
Mtunzi: Frank Silaa
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Katika historia ya mganga huyu inasemekana aliwahi kuhamishia mlima Kilimanjaro mkoani kwake kwa muda wa masaa matatu. Ahmedi Juma, ndiyo jina la mganga huyu, japokuwa watu wengi wanamfahamu kwa jina la Kiboko, kutokana na sifa yake ya kutokushindwa na jambo.
KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA NAYO...
Mara baada ya malipo katika nyumba ya wageni ya Kibo guest house iliyopo mjini Moshi, Benedict na mwenzie walijitutumua kubeba mabegi yao hadi kwenye chumba namba 8. Pamoja na kwamba walionekana kuwa na uchovu mwingi wa safari lakini kila mmoja alionyesha hamu ya kumtamani mwenzie kimapenzi. Safari yao ilikuwa ni ya furaha sana. Ucheshi wa Benedict ulisababisha tabasamu na vicheko mwanana visififie katika uso mzuri wa Adela. Baada ya kutua mabegi yao chumbani mule, Adela alishindwa kuendela kukumbatia hisia zake kwahiyo alimvuta Benedict kisha wakaanza kunyonyana ndimi. Mapenzi yalianza kukolea huku miguno ya kimahaba ikiendelea kushika hatamu, pindi walipokuwa wakitomasana taratibu.
Naam! Ulikuwa ni muda ambao kila mmoja alionyesha kuwa, alikuwa anautamani haswa. Adela alisikika akihema kwa pupa wakati Benedict alipokuwa akizidi kumshikashika katika sehemu mbalimbali za mwili wake. Hisia za Benedict zilizidi kuja juu, jambo ambalo lilipelekea amsukume Adela na kuangukia kitandani. Benedict alivua tai iliyokuwa ikining’inia shingoni na kuitupa pembeni, kisha akafungua vifungo kadhaa vya juu ya shati lake harakaharaka na kupanda kitandani, ambapo waliendelea na michezo ya kimahaba. Waliendelea kufurahishana kitandani pale huku Benedict akiendelea kuzisasambua nguo za Adela moja baada ya nyingine. Mapigo ya moyo wa Adela yanaenda kwa kasi mno, kwasababu anachokifanya muda huu, ni kipya kabisa katika maisha yake.
Hajawahi kulala na mwanaume ila leo amedhamiria kabisa kuonja ladha ya penzi. Amechoka kusimuliwa na marafiki zake ndiyo maana leo anataka ajionee mwenyewe. Bila kupoteza muda Benedict anakuja juu ya kifua cha Adela na kisha wanaanza kupeana mapenzi mazito. Adela anasikika akilalama kuhisi maumivu, kwavile ilikuwa mara yake ya kwanza, kufanya tendo hilo. Sekunde kadhaa baada ya wapendanao hawa kuanza kupeana penzi, wanakatisha zoezi lao baada ya kushuhudia mtikisiko wa ajabu ukitingisha kitanda chao pamoja na chumba kizima kwa ujumla.
Ghafla vishindo vizito pamoja na kelele za watu kutoka nje vinaanza kusikika vikiomba msaada. Wakati Benedict na Adela wakiwa katika hali ya sintofahamu wanashangaa kuona ukuta wa chumba chao unaporomoka na kuwajeruhi vibaya kichwani. Hofu inajaa mioyoni mwao baada ya kuona wapo katika eneo la hatari kwa muda ule. Harakaharaka Benedict anamshika mkono Adela na kuanza kukimbia kuelekea nje ya chumba kile ili waweze kunusuru maisha yao. Hata hivyo jitihada zao za kukimbilia nje zinagonga mwamba baada ya kuangukiwa na kifusi cha ukuta wa nyumba. Benedict anaonekana kufukiwa zaidi na kifusi hiki huku Adela akionekana kurushwa pembeni, na kupata majeraha makubwa mwilini mwake.
Moyo wa Adela unapata maumivu makubwa sana baada ya kuona mpenzi wake amefukiwa katika kifusia ambacho hawezi kumnasua. Anachukua jukumu la kupiga kelele ili kupata msaada lakini, kila mtu kwa wakati ule anaonekana kukimbia huku na kule kuokoa maisha yake. Vilio vinatawala kila kona ya mji kutokana na vifo vilivyokuwa vikitokea muda ule. Majengo ya ghorofa yaliyokuwa katikati ya mji yote yanaonekana kuporomoka kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililokuwa linasumbua mji wa moshi usiku ule. Ni tetemeko kubwa ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Tanzania, kwani linagharimu maisha ya watu wengi sana.
