BABA KIUMBE WA AJABU (11)

Zephiline F Ezekiel
BABA KIUMBE WA AJABU (11)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA KUMI NA MOJA TULIPOISHIA... jamani ni kwa sababu gani? “Masalu mimi nina tatizo gani jamani, mbona kila siku matatizo yanaongezeka ni kweli mganga atanisaidia mbona mimi ni maiti inayotembea ninayesubiri kufa. Ni kweli mganga atanisaidia? JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... Mbona sina thamani ya dunia kifo changu kashikilia baba kama cha dada Monika. “Maisha haya mpaka lini kidonda mimi na sasa wamechukua nguvu zangu za kiume. Nini kimebakia kama si uhai wangu, kweli mganga atanisaidia?” Baada ya kusema yale aliondoka kipande cha mti wa mnyaa sikioni na kuutupia kwenye kapu la dawa lililokuwa pembeni yake. “Umesikia?” “Ndiyo.” “Yaliyozungumzwa yana ukweli?” “Ndiyo.” “Unajijua kuwa wewe ni maiti?” “Maiti?” Kauli ya mganga ilinishtua sana. “Hujijui?” “Sijijui.” “Mpaka sasa hivi upo sawa kama nduguzo?” “Kivipi?” “Viungo vyako vipo sawa?” “Vipo sawa.” “Kipi kilic…