha wewe”
Nilimfwata nyuma nyuma mpaka kwenye ile ofisi ya Mizani,
“Dulla vipi hapo mbona ofisi yenu chafu hivyo”
“Hahahahaaaa ukiona hivyo ujue inafanyiwa kazi, vipi karibu”
“Ah napita tu ila nimewaletea huyu jamaa awasaidie kuisafisha apige deki vizuri”
“Haya asante kwa kutujali”

Nilikabidhiwa fagio, dekio na ndoo kisha nikaambiwa nihakikishe panang’aa.
Safari hii sikuweza kuvumilia, nilianza kufagia huku nalia, nikamaliza kisha nikachota maji kwenye bomba lililokuwa nje ya zile ofisi nikaanza kudeki huku nalia pia.
Mpaka namaliza nilikuwa nimelia mno, wale jamaa wakaniambia nikamwambie Yule askari kuwa nimemaliza, kisha nikaenda.
“Sasa ole wako nifike hapajang’aa”
Tuliongozana mpaka pale ofisini kisha nikaanza kushushiwa makofi na mateke.
“Jinga sana wewe, hapo umesafisha au umechafua”
“Haya kunja ngumii uanza kupiga Pushap hapo”
“chini….juu….chiniiiiii…..juuuuu, nikipiga kofi unashuka, nikipiga unapanda”
Zoezi la pushap liliendelea kwa nusu saa nzima hadi nikajisikia kama nakufa, nilianza kusikia harufu ya damu kifuani, nililia mpaka machozi yakakauka lakini hakuna aliyenionea huruma.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)