Adela anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake ili waweze kunusuru maisha ya mpenzi wake lakini inashindikana kutokana na ukubwa wa kifusi kilicholala juu ya mwili wa Benedict. Kitendo cha Benedict kufukiwa na kifusi cha ukuta kunapumbaza akili ya Adela na kusahau kwamba bado yupo katika eneo la hatari. Wakati akiendelea kulia kwa nguvu akiomba msaada, sauti yake inazimika ghafla baada ya kupondwa na kitu kizito kichwani na kupelekea fahamu zake kupotea kabisa. Mji wote wa Moshi unakumbwa na giza nene kutokana na uharibifu mkubwa wa miundombinu uliojitokeza pindi tetemeko la ardhi lilipokuwa linaarindima.
********
Vichwa vya habari katika magazeti yote, yanaonekana kupambwa na habari ya utata wa vifo vya wafanyabiashara wakubwa wa nguo jijini mwanza. Vifo hivi vinabaki kuwa kama fumbo kubwa katika akili za watanzania wengi, kwani wapo wanaohusisha na mambo ya siasa na wapo wanaolihusisha na imani za kishirikina, ingawa hakuna aliyekuwa na uwakika. Watu wengi wanaonekana kuguswa sana na vifo hivi vya watanzania wenzao ambao wamekuwa wakipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha. Kila kona ya nchi habari hii inaonekana kusumbua fikra za watu wengi hususani wafanyabiashara wa nguo.
“Je ni zamu ya nani sasa?” hili ni swali ambalo wafanyabiashara wengi wa nguo wamekuwa wakijiuliza kila mara baada ya kuona jinamizi linawaangamiza wao tu. Pamoja na kuumiza vichwa sana kumtafuta mchawi nani lakini hawakufanikiwa kugundua ukweli upo wapi. Serikali inaunda tume itakayohusika na uchunguzi wa mauwaji ya wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakipoteza maisha kila iitwapo leo. Chakushangaza ni kwamba tume iliyoundwa kuchunguza vifo hivyo vya utata, wanakosa kabisa pakuanzia kufanya upelelezi wao ili kubaini chanzo. Hivyobasi zoezi la upelelezi linaonekana kufeli ingawa serikali haiweki bayana juu ya kushindwa kwake kugundua sababu ya vifo wa wafanyabiashara hao.
Vifo vya wafanyabiashara wakubwa wa nguo, kumi na wawili ilikamilisha idadi ya watu ambao Vivian alidhamiria kuwapeleka kuzimu kuliwa nyama. Hakuwa na mpinzani tena katika biashara ya nguo aliyokuwa anaifanya jijini mwanza. Mamia kwa mamia ya wateja wanamiminika dukani kwake kufanya manunuzi ya nguo ambazo zilionekana kuwa na mvuto sana. Wingi wa wateja dukani kwake kunamfanya awe na furaha muda wote kwasababu wateja waliokuwa wananunua nguo katika duka lake wanakuwa wameunganishwa moja kwa moja na ufalme wa kuzimu pasipo kujua. Kuzimu kunarindima kwa furaha kwasababu wafuasi wanaongeza kwa kasi kila kukicha. Uzuri wa asili pamoja na maneno matamu kwa wateja inapelekea kupata msongamano wa wateja ambao wanahitaji huduma dukani kwake.
Fauku na hayo lakini pia majini yaliyopo dukani kwa Vivian yanafanya kazi kubwa ya kuwavuta wateja ili waweze kufanya manunuzi katika duka hilo. Uso mzuri wa Vivian hauishiwi tabasamu kwasababu malengo yake ya kuwapeleka binadamu kwa wingi kuzimu linatimia. Furaha inayofurukuta moyoni mwa Vivian kiukweli haielezeki kwa kalamu na karatasi, kwasababu ni furaha isiyomithilika. Kwa upande wa Nelson anaona mambo yanakwenda sawa sawia kwasababu akili yake imefungwa. Kila mara anamsifia mke wake kwa kuonyesha uwezo mzuri katika biashara ile. Mauzo yanaongezeka kila kukicha kutokana na utitiri wa wateja dukani.
