BABA KIUMBE WA AJABU (4)

Zephiline F Ezekiel
BABA KIUMBE WA AJABU (4)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA NNE TULIPOISHIA... Nilimuhadithia baadhi ya mambo kisha nilimueleza ya yeye kulima wakati tuna pesa. “Eti mama hata kulima kwako amesema ni imani za kishirikina iweje tuwe na pesa wewe ulime wakati ungewalipa watu wakatulimia?” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... “Mmh, mbona makubwa!” Mama alizidi kushangaa. Mama alisema huku akitoka shambani na kunisogeza chini ya mwembe. “Masalu wewe hayo unayaamini?” “Siwezi kuyaamini japo kuna mengine yana ukweli.” “Nakuomba asikubaliane na maneno ya Monika ni ya uongo.” “Mama mbona baba alisema jana litakalomtokea asilaumiwe , nini kitamtokea dada Monika?” “Wee Masalu!” Mama alizidi kushtuka kuona ninajua vitu vingi. Ilionesha mama aliamini siyajui mengi kuhusiana na mambo yaliyokuwa yakitendeka nyumbani. Nilimuona akifuta jasho kwenye paji la uso kisha alinipandisha na kunishusha na kusema. “Masalu wewe ni mtoto, …