
Mtunzi: Ally Mbetu
SEHEMU YA KUMI NA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Nashukuru mzee wangu.”
“Basi ondoa hofu hakuna chochote kitakachokukuta, kila atakayekugusa kitamrudia.”
Niliagana na mganga kisha nilimpitia mpenzi wangu na kurudi hotelini kujiandaa na kwenda msibani.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
SASA TUENDELEE...
Tukiwa njiani simu ya dada iliita, nilitaka kuacha kuipokea lakini niliipokea ili nijue ana shida gani.
“Haloo,” nilipokea.
“Asante Masalu, asante sana.. njoo umle nyama baba,” dada alisema kwa sauti iliyoonesha analia.
“Tena wewe ndiye ninayekutafuta mchawi mkubwa, nakuapia sitakusamehe wewe na wote hata marehemu baba mpaka nakufa. Vitendo vyote mlivyonitendea hamkuridhika mpaka mnaitaka roho yangu kwa nguvu? Hivi nikifa mtafaidika nini?”
“Nani anataka kukuua?”
“Kitendo mlichofanya wiki moja iliyopita sitawasamehe mpaka nakufa, mnanilaumu nahusika na kifo cha baba. Hebu niambieni mimi nimefanya nini kuchangia ugonjwa mpaka kifo cha baba. Kinyonga mliyemtumia ili mniue ndiye aliyemmaliza baba kwa taarifa yenu.”
“Ha! Umejuaje?” Dada alishtuka.
“Nakuapia nilikuwa nina mpango wa kuwasamehe, lakini kwa kitendo mlichokitenda jana saa sita usiku sitawasamehe milele na mimi nitajua cha kuwafanya, endeleeni kuroga nami sasa naingia vitani tuona nani zaidi.”
Kauli yangu ya vitisho japo sikuwa na nia hiyo ilimfanya dada akate simu.
“Masalu vipi mbona sikuelewi?” Mpenzi wangu aliniuliza.
“Wee waache tu.”
“Nani huyo?”
“Dada.”
“Mbona mnatishana?”
“Namtisha namwambia ukweli!”
“Kwa nini umewaambia mapema?”
“Lazima waujue ubaya wao na tena nawafuata msibani wanieleze kisa na mkasa cha kuyatafuta maisha yangu,” nilijikuta nikipandwa na hasira.
“Punguza hasira tukifika hotelini tutalizungumza, umeshawajua wabaya wako kwa nini uchanganyikiwe?”
Nilikubaliana na mpenzi wangu kurudi hotelini, tulipofika nilikuwa bado na hasira kwa kauli za dada kuwa nitamla nyama baba yangu aliyefariki kwa ajili yao wenyewe. Nilijikuta njia panda katika maamuzi yangu ya kwenda kwenye msiba wa baba. Nilijikuta nikipata ujasiri wa kwenda kwenye msiba wa baba.
“Aisee wacha niende kwenye msiba wa baba,” nilimwambia mpenzi wangu.
“Masalu nakuomba usiende.”
“Hapana lazima niende.”
“Panaweza kutokea ugomvi.”
“Na utokee, tena nakwenda kuwapa makavu.”
“ Nakuomba usiende mtatiana aibu.”
“Nisipokwenda watu hawatanielewa.”
“Bora wasikuelewe kuliko aibu itakayowakuta.”
“Hakuna aibu, mganga amesema hawatafunua midomo yao kusema lolote kwa kuiogopa aibu.”
“Mmh! Lakini ningekuwa mimi nisingeenda.”
“Lazima niende na leo watanitambua, siwezi kuishi na maadui zangu na kuwachekea.”
”Hayo ndiyo ninayokukataza, kama huwezi kuzuia hasira zako hakuna haja ya kwenda.”
“Nitajitahidi lakini moyo unaniuma baada ya kujua ubaya waliotaka kunifanyia usiku wa kuamkia leo.”
“Lakini si umepata kinga?”
“Ni kweli, lakini kama nisingepata ingekuwaje?”
“Ungepotea, lakini nakuomba ulimalize jambo hili kwa busara.”
“Nimekuelewa.”
Nilijiandaa na baadaye tuliondoka na mpenzi wangu ambaye nilimuacha nyumbani kwao na mimi kwenda kwetu. Nilipofika nilikuwa watu wengi wamekusanyika nje ya nyumba yetu wakiwepo wafanyabiashara wenzetu.
Sehemu kubwa ilikuwa imejaa magari ya watu, nilipoteremka kwenye teksi na kutembea kwenda ndani, kila aliyenitazama alinishangaa. Wengi walinipa pole ya kifo cha baba, niliwaitikia na kuingia ndani. Nilipofika ndani ndugu zangu walishtuka kuniona.