**********
Marwa anafika kwa mganga na kumweleza adhma yake ya kutaka kuitoa roho ya Benedict. Baada ya makubaliano mganga anaanza kufanya mambo yake ya kichawi ili aweze kumsaidi mteja wake. Kwa muda wa dakika thelasini majini yaliyokuwa yakitumwa kwenda kumuuwa Benedict yalikuwa yanashindwa kufanikiwa. Alitumia mbinu zake zote ili aweze kumnasa Benedict lakini kila njia ilionekana kubuma. Mganga alikunja ndita kwa hasira huku kijasho chembamba kikimchuruzika usoni mwake. Alikuwa yupo katika wakati mgumu wa kuwaza ni kwa namna gani ataweza kumsaidia mteja wake ili hali kazi aliyopewa inahatarisha maisha yake. Kwa mganga yeyote apande ama ashuke kumloga Benedict ni jambo ambalo haliwezekani kabisa. Benedict alichukuliwa na mama yake bila kujijua na kupelekwa kuzimu na kisha akajazwa majini yenye nguvu ya kipekee, elfu na mia tano ya kumlinda popote atakapokuwa. Kwa maana hiyo Benedict hawezi kudhurika kwa lolote isipokuwa kwa mapenzi ya Mungu pekee.
“Kwa inavyoonekana huyu mtu unaetaka kumuuwa analindwa na majini hatari sana ambao kwa nguvu zangu sintaweza kupambana nao, kwahiyo nakushauri nenda katafute mganga mwingine atakayeweza kukusaidia kwani mimi sintaweza.” Hilo lilikuwa ni jibu la mganga ambalo lilimkata maini Marwa.
“Naomba unisaidie mganga, nitaongeza pesa zaidi endapo utanifanikishia zoezi hili la muhimu.” Marwa alizungumza kwa huruma kusudi mganga aweze kumuhurumia.
“Haiwezekani kijana, naomba uondoke.” Mganga alizungumza kwa jazba kidogo.
Kwa mara ya kwanza mganga Ahmedi anakiri kushindwa kumsaidia mteja wake. Hiyo yote ni kwasababu amekutana na mtu ambae aingiliki kirahisi. Kwa unyonge kijana Marwa anaondoka kwa mganga akiwa na mwonekano wa kukataa tamaa. Hakuwahi kudhani kwamba mganga yule atashindwa katika jambo kama lile. Hakujua njia mbadala yakufanya ili aweze kumdhuru Benedict, kusudi aweze kupata nafasi kwa Adela. Hasira iliyokuwa kifuani mwake ilipelekea kumwaga machozi hadharani wakati alipokuwa njiani akireje nyumbani. Kwa hasira aliyokuwa nayo angefanikiwa kukutana uso kwa uso na Benedict angeweza kummeza mzima mzima. Hakuwa tayari kukubali kushindwa kumpata Adela kwasababu ya upendo wa dhati aliokuwa nao kwake. Anampenda hadi anahisi kuumwa, ndio maana amejidhatiti kwa lolote na kwa chochote ilimuradi Adela awe wake.
Kwa muda wa dakika nne na sekunde arobaini na tatu, tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa skeli ya richter 5.9, lilisababisha vifo vya watu wengi mkoani Kilimanjaro. Jeshi la polisi wakishirikiana na jeshi la wananchi wa Tanzania, wanaendelea na jitihada za kuokoa majeruhi wa ajali hii ya kihistoria. Kutokana na wingi wa vifo vilivyotokea, chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya KCMC inaonekana kujaa. Vilio vya uchungu vya ndugu jamaa na marafiki vinatawala nje ya hospitali usiku huu. Ambulensi pamoja na magari ya polisi yanaonekana kuleta miili ya marehemu kwa wingi hospitalini hapa. Idadi ya watu waliofariki inadhaniwa kuwa ni kubwa mno kulingana na ajali yenyewe. Hali ya hewa ni ya mvua mvua lakini bado haiwi sababu ya kuzuia msururu wa watu wanaoendelea kumiminika hospitalini hapa.
Katika wodi ya wagonjwa mahututi napo panaonekana kusheheni wagonjwa wengi kupita kawaida. Hali za majeruhi wengi ni za kukatisha tamaa, kutokana na majeraha ya kutisha katika miili yao. Madaktari na wauguzi wanaonekana kupishana huku na kule kunusuru hali za wagonjwa waliofikishwa hospitali. Miongoni mwa wagonjwa wanaoonekana kuwa na hali mbaya zaidi ni pamoja na Benedict. Hivyo basi hali yake mbaya inapelekea jopo la madaktari kukusanyika kwa pamoja ili waweze kuokoa maisha yake.
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi