MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (56) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA HAMSINI NA SITA TULIPOISHIA... Kwa fedha ambazo alikuwa anaingiza na kuziweka kwenye Akaunti ya Glory alimruhusu mdogo wake kufanya mradi wowote ambao angeona unafaa. Glory alikubaliana na kaka yake lakini alimsihi kuwa asuburi kidogo amalizie masomo yake huku akiendelea kutafakari ninini cha kufanya. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Siku zilizidi kwenda ambapo Sam alianza kuchoka kutumikia mabwana wawili yaani serikali pamoja na washirika wengine ambao walikuwa wanafanya biashara haram. Kuna wakati alikuwa anaombwa kutoa ulinzi kwa washirika wake lakini badala yake aliwachoma na kuwakamatisha kwa askari wengine. Hali iliendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu ikabidi wale jamaa zake waghairishe kuutumia mkoa wa tabora kwenye mambo yao. ……………………………… Kutokana na vituko vya Gwakisa Verity aliamua kuhamia Dar es salaam kwani hata hivyo aliona ni sehemu ambayo ita…