BABA KIUMBE WA AJABU (7)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA SABA TULIPOISHIA... “Nimekuelewa mama yangu, nimekuelewa sina budi kukusikiliza.” “Asante Masalu, siku zote niliamini wewe na Monika ndiyo watoto wangu wanaonijali, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... endelea kunijali mwanangu wewe ndiye tegemeo langu, soma unikomboe.” “Nitafanya hivyo mama yangu, nakuahidi kuwa kimbilio lako.” “Asante mwanangu.” Baada ya mazungumzo marefu tulirudi nyumbani, lakini bado aliniacha na maswali lukuki moyoni mwangu, nilijikuta nakubaliana na shemeji, bwana wa Monika kuwa mwili wa dada umefichwa ndani pamoja na mtoto wa dada Mihayo . SIKU TATU BAADAYE Siku tatu baadaye nilipata taarifa za kusikitisha za kifo cha utata cha shemeji aliyekuwa bwana wa Monika. Taarifa zilizonitisha na kuamini mazungumzo yangu na mama juu ya taarifa zinazosambazwa na shemeji zilimfikia baba na kuamua…