BABA KIUMBE WA AJABU (9)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA TISA TULIPOISHIA... Nilishindwa tena kumueleza kitu chochote, nilibakia kupelekwa kama mkokoteni usio na breki. Tulipoingia ndani mpenzi wangu alionekana na shauku kwa kunivamia kutaka mapenzi. Nilijiuliza nitawezaje kumkatalia tusifanye mapenzi ikiwa tayari ameishalipia chumba? JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... Nilijiuliza kama nikifanya mapenzi itakuwaje, nilijikuta nikisemea mwenyewe “Liwalo na liwe” niliamua kufanya mapenzi siku ile. Kilichomshtua mpenzi wangu ni kitambaa nilichokuwa nimejifunga mguuni. “ Masalu nini hiki?” “Niliumia,” nilidanganya. “Sasa mbona umejifunga kitambaa badala ya dawa?” “Natumia dawa za asili .” “Ulifanya nini?” “Niliumwa na nyoka wa maajabu .” “Una maana gani?” “Nilikuwa nimelala ndani nikaota naumwa na nyoka.” “Enhee.” “Nilipoamka si ndiyo nikakuta natokwa damu.” “Mungu wangu, baada ya hapo ikawaje?” “Nilikimbizwa hospital…