Sikujali hali ile, niliingia chumba alichokuwa mama, aliponiona aliacha kulia na kunitazama kama kiumbe cha ajabu. Kwa vile kila kitu nilikuwa nakijua sikuijali hali ile na kumsalimia.
“Shikamoo mama.”
“Marahaba.”
“Poleni.”
“Asante.”
“Mnazika saa ngapi?”
“Sijajua mipango yote wanafanya ndugu zako.”
“Kwani Masalu ulikuwa wapi?” Mama wa jirani aliniuliza.
“Nilikuwa safari.”
“Ooh! Pole sana kwa kumpoteza kipenzi baba yako, najua kiasi gani alivyokuwa akikupenda.”
“Ni mapenzi ya Mungu.”
“Na kweli, ni yeye aliyetoa na ndiye aliyetwaa.”
“Kila neno litatimia.”
“Masalu,” sauti kali ya dada iliniita.
“Unasemaje?”
“Njoo nje.”
“Kufanya nini?”
“Nimekwambia njoo au nitakutoa kwa nguvu.”
“Jeuri hiyo huna.”
“Salome hebu zungumzeni kwa ustaarabu hamjui hapa ni msibani?” Mama aliingilia kati.
“Kafuata nini? Namuuliza kafuata nini, aliyotaka yamekuwa anataka nini tena?”
“Tena wewe malaya wa kike funga domo lako,” Kwa mara ya kwanza nilimvunjia heshima dada yangu.
“Jamani mama Salome ni maneno gani hayo?” Jirani alitushangaa.
“Samahani jirani naomba utupishe mara moja,” mama alimtoa nje jirani baada ya kuona tunataka kumwaga mtama kwenye kuku wengi.
Baada ya jirani kutoka nje, tulibakia watatu ndani, mama alisema kwa sauti ya kilio:
“Salome unafanya nini?”
“Mama hujui aliyofanya mwanao, kamuua baba kisingizio eti tulitaka kumuua jana.”
“Una uhakika gani nimemuua baba?” Nilimuuliza.
“Kumbuka ulipokuja kumuona baba alisema tukuondoe kwa vile unataka kumuua.”
“Sikiliza wee malaya,” nilimnyooshea kidole dada.
“Ha! We niliyekushika kinyesi chako unanivunjia heshima?”
“Tena shetani wa kike, yaani nakuapieni yote mliyoyafanya juu yangu hamkuridhika, mkaamua jana kunifutilia mbali kwa uchawi wa kinyonga? Mama nisikilize vizuri tena kwa makini. Sitaisamehe familia yako mpaka naingia kaburini.”
“Usitutishe mchawi mkubwa.”
“Nafahamu kila kitu mnakijua hata mama niliyekuwa nakuamini kwa ajili ya mali unakubali wanao tuishe kwa ajili ya tamaa ya wachache. Nilikuwa na huruma na ndugu zangu na kukubali kuteseka kwa ajili yao, lakini hili la kutaka kuniua sitawasamehe milele.”
“Muongo mkubwa, wewe ndiye uliyemuua baba.”
“Mama nimemuua vipi baba?”
Mama hakujibu alitazama chini kwa aibu, niliendelea kusema kwa hasira lakini sauti ilikuwa ya chini.
“Dada Salome unajua kila kitu wewe ndiye uliyempa dawa mpenzi wangu anipake ili kuua nguvu zangu za kiume mlifanikiwa. Lakini mlisahau mimi si mzimu wa familia nilijua mlitaka kunitoa kafara kama dada Monika lakini mambo hayakwenda hivyo.
“Niliweza kupita chini juu na kuweza kuidhibiti hali hiyo, baada ya hapo hamkuridhika mkataka kunigeuza ndondocha mkashindwa na mwisho mkataka kuniua matokeo yake mmemuua baba. Mnakosa haya kunishtumu, hivi uchawi wenu wa kinyonga ungefanikiwa mimi ningekuwa wapi?
“Nasema hivi naondoka si hamnitaki, naondoka ila nawatahadharisha mkiendelea na mchezo wenu mtapukutika wote kama mlivyomtanguliza baba. Mimi si Monika ni Masalu,” nilisema nikiwa nimebadilika, sikuwa Masalu wa kuonewa tena.
“Masalu,” Dada Monika alitaka kusema kitu.
“Kwanza kabla sijaondoka nataka niione maiti ya baba yangu kwa mara ya mwisho.”
“Hapana Masalu baba huwezi kumuona,” dada Monika aliweka ngumu.
“Unajua nawastahi sana, najua kila kitu, kama mnataka siri yote nikaitoe kwa watu nje nikatazeni,” nilipiga mkwara mzito.
“Maiti ya baba yako imeharibika,” mama alisema kwa sauti ya upole.
“Hata kama iweje ni baba yangu nina haki ya kumuona.”
