MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (9) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA TISA TULIPOISHIA... Mpira ulikuwa umeanza na watu walikuwa wanashangilia kweli kweli, timu ya JWTZ ilionekana iko imara sana kwani mpaka inatimu dakika ya 15 tayari walikuwa wameshapeleka mashambulizi mazito sana kwenye lango la timu ya Polisi na dalili zilionyesha Timu ya Polisi itafungwa. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Dakika ya 30 tayari mchezaji machachari ambaye kwasasa anachhezea klabu ya Simba alikuwa ameachia shuti kali lililomshinda golkipa na kuelekea langoni ambapo beki wa Timu ya jeshi la polisi aliamua kuudaka kwa mikono. Kwa sharia za soka ilibidi Yule beki alimwe kadi nyekundu na penati ikawekwa. Watu wote uwanjani walitulia kimya wakisikilizia penati ile…… Goooooooooooooo! Timu ya Polisi ilikuwa imefungwa goli moja baada ya mpiga penati kuachia shuti kali lililompiga kipa kicwanii na kurudi uwanjani na kukutana tena na mpigaji wa penati…