MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (56)

0

SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
TULIPOISHIA...
Kwa fedha ambazo alikuwa anaingiza na kuziweka kwenye Akaunti ya Glory alimruhusu mdogo wake kufanya mradi wowote ambao angeona unafaa. Glory alikubaliana na kaka yake lakini alimsihi kuwa asuburi kidogo amalizie masomo yake huku akiendelea kutafakari ninini cha kufanya.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Siku zilizidi kwenda ambapo Sam alianza kuchoka kutumikia mabwana wawili yaani serikali pamoja na washirika wengine ambao walikuwa wanafanya biashara haram.
Kuna wakati alikuwa anaombwa kutoa ulinzi kwa washirika wake lakini badala yake aliwachoma na kuwakamatisha kwa askari wengine.
Hali iliendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu ikabidi wale jamaa zake waghairishe kuutumia mkoa wa tabora kwenye mambo yao.
………………………………
Kutokana na vituko vya Gwakisa Verity aliamua kuhamia Dar es salaam kwani hata hivyo aliona ni sehemu ambayo itamfanya aendeleze miradi yake kwakuwa mtaji wake pia ulikuwa umekua sana.
Kitendo cha kuhama kilimfanya Gwakisa azidishe chuki kwa Sam akiamini yeye ndie amemshawishi japo ukweli haukuwa hivyo.
Kuhama kwa Verity kunamfanya Rafiki nae aanze taratibu za kuhamia Dar es Salaam kwani aliamini ni sehemu rahisi kwaa yeye kukutana na mme wake ambaye mara kwa mara alikuwa anaenda Dar es Salaam kikazi huku Mbeya kukionekena kuwa mbali zaidi.
Baada ya muda kidogo alifanikiwa kuhamia kweli Dar es Salaam akawa anakaa Mtoni Kijichi karibu kabisa na ufukweni ambapo Sam aliikuwa amenunua nyumba ya kisasa sana maeneo hayo.
Verity alikuwa amepanua sana biashara zake na kuanzisha mradi mwingine wa kuuza asali ambayo alikuwa anaichukulia mikoa ya Tabora, Shinyanga na Singida.
Safari zake za mara kwa mara kwenye mkoa wa Tabora zinamkutanisha tena na Sam ambapo mara nyingi akiwa huko anakuwa na Sam baada ya kumaliza mizunguko yake ambapo hukaa maeneo ya starehe hadi usiku wa manane na kisha kila mtu kwenda kulala kivyake.

Siku moja ambayo ilikuwa ni usiku wa saa tisa kasoro Sam akiwa ametoka club na Verity alimpeleka kwenye hoteli ambayo huwa analala anapokuwa Tabora kwenye biashara zake.

Baada ya kumuacha Verity pale hotelini aliondoka akiwa na mlinzi wake mmoja ambaye ndie alikuwa dereva wake pia mpaka alipofika nyumbani na kisha kumruhusu Yule dereva akalale na Gari lile kama kutakuwa na lolote atampigia simu.
Yule mlinzi aligeuza gari lakini kabla hajaondoka maeneo yale gari ilipigwa mkono na kuamua kuisimamisha,

Sam akiwa hajaingia ndani alisikia makelele akaamua kutoka lakini alipotoa mwili wake na kukuta dereva wake akichezea kipigo alihisi kitu cha moto kikipita kwenye upande wa kushoto wa kifuani na kingine katikati ya tumbo hapo hapo akaanguka chini.

Alipoangalia vizuri mbele akakuta mtu amemnyooshea bunduki akiwa amelala palepale chini lakini hakumtambua Yule mtu ni nani kwani uso wake ulikuwa umezibwa kwa maski.

Yule dereva alishtuka baada ya wale watu kupotea na kumuacha bosi wake akitokwa damu nyingi, hapo hapo alipiga simu polisi ambapo gari za Polisi zilikuja haraka na kumbebeba RPC sam hadi hospitali huku akiwa hana dalili ya uhai.

Kwa mbali taswira ya Sam ilikuwa inakusanya kumbukumbu za maisha yake ya nyuma lakini katika yote aliyokumbuka ni Siku Mama yake Aliposhikwa Tako mbele yake na hapo akaamua kutafuta maisha mazuri ili amuokoe mama yake kutoka kwenye kazi za kiuzalilishaji.
Ni wakati huu pia alikuwa anamuona mama yake amevaa mavazi mweupe peer na ya kung’aa anataka kumpokea lakini kwa onyo kuwa “tubu kwanza dhambi zako ndio uje huku nilipo”

Neno la mwisho ambalo madaktari walimsikia Sam akilisema ni “Mungu wangu naomba unipokee” na baada ya kusema hivyo akaaga dunia.

Asanteni sana wote mliokuwa nami kwenye simulizi hii mpaka hapa ilipofikia…. Kama unataka kujua ni kitu gani kilitokea baada ya RPC SAM kufariki ungana nami katika Season Nyingine inayofwata kwa Jina la “MY DAD’S EMPIRE”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
MWISHO

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)