“Masalu acha tu baba yako azikwe, ameharibika sana,” mama aliendelea kunibembeleza.
“Mama mimi si mtoto wako?”
“Mtoto wangu.”
“Aliyekufa si baba yangu?”
“Baba yako.”
“Basi nipeleke nikamuone.”
Walitazamana kwa muda kisha mama alisema kwa sauti ya chini.
“Salome mpeleke mdogo wako akamuone baba yake.”
“Mama tulizungumza nini?”
“Salome sitaki ubishi hebu maliza hili kwa nini tuwafaidishe watu?”
Nilipelekwa chumba ulicholazwa mwili wa baba, nilikuta amefunikwa shuka, niliifungua upande wa kichwani. Kidogo nikimbie baada ya kukuta kiumbe cha ajabu kilichokuwa kama mnyama chenye manyoya na meno ya kutisha. Nililivuta shuka lote, sikuamini nilichokiona. Baba alikuwa amebadilika na kuwa kiumbe wa ajabu, mwili mzima akiwa na manyoya kama mnyama.
Nilimgeukia dada Salome.
“Baba yupo wapi?”
“Si huyo mbele yako.”
“Hapana huyu si baba yangu, naomba unioneshe baba yangu,” nilijikuta nikipandwa na hasira.
“Masalu huyu ndiye baba, tangu alipoanguka kila siku alikuwa akibadilika na kuwa kiumbe cha ajabu mpaka mauti yalipomkuta,” dada Salome alinipa maelezo ya sababu ya hali ya baba kuwa vile.
“Jamani mmeona mwisho wa ubaya aibu kama hii.”
Mara mlango ulifunguliwa na kuingia kaka zangu walioonekana wanatoka kunywa.
Jamani huyu mchawi amefuata nini?”
“Mama ndiye kampokea,” dada Salome alijibu.
“Toka nje, hebu kalete panga amfuate baba.”
“Kama jana mlishindwa kuniua kwa uchawi wa kinyonga na matokeo yake mkamuua baba, hamtaweza kuniua kamwe. Nitaondoka kwa kupenda si kwa kulazimishwa na familia ya wanga.”
Baada ya kusema vile niligeuka na kutoka nje, bila kuzungumza na mtu niliwapita watu ambao hawakuelewa kinachoendelea. Nilielekea barabarani na kukodi teksi iliyonipeleka nyumbani. Nilimpigia simu mpenzi wangu anifuate nyumbani. Alishangaa na kuniuliza:
“Vipi mbona unasema upo nyumbani kwako wapi, msibani?”
“Noo, kwangu kabisa.”
“Utani huo, si ulikwenda msibani au baba yako hakufa?”
“Amekufa.”
“Sasa mbona upo nyumbani?”
“Ni hadithi ndefu njoo mara moja nyumbani.”
“Nakuja.”
Nilikata simu na kujilaza kwenye kochi nikiwa bado hasira imenijaa moyoni. Baada ya muda mpenzi wangu alifika nyumbani na kunikuta katika dimbwi la mawazo. Hata alipoingia sikumuona alinishtua kwa kuniita.
“Masalu....Masalu.”
“Ee..eeh.”
“Jamani mbona hivyo?”
“Aah, umekuja saa ngapi?”
“Ndiyo naingia, mbona umerudi mapema mmeshazika?”
“Bado.”
“Sasa mbona umerudi?”
“Wee acha tu.”
“Kuna nini tena?” Aliniuliza kwa mshtuko kidogo.
“Wee acha tu.”
“Niache nini Masalu! Hebu nieleze kuna nini?”
Sikuwa na budi kumueleza niliyokutana nayo msibani, mpenzi wangu aliniangalia kwa huruma na kusema:
“Lakini Masalu we mbishi sana, si nilikueleza usiende ukabisha.”
“Ilikuwa lazima niende kwenye msiba wa baba yangu kwa vile unanihusu.”
“Japo unakuhusu lakini mazingira yake hayakuwa mazuri.”
“Yawe mazuri vipi ikiwa aliyekufa ni mzazi wangu?”
“Sawa mzazi wako lakini unajua kifo chake kilitokana na nini, Na dada yako baada ya kifo cha baba yenu maneno aliyokuambia, sasa nini kigeni kwako?”
“Nimekuelewa, lakini watanitambua.”
“Lakini Masalu we mbishi sana, si nilikueleza usiende ukabisha.”
“Ilikuwa lazima niende kwenye msiba wa baba yangu kwa vile unanihusu.”
“Japo unakuhusu lakini mazingira yake hayakuwa mazuri.”
“Yawe mazuri vipi ikiwa aliyekufa ni mzazi wangu?”
“Sawa mzazi wako lakini unajua kifo chake kilitokana na nini, Na dada yako baada ya kifo cha baba yenu maneno aliyokuambia,
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi