Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“chini….juu….chiniiiiii…..juuuuu, nikipiga kofi unashuka, nikipiga unapanda”
Zoezi la pushap liliendelea kwa nusu saa nzima hadi nikajisikia kama nakufa, nilianza kusikia harufu ya damu kifuani, nililia mpaka machozi yakakauka lakini hakuna aliyenionea huruma.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Mbaya zaidi wakati waliponiona nayamudu yale mazoezi vizuri wakasema eti mimi ni sugu nimeshazoea matukio.
“Niliwaambia huyu ni kibaka, huoni anavyoyamudu haya mazoezi, lakini na ukibaka wako leo utatapika damu”
“Afande samahani, mbona kama huyu kijana namfahamu?”
“Acha huruma zako wewe huwezi kumjua huyu labda kama amewahi kukuibia”
“We mtoto mbona kama sura yako sio ngeni machoni kwangu”
“Ha..ha…hata mi…mi nakufaham da..da, nisaidie naumia”
“Tulionana hapa hapa dada nilikuja na Konda wa Semitrela Juzi”
“Ahaaaaa, dulla nyie hamumkumbuki huyu kijana”
“Haaa ndio huyu kwani, mbona ana majanga hivi, kimekupata nini?”
“Haya baki na wenyeji wako hapa” (Yule askari alisema kisha akaondoka zake)
Wale jamaa walinihoji nikawaelezea kisa kizima mpaka Yule dada nikamuona analia machozi kabisa.
“Usijali dogo. Utafika mbeya leo, lakini mbona umechafuka sana, Nifwate”
Tuliondoka na Yule dada hadi kwenye duka la nguo akaninunulia traki suit ya blue na sendo kisha akaniambia nibadilishe nivae zile
Nilipobadilisha nguo alininunulia chipsi mayai na soda kisha akaniambia nipumzike hapo atakuja baadae.
Ilikuwa ni baa flani hivi ambapo nilikaa huku naangalia tv, mwili ulikuwa umechoka sana mpaka nikajisikia kama homa, viungo vilikuwa vimelegea vibaya sana, moyoni nilijiuliza kwanini nina majanga hivi?
Baada ya lisaa ,limoja Yule dada alikuja akaniambia nimfwate.
Tulienda mpaka barabarani kisha akaja baba mmoja akasema “Ndio huyu?”
“Ndio mwenyewe naomba umshushe pale stendi sawa?”
“sawa”
“Sasa dogo wewe nenda, hii gari ni mpya imetoka Bandarini inapelekwa Zambia sasa wewe watakushusha mbeya stendi”
“Haya dada”
“Chukua namba zangu na hela ya kula njiani”
“Asante dada”
Tuliingia kwenye gari aina ya Prado kisha safari ikaanza, ndani ya gari tulikuwa wawili tu, mimi nyuma dereva mbele hakuna kuongeleshana.
Mwendo wa ile gari ulikuwa kasi sana na kazi yangu ilikuwa ni kusoma vibao tu, Morogoro, Mikumi, Kitonga, Ilula, Mafinga, makambako, …..mpaka tunaingia mbeya ilikuwa ni saa sita usiku.
“Dogo shuka umefika”, alinibwaga pale kisha akatimua vumbi.
Sikujua pa kwenda mimi usiku ule, nilisikia makelele kwa mbali kama vile watu wanashangilia nikaamua kwenda huko,
Nilipofika karibu nikakuta watu wamejazana kwenye ukumbi wanaangalia mchezo wa ngumi ambapo saa tisa usiku alitakiwa apande TYSON na EVANDA.
Nililipa kiingilio namimi nikakaa pale nikaanza kusikilizia mchezo kwa kuwa nilikuwa mpenzi wa ndondi nilijikuta nikifurahia na kusahau machungu yote.
Mpaka saa kumi na moja pambano lilikuwa limeisha na kila mtu alikuwa akienda kwake.
Ni kama kulikuwa kumekucha na pale stendi walijazana wasafiri kibao.
Nilizuga mpaka pakapambazuka vizuri kisha nikaanza kuulizia kwa Yule afisa wa polisi.
*Naomba nisilitaje jina lake hapa kwasababu mpaka saivi ni askari tena wa cheo kikubwa mno hivyo nitatumia jina la AfANDE MNDEME.*
Nilianza kuulizia watu kwa afande mndeme kisha mama mmoja akaniuliza “Huyu RPC Mpya wa Mbeya”
“Ndio mama”
“Nenda pale makao makuu ya Polisi mkoa”
“Sipajui mama”
“ panda hais hapo wambie wakushushe polisi, panda hiyo hapo”
…………………………….
