Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mpira ulikuwa umeanza na watu walikuwa wanashangilia kweli kweli, timu ya JWTZ ilionekana iko imara sana kwani mpaka inatimu dakika ya 15 tayari walikuwa wameshapeleka mashambulizi mazito sana kwenye lango la timu ya Polisi na dalili zilionyesha Timu ya Polisi itafungwa.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Dakika ya 30 tayari mchezaji machachari ambaye kwasasa anachhezea klabu ya Simba alikuwa ameachia shuti kali lililomshinda golkipa na kuelekea langoni ambapo beki wa Timu ya jeshi la polisi aliamua kuudaka kwa mikono.
Kwa sharia za soka ilibidi Yule beki alimwe kadi nyekundu na penati ikawekwa.
Watu wote uwanjani walitulia kimya wakisikilizia penati ile……
Goooooooooooooo!
Timu ya Polisi ilikuwa imefungwa goli moja baada ya mpiga penati kuachia shuti kali lililompiga kipa kicwanii na kurudi uwanjani na kukutana tena na mpigaji wa penati aliyemalizia kwa shuti dogo lililoingia nyavuni bila wasiwasi.
Uwanja ulikuwa umelipuka kwa shangwe za Upande wa JWTZ Kwani walikuwa wanaongoza, walikuwa wakiimba nyimbo nyingi ambazo zilikuwa zinawadhihaki jeshi la Polisi kuwa wao ni wanawake zao.
Polisi walikuwa wamechuukia mno na harufu ya Vurugu ilikuwa inanukia, hasara kwa tiku ya jeshi la Polisi ni kwamba Golkipa wao alikuwa ameumia na kalala chini huku akitibiwa.
Aliamka huku akionekana kuwa mchovu lakini akalazimishwa kucheza kwani hawakuwa na golikipa mwingine.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa timu ya Jeshi la polisi kuwa Ieshafungwa goli Moja.
Shangwe za JWTZ zilikuwa nyingi na walikuwa wanazunguka uwanjani kwa style ya kupiga Kwata huku wakionyesha ishara ya Salute.
Polisi walikuwa wanapeana mikakati mingi ya kukomboa goli huku wakiulizana watapata wapi golikipa wa kuwasaidia.
“Mimi ni Golikipa Mzuri, niko tayari kucheza”
Niliongea kwa kujiamini lakini watu walikuwa wamenikodolea macho tu….
“Kwani wewe ni nani?”
“Mimi naitwa Sam, naishi hapo kwa RPC”
“Wewe ndie ulikuja siku ile ukiw aunaulizia RPC anakaa wapi?”
“Ndio, ni mimi”
….achaneni nae bwana hatuwezi kuchezesha mtu ambaye hatumjui, hata hivyo mchezaji anatakiwa awe askari….
Askari huyu alisikilizwa na hatimaye watu wakanipuuza na kipenga cha kuita wachezaji uwanjani kilipulizwa na wachezaji wakaingia huku wadau na mashabiki wakirudi kwenye mabenchi yao.
Moyoni nilikuwa naumia sana kwani niliona kabisa kuwa nina uwezo wa kuisaidia ile timu lakini hawaniamini.
Mechi ilikuwa imeanza kwa kasi huku Timu ya Polisi ikifanikiwa kurudiha goli kunako dakika ya Tatu tu ya kipindi cha pili.
Hali hii ilisababisha mchezo uwe mkali na wa kuvutia ambapo dakika ya kumi ya mchezo tayari JWTZ walikuwa wameongeza goli na ubao ukawa unasoma 2-1.
Tambo na makelele uwanjani kutoka kwa JWTZ dhidi ya Jeshi la Polisi zilikuwa nyingi sana, upande wa Jeshi la Polisi ukiwa unaongozwa na RPC walikuwa na hasira sana wakitamani goli lirudi.
Dakika ya 26 kipindi cha pili kona iliyokuwa inapigwa upande wa Jeshi la Polisi ilisababisha kuumia kwa mara ya Pili kwa Golikipa wa Polisi ambaye hakuweza tena kuendelea na hapa Polisi wakawa wameweka mikono kichwani wasijue cha kufanya.
Kwa ujasiri nilimuendea Yule Kocha nikamwambia “ nichezeshe mimi, sitakuangusha”
kocha aliniangalia kwa macho ya kidadisi huku akiwa amenikazia sana na kuonekana kunikagua juu mpaka chini kisha akamfwata Kamisaa na kumwambia
“Nabadilisha golikipa”
Kamisaa alifanya mawasiliano ambapo Golkipa Yule aliyekuwa ameumia alitolewa akawa anatibiwa nje na mimi nilikuwa ndani ya Jezi naingia uwanjani.
Kati ya watu walioshangaa mimi kuingia uwanjani ni RPC ambaye alimfwata kocha akimwambia anitoe lakini wakati anamwambia hivyo tayari nilikuwa naruka ruka kwa manjonjo golini kwangu.
Kila mtu alikuwa ananishangaa kwani wengi walikuwa hawanijui. Dakika zilikuwa zimesogea huku nikichomoa mikwaju michache midogomidogo na hatimaye dakika ya 45 ya kipindi cha pili timu ya jeshi la polisi ikarudisha goli na mchezo kuwa 2-2.
Uwanja ulikuwa umelipuka na mimi nilipata ujasiri nikawa napanda mpaka mbele kusaidia mashambulizi kitendo kilichofanya nishangiliwe kupita maelezo.
Mwembwe zangu ziliniponza dakika ya mwisho ya nyongeza kwani nikiwa nimetoka langoni nasaidia mashambulizi ilipigwa kaunta ataki ambayo ilinilazimu nikwatue mchezaji wa JWTZ katika eneo la hatari kwani alikuwa anelekea kufunga.
Nilipigwa kkadi ya Njano na penati ikawekwa, ukweli nilijisikia vibaya sana kwani nilijua lawama zote zitakuwa kwangu na kweli hata kabla ya penati kupigwa niliwasikia wachezaji wa timu yangu wakiongea kwa lawama ambapo nilisikia mmoja akisema
“Kocha nae sijui magolikipa wengine anawatolea wapi, ona sasa anatuponza”
Wakati huu uwanja mzima ulikuwa kimya wakisubiria penati ipigwa nah ii ndio ingeamua mshindi wa leo kwani muda ulikuwa umeshaisha.
Kama kawaida yangu nilikuwa niko Golini naruka ruka kwa mbwembe huku nikienda kushoto – kulia, Juu – chini alafu nawaonyeshea mashabiki ishara washangilie.
Kwa mbali nilimuona VERITY na RAFIKI wakiwa wamesimama sambamba na RPC wanaangalia penati hii.
Moyoni nilijawa na ujasiri wa ajabu huku nikiwa nimeukazia macho ule mira na akili yangu yote ikawa kwenye mpira.
“Prrrrrrrrrrrrrriiiiiiiiiii”
Kipenga kilipulizwa nikamuona mpiga penati mwenye misuli na mwili mkubwa akirudi nyuma hatua kadhaa, akili yangu yote ilikuwa mguuni, kwake, machoni kwake kujua anaangalia wapi na kwenye mpira.
Nilipomtazama machoni alipokuwa anakuja niligundua ameangalia sehemu mbili kwa wakati mmoja kisha akautazama mpira, akili yangu ilinituma kuwa sehemu ya mwisho kuangaliwa ndiyo atapigia mpira ule namimi nikawa nimejiandaa kuelekea upande ule.
Shuti kali lilipigwa nikaliendeeeeaaaaaaaaa kisha viganja vyangu viwili vikikumbatia kitu kikubwa cha duara ambacho nililala nacho chini kama nyani.
Nilikuwa nimeokoa Penati na uwanja mzima ukawa umetawaliwa na shangwe za Jeshi la Polisi.
Hakuna aliyeamini pale uwanjani kwamba penati ile haijawa goli, Refa alikimbilia eneo la golini nilipokuwa bado nimelala akiangalia mpira uko wapi.
Watazamaji uwanjani bado walikuwa hawajaamini kwamba mpira ninao kwapani, walidhani kuwa huenda umetoboa nyavu na kupitiliza.
Refarii akiwa bado hajapuliza filimbi ya kuashiria kama ni goli ama sio goli alikuja pale nilipo akainama kisha akanigusha ishara ya kunitaka ninyanyuke.
Nilinyanyuka kwa Madaha makubwa huku nikiwa nimeukumbatia mpira kwa mikono yangu miwili, kitendo hiki kiliamsha shangwe kwa watazaaji wote ambao walikuwa upande wa timu ya jeshi la polisi.
Katika hali ya furaha wachezaji wenzangu walinivamia kwa fujo huku wakinikumbatia hadi kuniangusha chini kwa furaha.
Kitendo cha kuurusha mpira mbele tu refarii alipuliza filimbi ya kumaliza mpira na kilifwata sasa ni hatua ya Penati kwani ilikuwa ni lazima mshindi apatikane na akabidhiwe zawadi kemkem na Kombe.
Manahodha wa timu zote mbili walikuwa katikati ya uwanja wakichagua goli la kuanzia nan i timu ipi ianze kupigiwa penati, shilingi ilirushwa na hatimaye timu ya JWTZ ndiyo ikatakiwa ianze kupiga penati hivyo nilipaswa kuelekea Golini.
