MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (6) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA SITA TULIPOISHIA... “chini….juu….chiniiiiii…..juuuuu, nikipiga kofi unashuka, nikipiga unapanda” Zoezi la pushap liliendelea kwa nusu saa nzima hadi nikajisikia kama nakufa, nilianza kusikia harufu ya damu kifuani, nililia mpaka machozi yakakauka lakini hakuna aliyenionea huruma. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Mbaya zaidi wakati waliponiona nayamudu yale mazoezi vizuri wakasema eti mimi ni sugu nimeshazoea matukio. “Niliwaambia huyu ni kibaka, huoni anavyoyamudu haya mazoezi, lakini na ukibaka wako leo utatapika damu” “Afande samahani, mbona kama huyu kijana namfahamu?” “Acha huruma zako wewe huwezi kumjua huyu labda kama amewahi kukuibia” “We mtoto mbona kama sura yako sio ngeni machoni kwangu” “Ha..ha…hata mi…mi nakufaham da..da, nisaidie naumia” “Tulionana hapa hapa dada nilikuja na Konda wa Semitrela Juzi” “Ahaaaaa, dulla nyie hamumkumbuki huyu kijana” …