“Shkamoo afande,”
“Marhabaaa una shida gani”
“Namuulizia afande mndeme”
“Bado hajaja ofisini na leo hatakuja”
“Wewe nani wake”
“Yeye ni Kaka yake Mama”
“Kwahiyo ni mjomba wako”
“Ndio” (nilidanganya)
“Mwita Muonyeshe kwa Afande Mndeme”
Nilipelekwa kisha nikaonyeshwa Nyumba. Nilielekea kwenye ile nyumba huku nikijipanga cha kusema.
Nilipofika nilipishana na gari getini ambayo ilisimama, ikashushwa kioo kisha sura ya mtu kama askari ikajitokeza dirishani.
“Wewe ni nani na unaenda wapi”
“Naitwa …….. namtafuta Afande Mndeme”
“Unamjua ?”
“Hapana ila nimeelekezwa kwake”
“Umeelekezwa na nani”
“Na afande Buretha”
“ahaaa kwasasa sina muda ila ingia hapo nyumbani jitambulishe unisubiri hapo”
Aliondoa gari kisha nikaingia ndani na kusalimia watu niliowakuta humo lakini cha ajabu hakuna hata aliye niambia kaa ama leta begi tukupokee.
Nilichukua jukumu la kukaa mwenyewe kwenye makochi hadi alipokuja dada mmoja ambaye nilijua kuwa ni mfanyakazi wa ndani na kuchukua kibegi changu akanitengea chai nikanywa.
Baadae nilimuona ameshika fagio anaenda kufagia nje, nilichukua lile fagio nikamwambia aendelee na kazi zingine.
Nilifagia uwanja, nikaona nyasi ni ndefu pale uwanjani nikachukua slesha nikaanza kufyeka zile nyasi hadi Yule mama na watoto wake wakaanza kushangaa huyu ni mgeni wa aina gani anakuja na kuanza kufanya kazi.
Sikuishia hapo, nilipalilia maua nikayaweka vizuri, yale yaliyokuwa yamefifia niling’oa nikachuma mengine nikapanda.
Mpaka inafika saa nane nyumba ilikuwa inavutia kama mpya, nilimuona mtoto wa kike mmoja akinifwata fwata na maswali mengi huku akinirembulia…..
Sijui kilitokea nini lakini taarifa zilionyesha kuwa AFANDE MNDEME hatimaye aliteuliwa kuwa RPC wa mkoa wa Mbeya.
Hii kwangu haikuwa nzuri kwani ilimtoa kwenye mamlaka ya KIPOLISI Taifa na kuhamia kwenye mamlaka kimkoa hivyo ingekuwa ngumu kuwa na maamuzi kwenye swala la kunitafutia nafasi ya mafunzo ya uaskari.
Ikumbukwe kuwa ni Moshi Kilimanjaro pekee ambapo ndio kuna chuo cha mafunzo ya upolisi CCP na sio sehemu nyingine, kabla ya uteuzi wa RPC Mkoa wa Mbeya Afisa Mndeme alikuwa ndie mkurugenzi wa Mafunzo ya Upolisi kitaifa na hivyo alikuwa na mamlaka kamili ya kunipatia nafasi.
………………………
Tabia ya mtu ni kama Ngozi, kamwe huwezi kuibadili. Maisha niliyoishi pale kwa RPC yalikuwa ya kupigiwa mfano, nilikuwa mtiifu na mfanya kazi bora.
Katika ile nyumba ya RPC kulikuwa na familia kubwa sana, alikuwa na Mke na watoto sita huku watano wakiwa wa kike na mmoja wa kiume. Watoto wake wote walikuwa nyumbani kwa wakati huu ambapo wawili walikuwa wako chuo kikuu na mmoja alikuwa sekondari.
Wale wengine watatu walikuwa bado wanasoma shule ya msingi ambapo mmoja wa kiume ndie alikuwa wa mwisho.
Watoto wawili wakubwa wakike ndio walikuwa mara kwa mara wanasaidiana na dada wa nyumbani baadhi ya kazi.
Ujio wangu ulikuwa kama mkombozi kwao kwani nilikuwa nafanya kazi ambazo walitakiwa wafanye wao.
Ukweli ni kwamba tabia yangu ni kufanya kazi bila kuchagua na bila kutumwa, mara nyingi mimi ni mtu wa kujitolea lakini hapa kwa RPC nilikuwa nafanya kazi kwa sifa, nilikuwa na lengo langu, kwanza nilitaka nipendwe ili niishi pale ndani kwa amani lakini pia kupendwa kungenifanya nisaidiwe shida yangu.
Nilikuwa naamka alfajiri saa kumi namoja na kuanza kudeki nyumba, nikimaliza kudeki naosha vyombo nikimaliza kuosha vyombo navifuta na kupanga kabatini.
Nikimaliza kupanga kabatini nje kunakuwa kumepambazuka hivyo naenda kufagia uwanja, namwagilia maua na kuhakikisha kuwa mazingira yanakaa safi.
