SHEREHE KUZIMU (27)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA ILIPOISHIA... Sambamba na hilo, Vivian alipaswa kutoa kafara ya watu wasiopungua 300 kama kuonyesha heshima kwa malikia ambaye amekubali kumuachia kiti kwa hiyari. Bila wasiwasi wala kusita, Vivian anakubaliana na vigezo vyote alivyoelezwa na malikia ili ndoa yake iweze kufungwa na hatimaye akabidhiwe cheo. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Kwahiyo Vivian aliamua atumie njia ya tetemeko la ardhi katika kupata idadi ya roho alizotumwa kwa wakati muwafaka. Hiyo ndiyo ikawa chanzo cha kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi mkoani Kilimanjaro , ambalo lilimuhusisha Benedict ambaye nae amekusudiwa afe kutokana na tukio hilo. Idadi ya watu waliokuwa wamekusudiwa katika kafara hiyo inaonekana kutimia kabisa, kwani jumla ya watu 300 waliripotiwa kupoteza maisha katika tukio hilo la kiistoria. Fikra za Nelson zilizidi kusumbuka kwa mawazo d…