Kwa mbwembwe nyingi nilianza kukimbia huku nikizungusha mikono yangu na kuwaonyeshea ishara ya mashabiki wa Jeshi la Polisi kushangilia, nao bila ajizi walilipuka kwa shangwe nyingi.
Uzuri ni kwamba pale uwanjani tayari mashabiki walikuwa wameshajigawa, wengine walikuwa wanashabikia upande wa JWTZ na wengine walikuwa wanashabikia upande wa POLISI. Wananchi ambao hawakuwa wanajeshi wala Polisi nao walikuwa wameshajogawa kwa mapenzi yao na kila mmoja alikuwa ameshachagua kati ya kushabikia JW ama timu ya Jeshi la Polisi.
Nilikuwa nimeshasimama Golini na tayari mchezaji wa JW alikuwa ameshaweka mpira kwenye eneo la Penati akisubiria refarii apige filimbi kisha apige mpiara.
Kama kawaida yangu nilikuwa situlii, nilikuwa naruka kwa mbwembwe mara upande huu mara upande ule, naenda mbele narudi nyuma.
Katika hali ya ajabu sana nilijikuta moyoni nikiwa na hofu sana, “priiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii”
Kipenga kilikuwa kimepulizwa na tayari mpigaji alikuwa amerudi kaa hatua nne nyuma,
Kusema ule ukweli nilikuwa nimelala kulia na mpira ulikuwa kushoto, tayari goli lilikuwa limeingia na mchezaji huyu alikuwa anashangilia akielekea walipo wenzake.
Zamu ya timu yetu kupiga penati niliomba ile penati nikapige mimi, walinikubalia nikaweka mpira kati nikarudi nyuma hatua kadhaa na kuachia shuti kali ambalo lilipaa juu ya goli na kudondokea upande wa mashabiki, maana yake nilikuwa nimekosa penati.
Nilijisikia mnyonge sana na hata wachezaji wenzangu walikuwa waeshika vichwa wakiona jinsi abavyo tulikuwa tunaenda kuukosa ubingwa kwani nilishafungwa penati moja na pia nilikuwa nimekosa penati niliyopiga mwenyewe, nilikuwa naumia kuona yale matokeo yananihusu sana mimi.
Nilijipa ujasiri na kuelekea Golini ambapo safari hii sikuwa na mbwembwe zozote ila nilikuwa makini sana kuwaangalia wapigaji wa penati.
Mpigaji wa safari hii alikuwa ni golikipa wa timu pinzani ambaye alikuwa ameweka mpira na kurudi nyuma hatua tano, aliachia shuti kubwa ambalo liliniuza kabisa nikaangukia upande wa kulia na mpira ukipita kushoto lakini sikukubali, nilirusha mguu wangu mmoja wa kulia ambao uliupaisha mpira na kuurudisha uwanjani kitendo kilichoamsha shangwe nyingi.
Mpigaji wa upande wetu alienda akapiga penati na kufunga kiulaini kabisa hivyo kila timu ikawa imepiga penati mbili, kukosa moja na kupata moja.
Niliirudi golini ikapigwa penati ambayo safari hii niliidaka kabisa kama nyani anayedaka buyu. Watu walishangilia lakini shangwe zao zilizimwa baada ya mchezaji wa upande wetu kupiga penati nje kabisa ya goli na kufanya matokeo yawe 1-1 hadi wakati huu ambapo kila timu imepiga penati tatu.
Nilirudi tena golini ambapoo mpira ulikuwa unapigwa kwa timu ya JW kupiga penati ya nne, penati hii niliipangua kwa mkono wangu wa kulia ambapo mpira ulikuwa umepigwa pembeni juu kabisa kwenye engo lakini niliruuka kama ngedere na kuugusa kwa mkono wangu wa kulia na kuutoa nje.
Shangwe uwanjani kwa Upande wa Jeshi la Polisi zilikuwa nyingi lakini zilizima ghafla kwani kila mtu alikuwa akimtazama mchezaji wa POLISI ambaye alikuwa anaenda kupiga penati ya mwisho ambayo itaamua matokeo.
Nilikuwa nina hofu kwani sikutamani kurudi tena golini kudaka Penati, nilikuwa nasali kimya kimya ili penati ile iwe goli.
Goooooooooooooooooooooooooooooo! Mpira ulikuwa wavuni na uwanja mzima ulikuwa ni shangwe na nderemo kwa upande wa polisi kwani tulikuwa tumeshinda Kombe hili.
Pamoja na kucheza mechi moja lakini kamisaa alinitaja kuwa Golikipa Bora wa michuano hii huku akiniita afande Sam.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)