Ndani ya siku kadhaa ambazo nilikaa hapa kwa RPC nyumba ilibadilika sana japo sikuwahi kuishi hapo kabla sijaja lakini niliwasikia wakisimuliana.
Japo RPC mpaka wakati huu sikumuona tangu tulivyopishana pale getini siku nakuja lakini sikujisikia vibaya kwani nilikuwa napendwa sana pale nyumbani.
Siku moja nikiwa nimemaliza kazi zangu za usafi nilimuona mke wa RPC ambaye kwa wakati huu nilikuwa namuita mama akiwa anatoka na furushi la nguo za kufua, zilikuwa ni nguo zake za mume wake pamoja na za wale watoto wadogo watatu.
Aliwaita watoto wake wale waliokuwa wanasoma chuo kikuu lakini wote hawakujitokeza, hapa ndipo nilipoamua kutumia fursa nyingine. Mama alivyoingia ndani tu nilichukua dishi nikajaza maji nikatia sabuni ya unga na kuanza kufua zile nguo nikianza na zile za watoto.
Alishangaa sana alivyojitokeza na kunikuta nafua, nilimuona akiwa amepigwa na butwaa lakini mwisho nikaona tabasamu likichanua usoni mwake.
Alinisogelea pale nilipokuwa nimeinama akanishika mgongoni akasema
“Asante mwanangu lakini hutakiwi kujitesa hivi, ungepumzika tu hizi ningezifua”
“Usijali Mama mimi najisikia tu kukusaidia”
“Jamani asante sana basi ngoja namimi nikae tuungane.”
“Ungeacha tu mama mimi hizi si kitu kwangu”
“Hapana ngoja tusaidiane”
Basi Yule mama alikaa na kuchukua dishi lingine kisha akaanza kufua nguo zake mwenyewe, tulifua huku tukipiga story mbalimbali ambazzo nyingi alikuwa akiniuliza kuhusu historia ya maisha yangu.
Sikumficha kitu nilimsimulia kila kitu kuhusu mimi na alisikitika sana ila akanisifu kwa kuwa mpambanaji na mvumilivu.
“Usijali Sam Hizi ni changamoto tu za maisha, Mume wangu ana roho ya utu sana atakusaidia tu”
“Nitafurahi sana akinisaidia”
Wakati tunaendelea kufua walikuja wale watoto wakubwa wa kike wa RPC wakachukua ndoo wakawa wamekalia pale tunapofua.
Nao walikuja na nguo zao chache wakaanza kuungana na sisi kwenye kufua, wakati huu tulikuwa tumeshafika katikati ya kazi ya kufua ambapo Yule mama aliamua kusuuza nguo na kuanika huku akiniacha mimi nikiendelea kufua.
Mtoto wa RPC aliyekuwa anaitwa Verity alikaa pale alipokuwa amekaa mama yake na kuanza kufua akiwa amekaa pale.
Katika kitu ambacho kilinishangaza ni kwamba wakati anafua macho yote yalikuwa kwangu kitendo kilichonifanya nifue kwa aibu.
Kitu kingine ambacho kilinishtua ni kwamba alianza kukaa kwa kuachia mapaja yake wazi. Hali hii ilinipa shida sana kwani ukweli Yule mtoto alikuwa mzuri na alikuwa na mapaja mazuri mno, yalikuwa meupe na manene, kwakuwa alikuwa amevaa kanga na chupi pekee ile kanga ilifunuka na kubakisha chupi nyeupe ikiwa iko wazi kabisa.
Yule mwenzie alimuita kwa lengo ambalo nilijua ni kumtaka akae vizuri japo waliambiana kwa ishara lakini sikuona mabadiliko yeyote kwani alicheka tu na hakurudishia kanga yake vizuri.
Mateso ndani ya mwili wangu yalianza kwani sehemu zangu zilianza kusisimka na kujikuta nikihisi mazingira ya kuaibika.
Aliyeninusuru kwenye ile dhahama ni mama mwenye nyumba kwani alipokuja tu Yule dada Verity alifunika mapaja yake haraka hivyo kuziruhusu sehemu za mwili wangu kurudi kwenye hali yake.
Katika mambo ambayo nilijiapia ni kwamba kama nitakaa kwenye nyumba ya mtu kwa lengo la kusaidiwa nitajizuia kwa nguvu zangu zote kutoshiriki mapenzi na mtoto wa ndani ya nyumba nitakayokuwa ninaishi.
Dada Verity nilikuwa namlaani sana kwani alikuwa anahatarisha nadhiri yangu lakini nilimuomba Mungu aniisaidie.
Zoezi la kufua lilisha vyema kisha tukaingia ndani kwa ajili ya chai, katika hali ambayo sikuittegemea siku ile Dada Verity aliniandalia chai na kuniwekea mezani kisha akaninawisha mikono na kunikaribisha.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)