SHEREHE KUZIMU (24)

Zephiline F Ezekiel
SHEREHE KUZIMU (24)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE ILIPOISHIA... Mwili wake uliishiwa kabisa nguvu na pia tumbo lilikuwa linanguruma kutokana na wasiwasi mwingi uliokuwa ndani ya mtima wake. “Unaumwa?” Bi Diana alimuuliza mume wake ambae bado alikuwa anashangaashangaa kama vile abiria aliyeachwa na gari, stendi. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... “Hapana, nipo sawa.” “Sasa kilichokuangusha na kupoteza fahamu ni kitu gani?” Bi Diana alihoji. Bashingwa alimsimulia mke wake kila kitu, mpaka ndoto mbaya aliyoiota. Bi Diana alishtuka sana pindi alipokuwa akimsikiliza mume wake akimsimulia ndoto ile iliyokuwa ya kutisha. Mume wake alipomweleza kwamba alipozinduka katika ndoto mbaya aliyokuwa anaiota, hakumkuta kitandani, alipuuzia kwa kuona kwamba, huwenda ndoto ilimchanganya kwasababu yeye alikuwa kitandani amelala. Furaha ya kukamilika kwa mipango ya mauwaji ya wapinzani wao wa kibiash…