SHEREHE KUZIMU (20)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI ILIPOISHIA... Kila mtu alikuwa aking’ata meno kutokana na baridi ilivyokuwa ikipenyeza katika ngozi ya miili yao. Kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inazidi kunyesha ilisababisha msafara uzidi kwenda kwa mwendo wa taratibu sana. Vivian alikuwa katika gari moja ambayo ilikuwa imebeba watu wa familia. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Mama yake pia alikuwepo katika gari hilo. Vivian alikuwa akiwasiliana na mama yake kwa ishara za kishetani ambazo hazikuweza kufahamika na mtu yeyote. Watu waliokuwa katika misafara walikuwa wakiimba nyimbo za maombolezo.. Nyimbo zile zilisababisha wawe wanajisikia vibaya sana kwasababu roho wa ibilisi alikuwa ndani yao. Kwa mwedo wa taratibu saa saba mchana msafara ulifika katika eneo la makaburi kwaajili ya kufanya maziko. Maziko yalifanyika wakati mvua ikiendelea kunyesha. Kila mtu aliyekuwa msibani alione…